"Saa nyingine ni vitu vidogo vidogo tu ndo vinavyotengeneza mshiko
mkubwa kihisia, sifa moja ya akili au ishara ndogo tu inaweza kumshika
kihisia mwanamke, vile vile ukitoa sifa mbaya ndo mwisho wako!."
Mwanamke hutumia muda mdogo sana kuamua kama una uzito wowote wa
kumfanya yeye atoke na wewe kutokana na vitu vidogo vidogo unavyofanya
na vile ambavyo huvifanyi ndo vinamsaidia kufikia kwenye maamuzi yake.
kiumeni.com imejaribu kukusanya njia rahisi za kumshika kihisia mwanamke
ambazo sio ngumu wala za kupoteza mda na zitatoa tofauti kubwa kati ya
kuangaliwa vibaya na kupewa namba ya simu...
- Msifie kwa kitu kizuri...
Ukimwambia mwanamke
anaharufu nzuri inayosambaza furaha, kutamfanya ajisikie vizuri, harufu
ya furaha ni harufu ambayo kila mtu anatamani kuwa nayo kila saa, hii
itakufanya upate wasaa wa kumuuliza vitu gani kwenye maisha yake
vinavyomfanya awe na furaha?, ambapo swali hili litamfanya avutiwe zaidi
na maongezi yako na kujisikia vizuri zaidi, ukimsifia kwa kitu kizuri
unakua mwanzo mzuri utakaokupa fursa na nafasi nzuri zaidi ya kuendelea
nae kimaongezi.
Wanawake wanapenda sana kutoa ushauri na wanavutika zaidi kwenye njia
hii maana utamfanye apate hisia umeona kitu kizuri kwake mpaka ukampatia
hio heshima ya kumuomba ushauri, kuwa mwangalifu hapa maana hautakiwi
kuonekana kama haujui kabisa juu ya kitu unachomuomba ushauri na
hakikisha usifanye asijisikie vizuri.
Ukiwa unaomba ushauri onyesha na wewe ulikua unafikiriaje juu ya hicho
kitu au jambo ulilokua unaombea ushauri, na maswali yawe ya urahisi
ambayo atatoa majibu kwa urahisi zaidi na hatimaye kuanzisha mazungumzo
mengine.
- Msifie kwa jinsi anavyoonekana...
Unatakiwa wakati ukitoa sifa, sifa ionekane ni ya ukarimu na sio
vinginevyo, kwa hio inabidi utoe sifa ambayo ni ya asilia, kwa mfano
usitoe sifa kama "Unamacho mazuri sana!", jaribu kusema "umependeza
kwenye hio nguo uliyoivaa!". Ni njia nzuri ya kumwambia kuwa ni mrembo
kuliko njia ya kwanza ambayo inaonyesha wazi sehemu mazungumzo yako
yanakoelekea.
Kumfungulia mrango mwanamke ni kitendo cha kiungwana sana, jionyeshe uungwana wako.
Ukiwa unataka kumjua msichana ni lazima ufanye unachoweza ili kumfanya
ajisikie vizuri, hii inamaanisha kuelekeza maongezi kwenye mambo ambayo
ukiiyaongelea atajisikia vizuri na kwenye mazingira aliyoyazoea, unaweza
kuelekeza maongezi yamuhusu yeye mwenyewe, wanawake wanapenda sana
kujiongelea kuhusu wao wenyewe.
Ukimuuliza maswali juu ya maisha yake ya zamani na vitu anavyovipendelea
utamfanya aongee kwa kujiamini zaidi, huku ukionyesha hamasa zako zipo
sio tu kwa ajiri ya muonekano wake.
Hakuna kitu kibaya kinachoonyesha mtu ulienae hana umuhimu kama kupokea
simu au kusoma meseji katikati ya maongezi, ukiwa unaongea na msichana
fanya akuone kama kuna mtu anakupigia na uikate simu mbele yake na
kizima kabisa, akikuuliza kwanini umefanya kitendo hicho, mwambie
mazungumzo yake yamekuvutia na unataka umsikilize yeye kwanza mengine
hayana umuhimu, utamfanya ajisikie na thamani kubwa sana kwako.
- Ongea na marafiki zake na jihusishe kwenye mazungumzo yao...
Ukiwa unafikiria kumtongoza msichana, lazima utakua unatathimini utu
wake, muonekano wake na mengineyo kama uwezo wake wa kuelewa mambo na
kufurahi, ndivyo hivyo hivyo mwanamke nae anatathimini, na hututathimini
ni kiasi gani ambacho tunaendana na jamii yake.
Wanawake huvutiwa na mwanaume mcheshi, anayependeka kwa urahisi na ni
mtu wa kijamii, kwa hio jiingize kwenye maongezi na rafiki zake na
ukiweza kuwavutia rafiki zake, utakua umemvutia na yeye pia, hakikisha
kipindi chote cha maongezi, uwe umeweka wazi kwamba yeye ndio vutio lako
kubwa.
- Kuwa katika hali ya usafi na uvaaji mzuri na wakupendeza...
Wanawake wanapenda wanaume watanashati, wanapenda kuwaona wakiwa wanapendeza na kunukia vizuri mda wote na nywele zilizo katika hali nzuri.
Hembu fikiria wewe unawatathimini wao kwa muonekano, kwa nini na wao wasifanye hivyo vivyo?.
Ni majaribu makubwa kutomwangalia mwanamke mzuri toka juu mpaka chini,
anavyokua mzuri zaidi ndivyo ilivyo ngumu kuweka akili yako kwenye
maongezi, hakikisha unamwangalia machoni, akikukamata unaangalia maziwa
yake wakati anakupa stori kuhusu mama yake ujue atakuona kuwa wewe ni wa
ajabu sana na moja kwa moja atajua umekuja kwake kwa ajiri ya kilichopo
katikati ya miguu yake tu.
No comments:
Post a Comment