a
wala hii haikufanyi usiwe wewe ulivyokuwa juzi. Amka watafute watu
waambie ni jinsi gani umeumia, toa machungu yote ya nafsini
mwako,inatokea kwa watu wengi Na wewe sio wa kwanza na wala sio wa
mwisho.
Usiamini kupita kiasi
Mapenzi
hayazuiliki ni kitu kinachokuja na kufunika moyo wako bila taarifa sio
rahisi kucontrol mapenzi juu ya mtu fulani. Lakini unaweza kucontrol
kumuamini mtu mwingine. Katika dunia tuliyonayo ni nadra kupata mtu
mwenye mapenzi ya dhati,usimuamini sana amini kuWa ni tabia ya wanadamu
kuchoka Na kutafuta vilivyo bora zaidi. Sisemi usiamini ila siku zote
amini lolote linaweza kutokea itakusaidia siku ikiwa ndivyo sivyo.
Kusalitiwa hakuondoi thamani na utu wako
Baada
ya kumfanyia yote uliodhani unamfanyia ili aendelee kukupenda lakini
ameondoka, roho inakuuma sababu unaona hakumbuki jinsi gani ulivyojitoa
kuhakikisha ana furahi na kuwa na amani siku zote. ii haiondoi ile asili
na thamani ya utu wako maisha. Ni vile tu huna habari ila yamewakuta
wengi na yataendelea. Kwanini wewe uone sio mtu tena, kwanini uone labda
wewe sio mwanaume tena? Kwanini uone eti pengine uanamme wako una
walakini Na sio yeye ndo mjinga kwa kutojua thamani ya penzi lako.
Amini anayekuja ni bora kuliko aliyeondoka
Ambacho
hukijui ni kuWa kuna wanawake mamia kwa mamia wanasubiri mwanaume wa
dizaini yako atokee ili kukamilisha maisha yao. Na ni bora kuliko
aliyeondoka na watathamini mapenzi yako kuliko aliyekutenda. Jipe sababu
ya kuamini wewe ni kama dini lililokuwepo enzi za babu zetu likichezewa
bao mpaka mkoloni alipokuja kuwaonyesha thamani na matumizi sahihi ya
madini!
Hautakiwi uache kupenda, hautakiwi upunguze juhudi za kumuonyesha mtu kama unampenda. Haijalishi ni mara ngapi unaumizwa unapofanya mazuri kwa mtu fulani usitegemee kitu hicho hicho kutoka kwa huyo mtu ila amini ni hazina uliyojiwekea na kuna siku utapata thamani ya penzi uliloliwekeza.
Hautakiwi uache kupenda, hautakiwi upunguze juhudi za kumuonyesha mtu kama unampenda. Haijalishi ni mara ngapi unaumizwa unapofanya mazuri kwa mtu fulani usitegemee kitu hicho hicho kutoka kwa huyo mtu ila amini ni hazina uliyojiwekea na kuna siku utapata thamani ya penzi uliloliwekeza.
No comments:
Post a Comment