"Facebook ni sehemu nzuri ya kukutana na wasichana, ila ikitumika vibaya
ni moja kati ya sehemu mbaya inayopunguza nafasi ya kuwa na msichana
yoyote yule".
Kuna sheria ndogo ndogo na taratibu ambazo kiumeni.com itakupa zinabidi
zifuatwe ili kukuongezea wigo wa uhakika wa kumpata msichana facebook,
na iwapo ukizingatia vizuri na ukaweka umakini utashangazwa na
mabadiliko utakayotokewa na kuyaona...
- Usimtumie mwaliko wa urafiki mapema mno...
Wapo wanaume wengi wanaomtumia mialiko mingi ya kumuomba urafiki, kwa
hio hakikisha usiwe mmoja wao, jaribu kutumia njia mbadala kama
kukomenti kwenye komenti za marafiki zake anazo zikomenti na yeye, na
hakikisha unakomenti kwa utata ili akujibu na tafuta rafiki yake ambae
pia ni rafiki yako ili aweze kuwatambulisha, na kama kuna uwezekano wa
kukutana nae nje ya facebook ni vizuri ukafanya hivyo kabla ya kutuma
mwaliko wa urafiki ili mpate kujuana kwanza, hii itaongeza wigo zaidi na
uhakika wa kuwa karibu.
Kumpoke mtu ambae hakufahamu vizuri mara nyingi huwa haviendani, kwanza
huyo msichana atakuona wa ajabu sana mpaka unashindwa kusema "Mambo?" au
sana sana anaweza akakupuuzia tu, na tofauti na hapo poke inauwa chachu
ya kuanzisha mazungumzo.
- Usijishushe na kuonekana mpumbavu...
Kama hakujibu meseji na chati zako ulizotuma kabla au komenti
ulizoziacha kwenye kuta za kurasa yake ya facebook, ni vizuri ukamwacha
kwanza mpaka akujibu mwenyewe.
- Fikiria kama vile kila mtu anaemjua yumo facebook...
Hapa tunamaanisha kila mtu, bibi yake, bosi wake, mwalimu wake, mama
yake, hii inamaanisha usiandike kwenye kuta wa kurasa yake mambo ambayo
hayaendani au usimwoganishe jina lake kwenye picha ambayo haina
muonekano mzuri, iwapo ukimdhalilisha mbele ya jamii yake sidhani kama
utakua na nafasi tena kumpata.
Sio kwa sababu ulishamchunguza kwenye kurasa yake na kugundua anachopendelea
na wewe ukajifanya una hobi hizo hizo na kuwa wa kwanza kuvisema kwake,
ukifanya hivyo utaharibu, ni vizuri ukamuuliza au mwache mwenyewe mpaka
atakapokuambia kwa maneno yake.
- Toa uhusiano kwenye mtandao...
Baada ya muda ni vizuri utoe uhusiano kwenye mtandao na uende nje ya
facebook na kukutana ana kwa ana, iwapo ukitumia muda mwingi wa
mawasiliano kwa njia ya mtandao, itakua ngumu kuuleta uhusiano katika
hali ya kawaida ya kidunia.
No comments:
Post a Comment