"Tunajua ni rahisi kuamini wanawake wote ni vichaa, hawakuelewi, hawajui kipi wanahitaji na mengine mengi!".
kiumeni.com tunaweza sema pole kwa bahati mbaya ulionayo, iwapo kama
bahati ingekua kweli ndo inasababisha wewe kuachwa kwa kila uhusiano
unaokuanao, tukiendana na ukweli kabisa, sababu ipo kwa yule
unaemwangalia kwenye kiio kila mara ujiangaliapo, haiwezekani wewe kuwa
unaachwa kwenye kila uhusiano unaokuanao na kusema sababu sio wewe.
Sio kusema kuwa wewe ni mtu mbaya au una sura ngumu kushinda wengine,
hapana!, ila unakua unarudia kufanya maamuzi mabaya pamoja na kuwa na
tabia flani flani mbaya ambazo zinasababisha haya kwa kila uhusiano unao
ufanya na wewe kujikuta ukiachwa, kuna baadhi ya makosa kwenye uhusiano
unajikuta unafanya bila ya wewe kujua.
Kama unataka kujua kwanini kuachwa ni kitendo kinachokua kinakutokea kwenye kila uhusiano, soma hapa na uone kama haya mambo ni mapya kwako...
- Unamuhitaji mpenzi wako kupita kiasi...
- Una wivu unaopitiliza...
Weka akilini sio kila mwanamke sio mwaminifu, "jiamini" na "jiamini unapendwa".
- Hauchukui wajibu kwenye makosa yako...
Ukitaka kukaa na msichana kwenye uhusiano na uendelee kwa muda mrefu jifunze kuchukua wajibu kwenye makosa yako.
- Unajishusha kwa kila jambo...
Wanawake wanapenda watu wenye msimamo na wanaojiamini,
mtu anayeweza kuongoza familia, kama akikuacha akaondoka naomba
usimshutumu maana nae anatafuta mwanaume aliye bora ambae hata kama
akianzisha familia nae anaweza kuiongoza familia.
- Haubagui...
- Hisia zako ziko juu mno kupita hali ya kawaida...
Kama unaendelea kuachwa katika kila mahusiano uliyonayo, ni vizuri
ukaanza kuchunguza na kuangalia nini unakosea na kurekebisha tabia
zinazopunguza hisia na hamasa kwenye mapenzi, ni muda wa kuanza kufanya
mabadiliko, kama kauli mbiu ya kiumeni.com, "badilika na kuwa mwanaume
mtanashati".
No comments:
Post a Comment