"Je upo kwenye uhusiano wa mapenzi na mtu maalumu ambaye hutaki kumpoteza?, Je unapata hisia mbaya na unahisi kunakitu hakiko sawa maana kila ukitaka kumbusu mpenzi wako au kukaa nae muongee hana hisia tena kama alizokuanazo awali, kila kitu anakuwa na kisingizio na mizungusho mpaka unapata hisia labda kuna mtu mwingine katikati?".
Nikitu gani unachokijua ambacho wanaume wanakifanya ila wanawake
hawakifanyi?, unajua ni nini?, wanaume hupingana na hali halisi katika
sehemu mbili za maisha yao, namba moja; huwa hawaulizi njia inaelekea
wapi au mahali walipo pindi wapoteapo njia na namba mbili; huwa
wanadhani wanawake wote hawaeleweki wala hawaendani nao.
Watu hawa kamwe huwa hawajiulizi kwanini baadhi ya wanaume wengine huwezi kukuta wamekataliwa na mwanamke
au wameachwa na mwanamke, je inawezekana kwamba baadhi ya watu hufanya
makosa kwenye mahusiano na makosa hayo hujirudia kutoka uhusiano mmoja
kwenda mwingine?, au inawezekana kwamba uchaguzi wa wanawake katika
wanaume si dhabiti?
Muongozo;
Wanaume walio na mafanikio kwenye mapenzi huwa hivyo sio kwa sababu ya
bahati, ila ni kutoka na kutumia kanuni za kuaminika na kuwa na mipango
thabiti.
Kiumeni.com
imekuandalia kanuni thabiti ambayo unatakiwa uifatilie vizuri na
kuielewa maana ndo itakuwa nguzo kuu ya mafanikio katika mahusiano yako
ya kimapenzi na kukufanyia mabadiliko makubwa ya utanashati.
Kanuni; Kuwa na chamgamoto.
Hamasa au mvuto wa mwanamke kimapenzi ni kitu cha muhimu sana cha
kuangalia iwe wakati unamtongoza mwanamke au uko naye tayari katika
mahusiano, wakati unamtongoza
hamasa inakuonyesha kiasi cha uhakika ulionao kukubaliwa au kukataliwa,
na katika mahusiano huonyesha kiwango cha mvuto wa kimapenzi
alichonacho mwanamke juu yako, hamasa hupungua na kuongezeka kutokana na
jinsi wewe unavyoendesha mapenzi na mpenzi wako, kanuni kuu ya kuongeza
hamasa ni jinsi unavyotoa changamoto kwa mwanamke.
Changamoto ni kitu ambacho wanawake wanakitaka na ndicho kitu pekee
kitakachomfanya mwanamke akae kwa muda mrefu, tuchukulie mfano umekutana
na msichana mpya na mnaanza kuongea, maongezi yanaendelea na yanazidi
kuwa matamu, unaanza kumwelezea kuhusu maisha yako pamoja na mahusiano
yako ya kimapenzi yaliyopita, na kumgusia juu ya wapenzi wako wa zamani
na mahusiano yako kwa ujumla na kwa jinsi anavyokusikiliza unajua kabisa
mpo ukurasa mmoja kwa mambo mengi mnayoyaongea, mpaka kufikia mwisho wa
maongezi umeshamwambia kila kitu kuhusu wewe, kwa hio kwa hapo unakua
umeshamaliza changamoto yeyote uliokuanayo.
Naposema umeshamaliza changamto namaanisha hutakiwi kuwa muwazi sana,
kama kaka yangu Abel anavyosema "Ukiona maongezi yamekolea na
anakuangalia kwa jicho la husuda, kinachofuatia ni kuaga ili umwache
anakufikilia.
Haimaanishi unampenda kiasi gani, unachotakiwa kuangalia ni kiasi gani
upendo wake unavyoongezeka kwako na jinsi anavyoanguka kwenye mapenzi
yako, ongoza matendo yako na maongezi yako, hakikisha haumsimulii mambo
yako yote, mwache mwenyewe atafute na kufungua kurasa moja hadi nyingine
ya maisha yako, kuwa changamoto kwa kumpatia kitu kitakachomfanya
akufikilie, mwanaume kiongozi
anatambua changamoto ni sehemu kubwa ya mahusiano ambayo kipindi hiki
wengi huwa hawazingatii, kwahio kama upo kwenye mahusiano ila unaona msichana wako amebadilika
inatokana na kushuka kwa hamasa yake kwako, na hamasa ikishuka sana,
tukichukulia hamasa kwa asilimia 0 mpaka 100%, na ikawa imeshuka chini
ya asilimia 40% atakua anakuona kama unamboa na ni kitu cha kawaida kwa
wanawake maana wanahitaji changamoto kwa wakati wote, na ikishuka sana
chini ya asilimia 30% lazima atataka muachane.
Kwahiyo unawezaje kuwa na changamoto muda wote?
Unachotakiwa kufanya ni kufanya hamasa yake juu yako iwe katika kiwango
cha juu muda wate na si vinginevyo, lazima uonyeshe kujiamini na
kujiheshimu kwa hio usije pitiliza na kujinadi sana na kitu kimoja
naomba ufahamu kujinadi ni kuzuri kwa yule mchekeshaji mwenye uelewa na
ujuzi mkubwa na wanawake, na ameshakuwa na wanawake wengi na
anachohitaji zaidi ni ngono pekee.
Jiongoze kama mwanaume kiongozi
, namaanisha tunza hisia zako na hakikisha zipo chini ya muongozo wako,
kama ulikua mtu wa kumuhitaji sana kila muda jaribu kumpa nafasi, kama
shemeji yangu anavyosema "Huwezi kukitamani kitu mpaka kipotee", na si
maanisha usionyeshe hisia zozote kama jiwe ila weka uwiano na hasa
katika mitoko yako ya kwanza.
Kujiheshimu na kujithamini ni sehemu kubwa ya kujiamini,
kujithamini ni nguvu chanya na itakupa mwongozo mzuri kwenye uhusiano,
kama haujiamini kwanini mtu mwingine akuamini?, tuachane na yote hayo
mwisho wa kina ni kwamba muonyeshe mpaka ulipo, ila sio kwa kumwambia.
Kuwa na maamuzi kwenye uhusiano na unatakiwa ufanye maamuzi ambayo na
kwako pia yanakunufaisha, na kama unamaamuzi yote kwake basi rafiki hapo
ni mteremko tu.
mwanaume kiongozi
anajiamini na anajithamini kwa hali ya juu na kufanya maamuzi ndani ya
mahusiano kwa umakini zaidi na saa zote anaziongoza hisia zake na kama
ukifanya hivi sawa, huyo msichana atakupenda daima na labda ndo atakaevalishwa ile pete.
No comments:
Post a Comment