"Hataki muwe zaidi ya hapo, anakuchukulia kama rafiki!"
Stori inakwenda hivi; baada ya kumwangalia kwa muda mrefu, huyu
mwanamke
anambae anakuuwa pole pole kwa mvuto wake, ambae anakila kitu ambacho
wewe macho yako kwako unaona ndo kile kinachoitwa na kutengeneza uzuri
usiopimika, ubongo wako unaamini ya kuwa mnaendana kwa kila kitu ila
kinachokuchanganya ni wewe kutokua na uhakika iwapo na wewe unampendeza
yeye, Kijana wa watu unajituma na kupiga moyo konde, leo hii unajikaza
kiume na kwenda kumwambia yale yote yaliyo moyoni mwako... mara...
'kwaaa...' anakujibu, "Oho, lakini mbona mie siku zote huwa nakuona na
kukuchukulia kama rafiki, kama rafiki.. rafiki tu!", moyo unapigwa na
radi ya maumivu, na huamini kilichokupata, huku kichwani sauti ya "kama
rafiki" ikijirudia rudia!.
Kama kungekua na kitu cha kuzuia hii dhihaka, ungetumia na kurudisha
muda nyuma, kiume.com tumekusanya dalili zote za kuangalia kabla ya
kupiga moyo kode na kwenda kumwambia yanayokusibu moyoni...
- Anajiamini sana akiwa na wewe mpaka mazoea yake yamepitiliza...
Msichana akiwa anajiamini sana kwako, ujue hapo umeshapoteza
unachotamani na umeishia kunawa, kwa msichana akimuona mtu anayempenda
kweli, utaona dalili...!, utaona hatulii, mara akae vizuri, na anakua
anajihisi tu mda wote, atashika nywele zake kuangalia kama ziko vizuri,
mapenzi asikuambie mtu kaka, mapenzi yanaleta kutokujiamini, na iwapo
anajiamini sana kwako na ashtuki akikuona, wala atikisi hata ukucha basi
hapo tafuta kitu kingine tu cha kufanya.
- Anakupa hadithi za wanawake wengine...
Msichana ambae yupo singo hana mpenzi, halafu ukiwa nae anakua
anakupa stori za wasichana wengine, hapo anatumia janja ya nyani, hapo
anakubadilisha akili usimwazie yeye na uwawazie hao wasichana wengine
anaokupigisha stori, achana kabisa na haya maongezi, anaweza kukwambia..
"ooho, unaonaje nikikupigia pande kwa rafiki yangu Janeti, si ni mzuri
eeh?", kaka hapo unapoteza mda tu.
- Hafanyi kile unachotaka...
Ukiona msichana hasikilizi kile unachotaka, yeye siku nzima anakuomba
umsaidie hichi, twende pale.., we ukimwambia ya kwako anaruka maili
tisa, ujue hapa huna chako, we upo pale ili akutumie tu na kwa sababu
hana hisia nawe hajiulizi hata huyu jamaa anajisikiaje!.
- Anatukana bila kujari uwepo wako...
Maneno anayotumia ni kama yupo na
mwanamke
mwenzie, na wala hashituki!, kaka hapa umeshakwenda na maji, mapenzi
yana heshima na anayekupenda huwa anashituka akiona tu uwepo wako, na
aibu yake sikuzote hua ipo karibu.
- Hataki kuonekana na wewe sehemu za wazi...
Ukimwambia tutoke wote, anakua na visingizio. Ukimwambia twende wote
nikusindikize uendako, hata kama ni sokoni... utamsikia "ohhoo, mi
nilishazoea kutembea mwenyewe wakati wote, mama atanielewa vibaya". Hapa
ni kwamba anaogopa utamwalibia chansi ya kukutana na mwanaume wa ukweli
achana na wewe masuruali tu, mama gani ambae hapendi mwanae aolewe?.
- Anakuomba misaada mda wote...
Msichana mwenye hisia nawe hawezi kukuomba misaada ovyo
hovyo, kwanza atakua hajiamini na hujiuliza maswali kama "Hivi
atanionaje na atajifikiliaje nikimuomba hiki?".
- Anakufanya kama spea tairi...
Siku akikubali kutoka mtoko nawe, utashangaa kaja na mashoga zake!, hii
anakua anafahamu kabisa kwa hio anakua anajihami ili usije ukapata
chansi ya kuwa wewe na yeye. Yeye saa zote ni vicheko tu..., kidogo tu
mara anaenda chooni, mwisho wa siku mbaba unaagwa usiku umeingia sie
tunaenda.
- hafanyi michezo yeyote ya kuwa karibu nae...
Mwanamke akikupenda anatamani saa zote awe karibu nawe, mara mjikute
mmeshikana mikono mda mrefu mpaka jasho, sasa huyu yeye atakua anakulia
taimingi, anakua anahakikisha hakuna mguso wa ajabu ajabu, kaka mguso
huleta hisia, na kama hana hisia kwako hawezi kufanya hivyo.
- Anaongea na wanaume wengine mbele yako...
Hivi hili si linaonekana kabisa, hili halina haja hata la kuliongelea,
ila mtu akiwa amependa inawezekana kabisa asilione hata hili, anakua
anajipa matumaini hewa!, huku kichwani akilipa sababu nyingine kabisa,
"Oooh yuko sosho sana!".Kaka hapo kama msemo wa kiumeni.com usemavyo,
"umeshaliwa kekundu".
- Hakutambulishi kwa rafiki zake...
Hana hisia nawe atakutambulisha kwa nini?, labda kwa sababu vocha zote
zinatoka kwako!, samahani kwa kuongea hivi najua nakukera ila ndo ukweli
wenyewe, na hata ukitambulishwa, utatambulishwa kama
rafiki tu, na hivyo ndo utabaki kuwa.
Cha kufanya jiongeze, na hata kama yeye ndo huwa anakupigia simu au
anakufata na anaonyesha hisia ujue kuna kitu zaidi ya wewe
kinachoendelea kumweka kwako.
No comments:
Post a Comment