Raha ya mapenzi!!!!! |
Fanya itokee siku moja asubuhi mnapoamka halafu mwambie kuwa alikuwa anakoroma usiku, kisha utashangaa na kugundua baadhi ya mambo mengine kuhusu mwanamke.
Kutoka
katika blogi moja ambayo imebobea katika kujadili mambo mbalimbali yanayo
zunguka ulimwengu (Dunia) ya Al-amini blogspot, leo nikakutana na baadhi ya mambo
ambayo katika ulimwengu huu kumbe wanaume hawayajui kuhusu wanawake, licha ya
kuwa wanaume wamezaliwa nao, kukuzwa na wanaishi nao.Tafsiri iliyotumika
yaweza kuwa sio rasmi, lakini imelenga zaidi katika kufanya mambo kueleweka.
Ombi langu kwako ni kufanya utafiti kisha utakubaliana na mimi au laa!!
1. Wanawake eti siku zote hawana kitu maalum cha
kuvaa. Na ndio maana wawezakuta katika kabati la mwanamke limejaa nnguo na mahenbegi
kadhaa, lakini asubuhi analalamika hana nguo ya kuvaa.
2. Wanawake ni viumbe wenye kupenda kuona kuwa
duniani kuna watu wabaya zaidi yao, na ndio maana vipindi vingi vya kuelezea
mikasa ya kinamama walioonewa vinapata umaarufu sana duniani.
3. Wanawake daima si watu wa kukosea. Huamini
kuwa, makosa wameumbiwa wanaume tu, na ndio maana wao hata wakikosea, kuomba
msamaha ni kwa bahati mbaya japo wakikosewa wasipoombwa msamaha ni tatizo kubwa
sana. Hujachunguza?
Sorry baby "wapii" |
“ Hapa unajaribu kumuomba msamaha lakini
anaonekana kuleta mapozi ya kike, ila anapenda kuombwa msamaha”
4. Wanawake ni wenye kupenda kulia sana tena
kila wakati. ILA hawawezi kufanya hivyo kama haupo karibu nao au kama huwezi
kusikia kilio chao wanapolia.Chunguza utagundua
5. Wanawake hupendelea sana kufanya manunuzi, maana hili ni moja
kati ya mambo ambayo wanaamini wana udhibiti nayo kuliko jambo lolote duniani
“Utamsikia
akikwambia sina viatu kabisa.....wakati vyengine havina pakukaa, ila mwanaume pea nne za viatu zinaweza kumchanganya”
6.
Wanawake wengi hupenda kuuliza swali la “Je, naonekana vipi hapo?”,
“nimependeza?” japo ukweli ni kwamba hawapendi majibu ya kweli kuhusu swali
hili. Mwambie hujapendeza “Utakiona kizaa zaa”
7. Mwanamke anaweza kujipamba akapendeza hata
kama anaenda kufanya kazi ya kunyweshea bustani, kusoma kitabu, kwennda jikoni kupika
au kutazama tv. Anaweza kukaa mbele ya kioo chake kwa mda ili apate kupendeza.
Wanasema mwanamke Urembo
8. Mwanamke anaweza kuendesha gari umbali wa
maili hata 100, kwa hofu tu ya kupotea kidogo endapo atatumia njia ya mkato
yenye uwezo wa kupunguza safari yake kwa maili 50 nzima
9. Wanawake hupenda sana kuongea kwa simu.
Anaweza kumtembelea rafiki yake na kuwa naye kwa wiki kadhaa, na anaporejea
kwake muda mfupi baadae akampigia rafiki yuleyule na wakaongea masaa zaidi ya
matatu kwenye simu.Chunguza utabaini?
10. Wanawake hupendelea kuchana nywele zao
kabla ya kulala. Jiulize kwanini sasa na utaambiwa wewe hujui kitu.
Hahahahahaha!!!
No comments:
Post a Comment