Mafanikio
ni kitu cha ajabu sana, wakati watu wengi wa kiangalia pesa kama
mafanikio wapo watu ambao huangalia kuwa na furaha katika mapenzi kama
mafanikio, mimi naangalia kufanya kitu ninachokipenda kama mafanikio.
Napenda kuandika na naweza kukaa kutwa nzima bila hata kukumbuka chakula
nikiandika tu.
Kwangu
kuandika kitu na watu wakakisoma ni mafanikio bila kujali napata pesa
au la. Katika maisha ukianza kupima mafanikio yako kwa kuangalia kiwnago
cha pesa unayoingiza basi jua unaelekea kubaya, iwe ni kazini, katika
biashara au katika mapenzi.
Hii
ni kwasababu kuwa kama unasukumwa na pesa basi unaweza kufanya kitu
chochote kile ili tu kupata pesa ya zaida lakini kama unasukumwa na
upendo wa kile unachokifanya basi nirahisi kufika mbali kwani utakifanya
vizuri na siku zote pesa hufuata vitu vizuri.
Labda
nitoe mifano mitatu katika mambo matatu, kwaza ni katika kazi, pili ni
katika biashara na tatu ni katika mapenzi. Katika kazi kwa maana ya
ajira, kama akili yako ikiwaza pesa tu, yaani nunafika ofisini badala ya
kuwaza majukumu yako unawaza pesa tu nirahisi kwanza kuharibu kazi za
watu, pili kuingia tamaa za rushwa na tatu kuipoteza kazi yenyewe.
Ukisha
pata pesa utawaza kuzitumia na si kutimiza majukumu ambayo ndiyo
yalikusababishia kuzipata hizo pesa, hii ni mbaya kiajira. Lakini katika
biashara ni rahisi kumuuzia mteja kitu kibovu kwakua tu unataka pesa na
ukishafanya hivyo mteja akifika na kukutana na kile kitu kibovu basi
inakuwa ndiyo mwisho wake kurudi kwako na unaweza kuwa ndiyo mwisho wa
biashara yako.
Tukirudi
katika mapenzi, kama akili yako iko kwenye pesa tu basi unaweza
kujikuta unakuw atayari kufanya mapenzi na mtu yeyote yule kwakuw atu
anapesa. Unaweza kufanikiw akuzipata lakini kwa gharama gani? Ubatya wa
pesa za namna hii inakufanya kuw amtumwa wa ngono, kwamba ili ueendelee
kupata pesa inabidi ufanye mapenzi na wanaume wengi au wanawake wngi
ambao hawakuvutii ili kutimiza mahitaji yako.
Unaweza
kuona ni kitu cha furaha kwa wakati huo lakini kadri umri utakavyokuwa
unaenda na kujikuta hujafaidika chochote zaidi ya kujidhalilisha ndipo
utaanza kujuta. Fanya kitu kwakua unapenda kukifanya na fedha
zitakufuata baadaye ukiwa unafanya kitu ambacho unakipenda. kwa kawaida
pesa haileti furaha bali huahirisha huzuni.
No comments:
Post a Comment