bupropion; hii ni dawa ya mgandamizo wa mawazo ambayo pia hutumika
kutibu watu wanaotaka kuacha sigara, hufanya kazi kwa kuondoa kiu kali
ambayo huipata pale tu anapoacha sigara. mgonjwa hutumia dozi ya 100mg
kutwa mara tatu huku akiendelea kuvuta sigara kisha wiki ya pili mgonjwa
huacha sigara na kuendelea na dawa hizi angalau kwa muda wa wiki saba.
nicotine; hii ni kemikali inayopatikana ndani ya sigara ambayo inamfanya
mtumiaji wa sigara ashindwe kuacha, hivyo wataalamu wameichukua
kemikali hii na kuiweka kwenye jojo au big g ili mtumiaji aweze kuila
kwa kutafuna jojo hizi kama mbadala wa sigara na baada ya muda fulani
apunguze dozi ya jojo hizi mpaka pale atakapokua ameacha kabisa na mwili
kuzoea kuisha bila nicotine. hutakiwi kutumia zaidi ya jojo 20 kwa
ndani ya saa 24.
clonidine; hii ni dawa inayotumika kutibu presha ya kupanda lakini pia
imethibitika kwamba inasaidia watu kuacha kuvuta sigara, matumizi yake
ni kidonge kimoja kutwa mara mbili....unaweza kuanza kutumia dawa hii
siku ya kuacha au siku tatu kabla ya kuacha na kuendelea nayo huku
ukipunguza dozi kwa siku nne mpaka tano. hutakiwi kuacha dawa hii ghafla
kwani huweza kupandisha presha ghafla.
varenicline; baadhi ya watafiti wanahisi dawa hii inafanya kazi kuliko
dawa nyingi za kuacha sigara, hufanya kazi kwenye ubongo kwenye sehemu
inayoitwa kitaalamu kama nicotine receptors kwa kumfanya mtumiaji asione
raha kuvuta sigara lakini pia huondoa ile kiu mtumiajia anayoipata pale
anapokosa kuvuta sigara. matumizi yake ni wiki mbili kabla ya kuacha
sigara na kidonge kimoja humezwa na maji mengi baada ya kula. dawa hii
huendelea kutumika mpaka wiki 12 na zaidi ili kumsaidia mtumiaje aache
kabisa.
notriptyline; hii ni dawa inayotumika kutibu mgandamizo wa mawazo,
ambayo pia husaidia kutuliza ile kiu mtu anayoipata anapokosa sigara.
huanza kutumiaka siku 10 mpaka 28 kabla ya kuacha kuvuta sigara..dawa
hii hupunguza uwezo wako wa kutumia mashine yeyote ya moto kwa kipindi
hiko.. ni vizuri usitumie mashine yeyote ya moto au kuendesha gari.
mwisho; dawa hizi zina madhara madogo madogo na makubwa kama ilivyo kwa
dawa zingine, ni vizuri kabla ya kuanza kuzitumia au kuzinunua uonane na
daktari ili ujue kama wewe zinakufaa kwani kuna baadhi ya dawa hazifai
wagonjwa fulani fulani kama wa moyo, kisukari au madonda ya tumbo.
bahati mbaya hata kuzipata hapa nchini kwetu ni changamoto kidogo lakini
kwa watanzania walioko nje wanaweza kuzipata hata watanzania wa ndani
ya nchi wanaweza kuagiza nje kama wanaweza
No comments:
Post a Comment