Wakati umekutana na mwanamke mrembo halafu ukapiga naye gumzo zuri,
unaweza mwisho kugundua kuwa ana boyfriend. Ama labda una rafiki
mwanamke mrembo ambaye tayari ana mpenzi. Kwa njia yeyote ile, kujua
kuwa mwanamke amechukuliwa kunaweza kukatiza
matumaini. Mwanzo, wanaume wengi hukatizwa tamaa wakati wamezungukwa na
wanawake warembo aina hii ambao tayari wameshachukuliwa.
Kukatiza stori fupi, hapa utakuwa umebakishwa na uchaguzi miwili ambayo
unapaswa kuchagua ikifikia hapa: unaweza kuamua kuachana naye, ama
unaweza kuchukua hatua ya usoni. Sasa hii haimaanishi ya kwamba unapaswa
huuvunja uhusiano ambao tayari yuko nao ama tayari anafurahia. Lakini,
kama anaonekana kuwa hajapendezwa na mahusiano ambayo tayari yuko, ama
umeingiwa na hamaki ya kumtaka awe girlfriend wako, basi kuna hatua
kadhaa ambazo unaweza kuzitumia ili umfanye aachane na mpenzi wake na
akufuate wewe.
Hatua #1 Chambua mahusiano yako
Kabla kuchukua hatua yeyote lazima uchambue mahusiano yake na wewe. Je
anakuchukuliaje? Kama amekuingiza katika himaya ya urafiki, basi tatizo
hapa halitakuwa kwa boyfriend wake bali uhusiano wake na wewe wa
kirafiki. Wanawake huwa na fikra mbilimbili kabla hawajaanza kudeti
marafiki zao wa dhati kwa kuwa hawataki kuharibu uhusiano wao wa
kirafiki nao.
Katika kesi nyingine, wanawake wanakuwa marafiki wazuri na mwanaume
kiasi cha kuwa hawaingiwi na mawazo ya kuwa wanaweza kuwadeti hata kama
wako single. Hii inaweza kuwa kama kesi unayoipitia sahizi. Hili neno
‘friend zone’/himaya ya urafiki linatumika sana na wanaume wengi
wanafanya makosa mpaka wanajikuta wameingizwa katika shimo hili ambalo
ni vigumu kujinasua – hili jambo liko na linakera sana. Kama umenaswa
katika hili jinamizi na ‘friend zone’ na mwanamke unayempenda, basi
fanya hima hima ujinasue na ufuate mbinu thabiti ambazo zitakujeuza
mwanaume tofauti ambaye anaweza kudeti naye.
Hatua #2 Jifanye kama uko single
Baada ya kuchambua mahusiano yenu, anza kufikiria mambo ambayo munaweza
kuyafanya mkiwa pamoja na mambo ambayo hupaswi kufanya akiwa na wewe.
Mfano hupaswi kuleta stori za kumhusu mpenzi wake, ili uweze kumsoma
kiwango gani ambacho anacho ikija kwa kumpenda mpenzi wake.
Kama hamzungumzii kuhusu mpenzi wake mara kwa mara katika maongezi yenu,
basi itakuwa ni ishara ya kwanza kuonyesha kuwa hayuko interested na
yeye sana. Hii itakurahisishia kazi kwako kuweza kumnasa kiurahisi. Kile
ambacho unahitaji kufanya nikumsuka zaidi, ongea na yeye vile ambavyo
anataka uongee naye, na pia mfanye akuone kuwa unavutia kadri wakati
unavyosonga.
Hatua #3 Linganisha ustadi wako wa mahusiano
Wakati huu, nni wakati wa kujilinganisha wewe na boyfriend wake kinjia
fioa, yaani kujipima uwezo wako na boyfriend wake kichinichini. Kwa
kuanza mambo, unapaswa kuongea kuhusu vile ambavyo unaweza kuwa
boyfriend mbaya kwa sababu unapenda maisha sana. Mbinu hii ya maongezi
ni ya viini macho ambayo tuliieleza kwa kina awali katika machapisho
yenu. Huku kutamfanya mwanamke kutaka kujua ni kwa nini unapenda maisha,
na ni kivipi utakuwa boyfriend mbaya kwake. Pia katika mazungumzo yako,
muelezee ni kivipi unayapenda maisha yako na jinsi unavyoishi. Kufanya
hivi kutamfanya mwanamke ajenge picha ya maisha yako akiwa na wewe.
Utamsisimua na kumfanya akuone kuwa maisha yako ni ya furaha wakati
wote.
Kwa kufuata hatua muhimu, unaweza kuiba atenshen ya mwanamke ije kwako,
na kuweza kumuwini mwishowe hata kama tayari ana boyfriend – aminia
hili. Pindi utakapofanikiwa, anaweza kukuonyesha hata dalili za kuwa
ameanza kufall na wewe na kumuacha mwanaume aliyempenda awali kabisa...
No comments:
Post a Comment