Katika mapenzi mara nyingi watu
tunaowapenda hua hawatupendi hivyo tunalazimika kuwa na chaguo la pili
au la tatu. Kwa watu wengi unapojua kuwa mwenza wako kakuoa au kakubali
umuoe kwasababu ya kukosana na mpenzi wake wa awali au kwasababu
ilishindikana kumpata yule anayempenda inakuondolea kujiamini.
Hii inatokea sana kwa wanawake unajua mwanaume alikuwa akimpenda mtu flani, ukahangaikaweee mpaka
akakuoa au hata hukuhangaika lakini baada ya kuachwa tena kwa kuumizwa
ndiyo akaja kwako. Hapo wanawake wengi huanza kutokujiamini na mara
kadhaa kuanza kujilinganisha na yule wa chaguo la kwanza.
Katika mapenzi unapaswa kufahamu kitu
kimoja kwamba kama kakuoa basi wewe ndiyo chagu lake na hakuna cha
chaguo la kwanzaau la pili. Hapa nikimaanisha kuwa kama hakumuoa huyo
ambaye anajifanya kumpenda au anampenda kweli inamaana kuna sababu
ambayo ilifanya iwe hivyo na kuna sababu ambayo imefanya wewe uoe au
kuolewa.
Kwa maana hiyo basi wewe umemzidi hiyo
sababu, labda ni dini, labda ni kabila, labda ni ndugu, labda ni tabia,
labda ni hakuwa akipendwa tu vyakutosha lakini wewe ushaolewa au umeoa
hivyo acha kujiona kuwa hustahili. Usingekuwa hustahili hiyo ndoa wala
asingekuona na kukutamani.
Acha kuishi katika kivuli cha yule mtu
kuwa ukimuona roho inadunda labda watarudiana au labda yeye ana kitu
ambacho wewe huna,jua wewe una ambacho yeye hana na ni huyo mwenza wako
hivyo asikuumize kichwa. Kama huyo mwenza wako anajifanya nayeye
kutomsahau X wake kila siku kumzungumzia muambie ukweli kuwa alimshindwa
kipindi hicho ndiyo sasa atamuweza.
Muambie atulie na kuendelea na maisha
kwani alishashindwa kumpata na kila saa asikukumbushe kumbushe kuwa
ulikuwa chaguo la pili. Asikufanye ujisikie vibaya eti kwakua alikua
anampenda mtu mwingine kabla muambie hata wewe kabla yake ulikua
unapenda mtu mwingine hivyo asikuumize kichwa kwa kushindwa kwake
kumpata aliyekuwa anamtaka.
KAMA HUAUTUMII VYAKULA HIVI NGUVU ZA KIUME UTAZISKIA REDION
KAMA HUAUTUMII VYAKULA HIVI NGUVU ZA KIUME UTAZISKIA REDION
No comments:
Post a Comment