Ushawahi kuwa na rafiki yako, ama una rafiki ambaye tabia zake sikuhizi
zimebadilika? Tabia zake zimekuwa tofauti na kama alivyokuwa zamani?
Rafiki yako huyu umemuona amejeuka ghafla kukupa atenshen yake yote
kwako?
Well, inawezakuwa amependezwa na wewe kiasi cha kuwa anatamani muwe
pamoja. Labda amefall na wewe. Hizi hapa ni baadhi ya mambo unapaswa
kuyaangalia kwa rafiki yako utambue iwapo amekuzimia au la.
#1 Wakati wanapojibu texts zako wanatumia muda mfupi sana ama muda mrefu kupita kiasi. Kama
anakuchukulia kama rafiki yako wa kawaida basi texts ama jumbe zake
huwa anakutumia kwa mwendo wa kawaida. Lakini kama iwapo ana hisia na
wewe utaona ukimtumia jumbe anakujibu papo hapo, yaani chini ya sekunde
moja :) , ama watapiga hesabu ya kila masaa 5 na dakika 24 ndio
wakutumie text nyingine (yaani kuonyesha kuwa wanapendezwa wakiwa karibu
yako)
#2 Wanakutumia text nyingi zaidi. Hii ni dalili moja kubwa kwa rafiki yako. Sana sana wao ndio wanaoanzisha maongezi na pia wanakutumia jumbe kwa wingi.
#3 Kila wakati wanakuuliza kama unapendezwa na mtu. Mara nyingi maswali haya watakuuliza wakati usiku wa kiza umewadia na kila kitu kimetulia, nyinyi wawili pekeenu mkiwa mnachat.
#4 Wanasistiza kuwa hawajapenda mtu kwa sasa. Kwa kawaida watasema haya yote kwa kuwa tayari washayalenga macho yao kwako wakiangalia iwapo utawakubali au la.
#5 Hawamkubali yule unayemzimia ama unayedeti. Ushawahi kuwa
katika deti flani halafu rafiki yako kila wakati anamkashifu
unayempenda? Ama kila wakati unapomtajia mwanaume unayemzimia
anakasirika ama atakatiza maongezi yenu? Well, hii ni ishara ya moja kwa
moja kuonyesha kuwa rafiki yako anakupenda wewe.
#6 Wanakualika muspend wikendi pamoja mkiwa pekeenu. Kama urafiki
wenu pamoja na huyu rafiki yako ulikuwa wa kutangamana na marafiki
wengine lakini ghafla wanakualika muspend Jumamosi nyinyi wawili pekeenu
basi hio ni ishara ya moja kwa moja kuwa kuna kitu kimeanza kupikika.
Mukiwa pamoja na marafiki zenu kuna maanisha kuwa atenshen yote itakuwa
kikundini, lakini mukiwa nyinyi wawili itabakia nyinyi wawili. Ishara ya
kuwa anakutaka uwe wake kabisa.
#7 Mara moja anaanza kukusifia kiundani. Mumezoea kuwa kila
wakati mkiwa pamoja mnaongea kuhusu yule mvulana msiempenda ama habari
za udaku, lakini hii siku moja ameanza kukusifia sifa za kama “Waa!
nywele zako zinanukia utamu.” Halafu hawakwambii jambo hilo tena.
#8 Wanatafuta visababu vya kukugusa.Wakati ambapo umeangusha neno
la kuchekesha, wanakugusa kwa kukugonga mkono. Wakati ambapo
hawajakuona kwa muda wa siku nyingi anakukumbatia kwa nguvu kiasi cha
kuwa unahisi joto lake. Kweli, hapo kunaweza kuwa na mambo
mawili...aidha ni rafiki aliyezoea miguso ama kuna ajenda ya kuwa
amependezwa na wewe.
#9 Watu wanawauliza iwapo mnadeti.Ama pia wanaweza wasiwaulize sababu wanachikulia nyinyi wawili mnadeti.
#10 wakati flani wanaleta mzaha nyote wawili mtoke out pamoja. Wanaweza
kusema “Ok, kwa kuwa leo ni wikendi hatuna kitu cha kufanya. Wewe uko
single na mimi niko single, si tutoke out lakini tuifanye kama deti
vile, twende kwa kwa mkahawa halafu twende sinema tukajienjoy.
Kirafiki?”
Hapa moja kwa moja hamaanishi kuwa ni mzaha bali anataka kujua reaction
yako itakuwa vipi. Ukikubali basi atapata nafasi ya kukusogelea zaidi na
zaidi.
#11 Wanataka mpige picha pamoja. Je hii ni ishara ya kuwa
anakupenda? La. Kila siku watu hupiga picha mara kwa mara. Lakini kama
wataanza kuiweka mikono kwa bega ama kiuno halafu siku ya pili unaiona
kwa instagram, ni ishara ya kuwa anakujali – na labda ni zaidi ya kuwa
marafiki.
#12 Wanakufanyia favour nyingi sana.Kwa mfano anakusindikiza hadi
nyumbani kwenu hata kama mnaishi mtaa wa pili na pia kukulipia bili
zako za hotelini. Anakusaidia kutafuta vitu vyako ulivyosahau pale
ulivyoweka na kadhalika...
Well. Hizi ni dalili daharihi kuonyesha kuwa kuna kitu ambacho rafiki yako anahisi kwako. Je wewe utachukua hatua gani?
No comments:
Post a Comment