Artikel Terbaru

Responsive Ads Here

Thursday, May 18, 2017

Jambo Unalolipenda na Kulitumikia Lina Uhusiano wa Moja Kwa Moja na Kifo Chako


hii inaweza kuwa ni fundisho gani kwa maisha ya binadamu ya kila siku, yapi maoni yako.
Upo uhusiano wa moja kwa moja kati ya kile unachokipenda na kifo chako.  Wazungu wanaita “hobby”, hivyo hobi yako inaweza kuwa njia kuelekea safari ya mwisho wa maisha yako.
Mpenzi wa kuogelea anaweza kuyapoteza maisha yake katika maji, mwanamuziki anaweza kufa kwa kuanguka jukwaani ama chumba cha rekodi, mwanamasumbwi anaweza kufa akiwa na mpenzi, mwendesha gari anaweza kufikwa na mauti akiwa katika usukani vivyo hivyo kwa tasnia zingine na watendaji wake.
Aliyekuwa nguli wa muziki wa dansi mwenye uraia wa Jamhuri ya Kidemodrasia ya Kongo, Papa Wemba, alifariki dunia kwa kuanguka jukwaani akitumbuiza. Janga hili linathibitisha mada yetu ya uwepo wa mahusiano ya kifo katika kile unachokipenda au kazi unayoifanya.
papa-wemba
Tumrejee Paul William Walker  aliyekuwa muigizaji mashuhuri ulimwenguni aliyezaliwa mwezi Septemba 12, 1973 huko Glendale, Califonia, na kufariki dunia Novemba 30, 2013  huko Santa Clarita katika jimbo la Califonia kwa ajali ya gari. Walker alifariki akiwa na rafiki yake Roger Rodas. Kifo cha Paul Walker kiliibua simanzi kwa wapenzi wa filamu ulimwengu. Hisia hizo zilisindikizwa na wimbo wa Wiz Khalifa “See You Again” uliotumika katika filamu ambayo alishiriki Furious 7.

paul-walker
Tuhitimishe na mchezaji  wa mpira wa miguu kiungo wa zamani wa Cameroon, Marc-Vivien Foé ambaye alifariki dunia kwa kuanguka uwanjani na kudhaniwa kazimia lakini taarifa zikathibitika kuwa amekufa baada ya kufikishwa hospitali.
marc-vivien-foe

No comments:

Post a Comment