Utafiti uliofanywa wataalamu wa masuala ya jinsia umeonyesha kwamba kuna mfanano katika hali ya ubongo hususani katika eneo liitwalo hypothalamuskwa wanaume ambao ni mashoga “gay males”na wanawake, sehemu hizi katika ubongo kwa mashoga na wanawake ni kubwa kuliko kwa wanaume wakawaida “straight males”.Ukubwa
wa eneo hili katika ubongo unaaminiwa pia kuchangia katika tofauti za
kijinsia, tofauti za uwezo wakiakili na uwezo wa lugha au kuzungumza. Na
hii ndiyo inayosababisha watafiti wengi kulinganisha uwezo mkubwa wa
kuongea “verbal abilities” walionao wanawake na wanaume mashoga “gay males”.
Hata hivyo zipo tafiti zilizoongeza kwamba kuna maeneo mengine pia
katika ubongo wa mwanaume wa kawaida na mwanaume shoga yanayotofautiana
kabisa kwenye mvuto wa kimapenzi. Tafiti hizi zinaonyesha kwamba eneo
linalohusika na mvuto wa kimapenzi katika ubongo wa mwanaume shoga
huhemshwa au kustuliwa na harufu ya jasho la mwanaume mwenzake wakati
hali hii haipo kwa mwanaume wa kawaida.Tafiti hizi zimehitimisha kwamba
asilimia 35 ya sababu za mwanaume kuwa au kutokuwa shoga, na mwanamke
kuwa msagaji “lesbian” au kutokuwa msagaji husababishwa zaidi na vinasaba “genes” na hizo asilimia 65 zilizobaki hazijapatiwa uhakika wa kisayansi ingawa mazingira yanatajwa zaidi kuhusika – Chris Mauki.
No comments:
Post a Comment