Mwanadamu ameumbwa na kiu kubwa ya kupenda kuwa sahihi, kuonekana
anaweza na pia kujiona kuwa anafaa na kukubalika. Kutokana na ukweli huo
Mwanadamu anajiona kuwa anao wajibu wa kufanikiwa na kukubalika
kutokana na mafanikio ayapatayo katika maeneo
mbalimbali katika maisha yake. Hatari iliopo kwa kila mwanadamu ni pale
anapojikuta ameshindwa kufanikiwa na ili asijilaumu yeye mwenyeawe
anamsingizia mtu mwingine au mazingira aliyopo. Mwanadamu wa kwanza
kushindwa kutii amri aliyopewa na Mungu nakula tunda walilokatazwa
alitoa kusingizio kwa kushindwa kutii amri aliyopewa hebu msikilize
hapa,“ Adamu akasema, Huyo Mwanamke uliyenipa awe pamoja nami ndiye
aliyenipa matunda ya mti huo, nikala Bwana Mungu akamwambia mwanamke Ni
nini ulilolifanya? Mwanamke akasema, Nyoka alinidanganya nikala” Pamoja
na visingizio walivyotoa wazazi wetu wa kwanza adhabu walipewa na Mungu
mwenye haki. Kwa maneno mengine ni kwamba ukosefu wa umakini au
uangalifu lazima utatuletea majanga ya aina fulani kwani ni wajibu wetu
kujitahidi kuepuka makosa au kushughulikia madhaifu tuyaonayo katika
mahusiano yetu.
Kuna sababu mabalimbalil zinazopelekea mtu kutoa visingizio lakini wengi hutoa visingizio kwa sababu zifuatazo.
1. Kuogopa kufikiriwa vibaya
2. Kuogopa kushindwa
3. Kuogopa mabadiliko
4. Kuogopa kuwajibika
5. Kuogopa kufanya kosa
6. Kuogopa ugomvi
7. Kuogopa kuonekana hujui au huwezi.
Watu wanaotumia visingizio mbalimbali kuhalalisha matatizo au madhaifu
yao hawajui kuwa wanajikosesha fursa ya kujifunza mambo mapya na kutatua
matatizo yao na hivyo kutengeneza mazingira mazuri ya kimapenzi.
Vifuatavyo ni visingizio mbalimbali ambavyo wapendanao hutumia kuharibu ubora wa husiano wao.
1. SINA MUDA WA KUTOSHA
Mwanzoni mwa mahusiano ya kimapenzi utaona wazi kuwa mpenzi wako
anafanya jitihada kubwa za kutafuta muda wa kuwa na wewe au kuongea na
wewe kwenye simu lakini baada ya muda fulani unasikia mpenzi yule yule
anasema kuwa ana kazi nyingi ( yuko bize) na hana muda wa kuwa na wewe
au kuongea na wewe.Hivi karibuni nimesikia kisa cha dada ambae mpenzi
wake aliemzoesha kumpigia mara kwa mara na baadae kuacha kufanya hivyo,
kaka huyo alitoa kisingizio cha kukusa salio la muda wa hewani na dada
huyo alipofuatilia aliona ni ukweli kwani biashara ya kaka huyo ilikuwa
na hali mbaya.Nilifurahi kusikia kisingizio hicho toka kwa mwanaume
kwani kwa sehemu kubwa wanawake wengi ni sugu katika kutumia
kisingiizio hicho .Swala la mtu kutumia kisingizio cha ubize mara kwa
mara ni dalili ya penzi kunyauka. Uonapo hilo limeanza kujitokeza tambua
kwa hakika kuwa penzi lake kwako limeanza kubadili muelekeo na huko
linakoelekea ndiko alikokazia macho yake na sio rahisi kukukumbuka
wewe. Iwapo utaamini hilo na mtu huyo bado anadai yupo bize nab ado
anakupenda basi tambua unayokazi ya kuleta mabadiliko ili mrudie hali ya
mwanzoni. Hebu fikiria yafuatayo kwa mtu anaesema yuko bize, Iwapo tuko
bize sana tukashindwa hata kupika chakula – tutakufa njaa. Iwapo tuko
bize sana tukashindwa kufanya usafi wa miili na nyumba zetu tutanuka na
kupata magonjwa. Kwa maneno mengine mpenzi wako naposema yupo bize mara
kwa mara maana yake ni kwamba haoni uthamani wa uhusiano wenu na hajali
iwapo utaharibika kwa ukosefu wa muda wa kujenga na kuimarisha uhusiano
wenu.
Hebu fikiria mfano mwingine, mtu anasema “ napenda sana kujisomea BIBLIA
au Quran lakini nakosa muda wa kujisomea” Je mtu huyo huyo iwapo
anatumia muda mrefu kuangalia TV au Kuchat na marafiki zake kweli
utasema kweli anapenda kusoma BiBlia au Quran?
Kila mmoja wetu ana masaa 168 kila wiki na iwapo unatoa kipaumbele kwa
mpenzi wako lazima uamue kupunguza mambo mengi ila ufanya mambo ambayo
yatamthibitisha mpenzi wako kuwa ni wa muhimu kwako.KWA mtu anaekupenda
lazima atoe kipaumbele kwako kwa kuweka mabo mengine pembeni.Kuelewa
vizuri maneeno yangu fikiria juu ya mzazi kuacha starehe ya pombe ili
fedha zitumike katika kusomesha mtoto wake,au pale unapomnunulia mpenzi
wako zawadi haimaniishi kuwa fedha unazotumia hazina kazi kwa upande
wako bali unataka umfurahishe mpenzi wako.
2. VISINGIZIO VYA KUTOJUA
Watu wengi wamekuta mahusiano yao yanaharibika kwa kuwa hawakufanya
bidii kufahamu mambo mengi juu ya wapenzi wao na hivyo kusubiri kuambiwa
kila kitu. Unaposubiri uambiwe kila jambo unamboa mpenzi wako.
Nakumbuka siku moja kupokea sms toka kwa mpenzi wangu na ilikuwa jioni
ambapo nilikuwa nimechoka na sikupenda kujibu kwa sms. Nilimpigia
mpenzi wangu na simu haikupokelewa na ukapita muda hakunipigia, baadae
kidogo kanibip, nikachelewa kumpigia kwa kuwa nilikuawa naongea na simu
nyingine, nilipomaliza nikampigia kwa mara ya pili tena simu
haikupokelewa. Baadae nilipoonyesha kuwa nimekasikirika kwa yeye
kushindwa kupokea simu yangu akasema kuwa “ Yeye alijua kuwa meseji yake
ningeijibu kwa meseji na hakujua kuwa ningepiga badala yake. Niliumia
na kumuuliza, “Je, tumewekeana mkataba kuwa sms lazima ijibiwe na sms”
akasema, hapana .Ndugu yangu unaona kisingizio alichotumia mpenzi huyo?
Anasema alikuwa hajui kuwa upo uwezekana wa mimi kupiga baada ya kukuta
sms yake. Je kisingizio hicho kitasaidia kujenga penzi au kubomoa?
Kuna watu wengi wanaleta utani unaofanana na ukweli na mpenzi
anapokasirika kutokana na utani huo hujitetea kuwa “ nilikuwa sijui kuwa
itakuumiza hivyo” Mtu mmoja ambae alikuwa anachukia watu wanaotumia
visingizio alisema hivi. Mimi huvunja uhusiano haraka sana. Sitaki
nizeeke kwa kumwelezea mtu mzima wapi ananiboa” Mtu huyo anaonyesha ni
jinsi gani uzembe wa aina yoyote ni kosa la jinai kwake.Ni muhimu ndugu
yangu ujitahidi kuwa makini kwani haiwezekani kuwa mpenzi wako
atakuambia kila kitu anachohitaji au kukichukia, ni juu yako kuonyesha
penzi la kweli kwa kujitahidi kuongezea maarifa ili uwe bingwa katika
kila eneo la uhusiano wako.Itakuwa rahisi kwa penzi kati yenu kuongezeka
iwapo mtajenga mazingira ya uwazi a,\mbapo unajisikia huru kuuliza
maswali mbalimbali.
3. VISINGIZIO VYA KIFEDHA
Kwa sehemu kubwa mahusiano ya kimapenzi huhusisha fedha katika maeneo
mbalimbali, muda wa maongezi kwa njia ya simu, gharama ya vyakula na
vinywaji, zawadi za hapo na pale na mahitaji mengine muhimu. Tafiti
zinawaonyesha kuwa pale mpenzi mmoja aonapo mwenziwe anatumia fedha
vibaya kiwango cha penzi na furaha kati yao hupungua. Hebu fikiria
ukweli wa utafiti huo, Je sio kweli kuwa mke ambae anamwona mume wake
kuwa hawezi kulala bila kunywa pombe ataongezeka furaha au furaha
itapungua, Je mume anaemuona mke wake anapenda kununua nguo za bei mbaya
kila mwisho wa mwezi je furaha yake itaongezeka au itapungua? Ni muhimu
uone kuwa kupungua kwa furaha kwa mmoja kutaathiri uwezo wake wa
kuonyesha
penzi motomoto na hivyo kuweka uhusiano wenu katika eneo la hatari. Eneo
lingine la kifedha ambalo ni hatarishi ni kuficha matumizi makubwa au
matumizi yasiokubalika. Mtu atapewa Ths. 50,000/= kwa ajili ya mahitaji
muhimu anatumia Tsh. 40,000/= na nyingine anatumia kwa matumizi yake
binafsi. Anasema sina hela kumbe anazo na anaziweka kwa ajili ya
matumizi haramu. Watu wengi hutumia visingizio mbalimbali kuhalalisha
kutotumia fedha zao kwa ajili ya wawapendanao au kujifanya hana fedha
ili kumnyonya mwingine. Visingizio hivyo unaweza kuvitumia na kujiona
mjanja kumbe mwenzio anajua unamdanganya na visingizio vyote utumiavyo
ni uongo mtupu. Kwa kuwa mpenzi wako hataweza kukuambia juu ya hisia
zake juu ya matumizi yako ya fedha au utegemezi wako wa fedha kwake
,taratibu penzi kati yenu linanyauka hadi kufa Kabisa.
VISINGIZIO VYA KURUHUSU MAOVU DHIDI YAKO YAENDELEE.
Sikatai kwamba ni kweli mara nyingine mpenzi wako kweli kabisa anakuwa
na kazi nyingi kuliko kawaida lakini kamwe usianze kumtetea ili
kuhalalisha visingizio vyake iwapo unaona wazi kuwa iwapo angefanya
bidii lazima angepata muda wa kukuonyesha wewe kuwa ni mtu wa muhimu
katika maisha yake. Mtu anakwambia yuko bize kweli kama kweli anakupenda
hawezi kuamka saa 8 za usiku na kukutafuta, ndio anatumia kisingizio
kuwa amechoka na kazi na hamuwezi kucheza ngoma ya wakubwa je kweli
haweza kujitolea akakuamsha saa 9 usiku mkacheza ngoma hiyo? Ukishindwa
kumkabili na kumwonyesha ulemavu wa kisingizio chake utaendelea
kujidanya kuwa unapendwa kumbe mwenzi ameshakuwa msagaji au shoga.
Tambua kuwa nyuma ya kila kisingizio kunasababu usioambiwa ya yeye
kusema hivyo. Usiruhusu mpenzi wako aamini kuwa utakubaliana na
kisingizio chochote anachotoa.
Iwapo unajikuta unakubaliana kwa urahisi na visingizio vya mpenzi wako
tambua kuwa uko katika uhusiano ambayo kamwe hutaweza kuwa na furaha ya
kudumu. Ni kweli kabisa kuwa unampenda sana mpenzi wako anaekuumiza
lakini ni muhimu ukumbuke kuwa hustahili kuwa mtu wa kuumizwa umizwa
mara kwa mara haswa na mtu anaendai kuwa anakupenda. Sio hilo tu na hata
pale ambapo unajikuta una mpenzi anaeboa mara kwa mara na moyoni unaona
kuwa kwa uhusiano wa muda mrefu mtu huyu hafai ,ni vyema kusikiliza
moyo wako badala ya kutafuta visingizio vya wewe kuendelea na uhusiano
usiiokusisimua kama unavyotamani iwe. Ni kweli hajakufanyia uhalifu
mkubwa lakini iwapo haonyeshi bidii ya kuleta uchangamfu na raha
unayohitaji ni wakati wa kufikiria upya juu ya uhusiano huo. Bila shaka
umeshawahi kusikia mtu akisema, “Akiwepo fulani nyumba inachangamka
sana.” Maneno hayo ni ushahidi kuwa uchangamfu ni wa muhimu sana
miongoni mwa wapendanao.
Ndugu
yangu, ni wakati wa kupiga vita visingizio vyoyote anavyotumia mpenzi
wako kukukosesha raha na wewe mwenyewe upigi vita visingizio
vinavyomkosesha raha mpenzi wako.Katika utafiti uliofanyika huko
UINGEREZA na shirika la sheria liitwalo Slater and Gordon UNAONYESHA
KUWA watu wengi hubakia kwenye mahusiano yanayowaumiza kwa visingizio
vya aibu ya kuachwa,woga wa kubakia bila mpenzi au woga wa kukosa
fedha walizokuwa wanapata kwa mpenzi huyo mtesaji.Ni wakati sasa wa
kuangalia upya kiwango cha furaha kati yenu kama kinaridhisha, kama
hakiridhishi angalia nia aina gani ya visingizio vinatumika kuendeleza
maumivu kati yenu na kupambana na visingizio hivyo kikamilifu.
PENZI LINAPOGEKA KUWA KERO
Mahusiano ya kimapenzi ni kitu kizuri sana ndio maana mara ya kwanza mtu
anapoingia katika mahusiano ya kimapenzi anakuwa na furaha kubwa sana.
Naomba uzingatie kuwa nimesema kuwa mtu anapoingia katika uhusiano kwa
mara ya kwanza, yaani kama ni mwanaume huyo anakuwa ndie mwanamke wa
kwanza kabisa kwake na kwa mwanamke huyo ndio anakuwa mwanaume wa
kwanza kabisa. Katika ulimwengu tulionao sasa ni mara chache sana
utaona kuwa mwanaume ambaye hajawahi kuwa na mahusiano ya kimahaba NA
MWANAMKE anaanza na mwanamke ambaye na yeye huyo ndio anaekuwa mwanaume
wa kwanza.
Tatizo tulilonalo sasa utakuta mwanaume ambaye tayari ameshakuwa na
mahusiano na wanawake 2 anaanza uhusiano na dada ambaye hajakuwa na
uhusiano wowote au dada ambaye ameshakuwa na mahusiano na wanaume wawili
anaanza mahusiano na mwanaume ambae hajawa katika mahusiano ya
kimapenzi.Katika mazingira kama hayo lazima mtu atajikuta analinganisha
mpenzi aliene sasa na Yule aliemtangulia.
Katika kazi yangu katika Clinic ya afya ya mapenzi huu ni mwaka wa kumi
toka nianze vipindi redioni na mara chache katika TV na asilimia zaidi
ya 95% ya wateja wanaofika ofisini kwangu ni wanaume na asilimia kati ya
30 hadi 40ni wanawake .Asilimia kubwa ya wanaume wanaokuja ofisini
kwangu wana matatizo ya nguvu za kiume au kuwahi kumaliza upandaji wa
mbegu dume.
Vilio vingi toka kwa wanawake ni kutoridhika na raha wanayoipata katika
uchezaji wa ngoma ya wakubwa na ukosefu wa penzi wanalohitaji na hasa
kushuka kwa mawasiliano na muda wa kuka pamoja. Wakati wanaume
wanalalamika kuwa wanawake wanawanyima haki zao za kucheza ngoma ya
wakubwa wanawake wanalalamika kuwa hawafurahii kucheza ngoma ya wakubwa
na wapenzi wao.BILA shaka hapo unaweza kuona chimbuko l mvutano
unaotokea katika mahusiano mengi ya kimapenzi.
Tafiti baada ya tafiti zinathibitisha kuwa udhaifu au uzembe katika
kucheza ngoma ya wakubwa unachangia sana katika migogoro inayojitokeza
katika mahusiano ya kimapenzi na zifuatazo ni SMS toka kwa wasikilizaji
wangu wa redio, SMS, ambazo zinaonyesha jinsi gani penzi linaweza
kugeuka kuwa kero kubwa
‘Dr. Nelson mimi ni kijana wa umri wa miaka 25 nimekuwa na mahusiano na
dada mmoja na huu tunaingia mwezi wa 3 cha ajabu ni kwamba dada huyo
hakuwahi kuniambia kuwa ameolewe na nikajikuta nampenda sana huyo dada.
Sasa nimegundua kuwa ni mke wa mtu na nashindwa kumuacha japo na mimi
nina mchumba. Sasa Dr. huyo mke wa mtu anataka azae na mimi jambo ambalo
linanichanganya akili na kuniletea kishawishi cha kufanya jitihada
nivunje ndoa yake nimuoe yeye Dr. nifanyeje?.”
“Dr. Nelson mimi naitwa Issa nina umri wa miaka 29 nimeoa toka mwaka
juzi. Tatizo ni kwamba kila nikimwambia mke wangu kitu cha maana kama
hajakipenda huniambia nitaenda kuolewa na mwanaume mwingine kwani
mwanaume sio wewe peke yako, mbaya zaidi wakati wa kucheza ngoma ya
wakubwa yaani hata kabla sijamaliza ananiambia toka mimi nimechoka na
mimi kulazimika kumaliza haraka haraka. Dr. hali hiyo inanichukiza sana
naomba unisaidie hali hiyo inasababishwa na nini?.”
“Kwa jina naitwa Joyce niliishi vizuri na mume wangu ikafika sehemu
akaona simtoshelezi na akanisaliti na kuniambukiza magonywa ya zinaa
mara 2. Hayo yakanifanya niende nje ya ndoa ili nipata kujua nina utamu
au uchungu, nikashangaa napewa sifa kibao n huduma kupewa nikaanza
kumnyima mume wangu unyumba na kuacha aendelee na dogo dogo.”
“Dr. mimi niko kwenye ndoa mwaka wa 11 mke wangu hunipa unyumba kwa
shingo upande. Pia ameshanitamkia kuwa hanipendi mimi nampenda Dr.
nifanyeje ili upendo urudi?.”
“Dr. Nelson asante sana kwa mafundisho yako ambayo yanatupa tumaini kuwa
upo uwezekano wa mtu kufurahia ndoa siku zote. Niko ndani ya ndoa na
nina tatizo. Toka niolewe na mume wangu ninapomsemesha anakuwa mkali na
akiwa nyumbani ni kimya hamna mazungumzo na mara nyingine yuko bize na
simu. Siku akikusemesha vizuri ujue anataka umpe ngoma ya wakubwa acheze
unanishaurije hapo?.”
Kesi ya kwanza ni ya mwana mke aliechepuka kwa kijana ambae hajaoa na
akajikuta amekolea penzi mpaka anataka atengeneze kumbukumbu ya utamu
aliopata kwa kuzaa na mwanaume mwingine na kesi ya pili ni ya mwanamke
ambae hampendi mume wake na si ajabu ana mchepuko. Je ni mambo gani
ambayo yanachangia katika kuleta mikorogano mbalimbali miongoni mwa
wapendanao? Najua yapo mambo mengi sana kama matatizo ya kifedha,
uchafu, wivu, ndugu, unene na ukosefu wa uwazi na maongezi ya kutosha
baina ya wapendano pamoja na madhaifu katika utendaji wa tendo la ndoa.
Lakini kwa kuwa sayansi ya mapenzi inathibitisha kwa kati ya asilimia
80% hadi 85% ya migogoro yote katika ndoa chimbuko lake ni hitilafu
katika kucheza ngoma ya wakubwa upo umuhimu wa kuangalia eneo hilo kwa
makini sana.
Ni vyema tuangalie eneo hilo kwa upya na kwa umakini mkubwa sana.
Mwanzoni mwa uhusiano kwa wengi kila kitu ni kipya na chenye uwezo
mkubwa wa kuleta msisimko mkubwa na mmoja au wote hupenda hali hiyo
tamu iendelee milele. Lakini kwa bahati mbaya mwanamke atapata shida
kufika kileleni iwapo atakuwa katika mazingira ambayo yanamletea huzuni,
wasiwasi, kutojiamini, hasira au kuwa na hali ya kujiona kama mtu
alieshindwa.
Mwanamke atajiona kama mtu alieshindwa pale anapojiona kuwa ni mnene na
hataki unene, pale anapojiona kuwa hana fedha za kufanya hili na lile
kama marafiki au majirani wanavyoweza kufanya na mbaya zaidi akiwa na
mume ambaye hawi karibu na yeye mara kwa mara inatengeneza uchungu
nafsini mwake.
Mwanaume anaposhindwa kuwa karibu na mpenzi wake mara kwa mara mwanamke
hujisikia vibaya kwa kuwa anajiona kama hana mvuto mkubwa sawa na yule
mama aliechepuka, na huko kwenye mchepuko akajikuta anasifiwa na
kuonyeshwa kuwa ni mtu wa muhimu kwa mafunzo aliopata mchepukoni.
Kama ulivyoona kwenye stori hiyo mama huyo baada yakupata mchepuko
aliona uhalali wa kumnyima unyumba mume wake na moyo wake usimhukumu
kabisa.
DR. David Barlow wa chuo kikuu cha Boston huko Marekani katika utafiti
wake wa kina ameshuhudia kuwa mwanamke ambaye huko nyuma ameshawahi kuwa
na mwanaume mwenye matatizo ya nguvu za kiume au kuwahi kumaliza au
kukosa hamu ya tendo la ndoa, anapojikuta mume aliyenae sasa ameanza
kuonyesha madhaifu kama hayo hiyo inamzuia mwanamke huyo kulainika na
kutokwa na vichocheo ambavyo vingemuwezesha afike kileleni kwa urahisi
na hivyo kumuona mumewe kuwa mwanaume wa ukweli.
Mbaya zaidi ni mwanamke ambaye mpenzi wake anaonyesha kuwa anataka apate
uhakika kuwa mpenzi wake wa kike amefika kileleni. Mwanamke anapokuwa
na mwanaume anaemtia presha ili afike kileleni na yeye anajikuta hisia
zake zinabadilika na kuwa tendo la ndoa kama kero fulani.
Hapo mwanamke huyo ataanza kudanganya kuwa amfika mahali ambapo
hajafika. Utaweza kuona uzito wa kero hiyo katika mesiji iliotoka kwa
dada mmoja isemayo hivi :
“Dr. Mimi napendwa na wanaume wawili na tatizo nililokumbana nalo ni
kwamba yule nisiempenda ndie ambae ananipa raha kubwa ninapocheza nae
ngoma ya wakubwa lakini huyu ninaempenda japo ana fedha nyingi
anaponihitaji kimapenzi naona kama usumbufu. Dr. nifanyeje nibadilishe
hali hiyo?”
Meseji hii inathibitisha kabisa utafiti wa Dr. DAVID Barlow niliemtaja
hapo juu kuwa mwanamke ambaye tayari ameshakuwa na mpenzi kabla yako
anapokulinganisha na mwanaume aliekutangulia anakosa amani lakini
hatakuambia hilo na kujikuta anakuwa na huzuni mara kwa mara.Mbaya
zaidi hali hiyo ikiendelea inaleta hasira kama dada mmoja
alivyonisimulia..
“DR.NIKO kwenye ndoa mwaka wan ne mume wangu ananipa kila kitu
ninachohitaji bila kujali bei yake lakini kwenye tendo la ndoa ni mvivu
na mara nyingine ananikewepa.NILIKUWA NAMPENDA SANA lakini kutokana na
hali hiyo katika eneo la ngoma ya wakubwa nimejikuta nimeanza
kumchukia.DR. UTANISAIDIAJE NIBADILISHE hali hiyo? “
Tatizo la wanawake kukosa hamu ya tendo la ndoa ni kubwa sana na
linachangia kuharibu furaha katika mahusiano mengi ya kimahaba. Tafiti
ya hivi karibuni inaonyesha kuwa moja ya tatu ya wanawake wenye umri
kati ya miaka 18 – 59 wanakosa hamu ya tendo la ndoa. Ni muhimu
kutambua kuwa hamu ya tendo la ndoa ni tofauti kabisa na uwezo wa
mwanamke kujisikia raha ya tendo la ndoa wakati linatendeka. Unaweza
kuona kama jambo ambalo haliwezekani lakini tafsiri zinathibitishwa kuwa
wapo wanawake wengi ambao wanajishangaa kuona hawana hamu ya tendo la
ndoa lakini wanapojitoa muhanga na kufanya mchezo huo hupata raha hadi
kufika kileleni.
Kiongozi wa ufatifi huo Profesa Alan Rilely wa chuo anasema kuwa ukweli
huo wa kisayansi bado unaonekaa sana miongoni mwa wanawake kati ya umri
wa miaka 18 – 54 mwanamke anapojitoa kumpa penzi mumewe ataweza kufika
kileleni iwapo mumewe huyo anayo maarifa ya kutosha katika kumwandaa
mkewe kabla ya yeye kupanda jukwaani na pia awe na uvumilivu wa kutosha
kutumia muda mrefu katika kumwandaa mkewe.
Mwanaume atumiapo muda mrefu katika kumwandaa mwanamke anasababisha
mwanamke atokwe na kichocheo kingi cha OXIYTOCIN kichocheo ambacho
hupunguza makali ya kichocheo kilelecho hicho kiitwacho CORTISOL.
Kupunguzwa kwa makali ya uchovu kunamruhusu mwanamke aanzzw kupata raha
japo mwanzoni alikuwa hana hamu ya kucheza ngoma ya wakubwa. Katika hili
ushahidi toka kwa mke wangu mwenyewe ambaye aliweza kufanya kukataa
kucheza ngoma ya wakubwa lakini nilipomchombeza akajikuta anafurahi na
tukaweza kucheza midundo mingi ya ngoma ya wakubwa. Kutokana na hali
hiyo kujirudia mara nyingi mke wangu siku moja aliniambia kuwa kusema
maneno haya “usingekuwa unapenda dini wewe ungekuwa muhuni sana”
Kwa wanawake wengi ukosefu wa ukaribu wa kutosha na wapenzi wao husaidia
wapoteze hamu ya tendo la ndoa jambo ambalo wanaume wengi hawajui pale
wanapojikuta wananyimwa nafasi ya kucheza ngoma wanayoipenda sana.
Ukosefu wa ukaribu unapunguza mshikamano wa kihisia cemotional
connection) na kumfanya mwanamke amwone mwanaume kama mzigo badala ya
kumuona kama sehemu yake mwenyewe utatambua kuwa mpenzi wako anakuwa
kama mzigo pale uonapo anakuwa mzito kukubaliana na wewe katika maeneo
mbalimbali ikiwamo kucheza ngoma ya wakubwa.
Wanaume wengine nao huwa vimeo na kupata shida kukubali kuwa wamepoteza
hamu ya tendo la ndoa na hivyo kusababisha wake zao au wapenzi wao wa
kike kuamini kuwa lazima watakuwa na mchepuko. Mwanamke anapoona kuwa
mumewe au mpenzi wake hana hamu na yeye na kuamini kuwa ana mchepuko
japo hana ushahidi wowote ni rahisi kwake kukubali kuingia katika
ulimwengu wa michepuko. Tatizo linakuwa kubwa zaidi pale ambapo mwanamke
ana hamu na mumewe na mumewe hana hamu na mke wake, katika hali kama
hiyo kwa kuwa mwanaume hataki aonekane kama kimeo (asieweza kazi ya
kiume) anakuwa mkali kwa mkewe. Hali hiyo imejirudia mara nyingi unakuta
mwanaume anakuwa mkali kwa mkewe katika makosa au madhaifu madogo
madogo jambo ambalo humuumiza sana mkewe. Maumivu hayo ya mwanamke
yanamfanya awe mouongo kufuatilia akili yake ya kimapenzi na hivyo
kutengeneza hali ya mchepuko.
Katika mazingira kama hayo hata pale mwanaume atakapokuwa na hamu na
mkewe na mkewe atakuwa katika hali ya ukavu kutokana na uvhungu
uliosababishwa na ukali wake yeye mwenyewe. Mwanamke huyo anapojikuta
anakuwa mkavu kwa mumewe jambo ambalo halikuwepo kabisa anashindwa
kukubali kuwa sasa tayari amekuwa kilema katika eneo hilo na hivyo
kujaribu kucheza na mwanaume tofauti. Kilichonisababisha kuandika mada
hii ni kutokana na simu mbili toka wanawake wawili tofauti ambao
wamejikuta sio vilema baada ya kuchepuka nje ya ndoa zao. Kujiona kuwa
sio wa kutamanika, kujivunia maumbile ya mwili wako ni jambo la muhimu
sana katika kusababisha vichocheo vya hamu ya ngoma ya wakubwa kufanya
kazi vizuri.
Ukiwa mnene, matiti madogo au bunduki ya kiume ndogo, makalio madogo au
mfupi wa kimo, ukiwa mweusi na unatamani ungekuwa mweupe hayo
yanapoingia akilini mirija ya vichocheo inasinyaa kushindwa kuleta
mtiririko mzuri wa hamu ya ngoma ya wakubwa. Pale mtu anapojiona kuwa
hana maumbile ya kutamanika anajikuta hafikirii sana juu ya raha ya
tendo la ndoa, mtu anapokuwa hafikirii mara kwa mara juu ya tendo la
ndoa anashindwa kutengeneza kiwango cha kutosha cha kichocheo cha
TESTOSTERONE ambacho husababisha hamu ya tendo la ndoa miongoni mwa wake
kwa waume.
Utafiti wa miaka 33 unaonyesha kuwa asilimia 15 ya wanawake wanaotumia
vodonge vya majira kuzuia kupata ujauzito wanapoteza hamu ya kucheza
ngoma ya wakubwa. Kiongozi wa utafiti huo daktari bingwa wa mambo ya
wanawake (GYNECOLOGIST) Dr. Lee sharman anasema wanawake wengi
wanasingizia idonge hivyo jambo ambalo sio la kweli. Utafiti huo
uliohisisha wanawake 8,400 ulionyesha kuwa asilimia 22 hamu ya tendo la
ndoa iliongezeka, asilimia 63 hawakuona badiliko lolote lile na ni
asilimia hiyo 15 tu ndio walioona upungufu wa hamu ya tendo la ndoa.
Dr. Lee anasema wanawake hao huona hicho kuwa kisingizio rahisi kwa
kuwa hawataki kuangalia maeneo mengine yenye uwezo mkubwa wa
kuwapunguzia hamu ya tendo la ndoa kama woga wa kuhoji mambo, kuogopa
migogoro, ukosafu wa uwazi, kushindwa kumweleza mwanaume kuwa ameshindwa
kazi ya kiume au ana maumbile madogo na kadhalika.
Uhusiano wa kimapenzi unahusu mambo mengi kama maongezi, fedha, usafi,
zawadi kukosoana na sio tendo la ndoa peke yake lakini ukiondoa tendo la
ndoa mengine yote yanakosa nguvu za kushiriki uhusiano wa kimapenzi.
Tatizo ni kwamba watu wengi hawajui kuwa tendo la ndoa linaweza
kuongezea nguvu mambo mengine na hivyo kufanya bidii kubwa katika hilo.
Tatizo ni kwamba ukifanya bidii katika eneo hilo na ukapuuzia maeneo
mengine utakuwa unatengeneza upinzani wa wewe kufurahia tendo la ndoa
toka kwa mwenzio japokuwa anakupenda. Na sio hilo tu bali pia ukifanya
bidii katika maeneo mengine na kupuuzia tendo la ndoa lazima utazua
mgogoro kati yenu.
Watu wengi wanashindwa kuwa makini katika maeneo mengi ya kimahusiano
lakini ni wepesi sana kulaumu pale mpenzi anapomwacha au kumsaliti. Ni
kweli kabisa kuwa mwisho wa uhusiano unaumiza sana bila kujali nani
amesababisha hilo lakini wengi hawachukui tahadhali. Unaweza kusema kuwa
hata ungefanya nini kama mtu atakuacha atakuacha tu, hivyo ni kweli
lakini pale unapoachwa
JE NGOMA YA WAKUBWA YAWEZA KUVUNJA NYUMBA?
Tunaposikia watu maarufu hasa wasanii wamevunja mahusiano yao huwa
tunashangaa sana kwa kuwa hao ni watu wenye fedha nyingi sana na
kutokana na umaarufu wao usingetegemea hali hiyo kutokea. Mara nyingi
tunasikia kuwa usaliti, ulevi au fedha ndio vitu vinanvyochangia ndoa
nyingi kuvunjika lakini hatusikii kuwa matatizo ya nguvu za kiume,
ukubwa wa maumbile au udogo wake au ukosefu wa ufundi wa kutosha katika
uchezaji wa ngoma ya wakubwa kuwa ni visababisho ukweli ni kwamba
madhaifu katika eneo la tendo la ndoa yamewaleta wengi sana katika ofisi
yangu.
Mwanzoni mwa uhusiano mara nyingi kila mmoja anajiona kuwa ni mwelewa na
yanakuwepo matarajio kuwa huenda madhaifu hayo yatatokomea baada ya
muda Fulani jambo ambalo kwa wengi halitokei. Pale inapokuwa wazi kuwa
tatizo halitatokomea, huzuni na hali ya kukweka kushiriki kucheza ngoma
ya wakubwa wanatokea. Hali hii humfanya mmoja au wote wawili kujisikia
upweke ndani ya nafsi yake na upweke huo hubadilika kuwa uchungu na
mwishowe kuwa hasira. Inapotokea kuwa ni mmoja ambaye ana tatizo,
fedheha na kujiona kama kimeo itasababisha awe mkimya au atumie ukatili
kumkwepa mpenzi wake anayependa wacheze ngoma ya wakubwa mpenzi ambaye
hana tatizo atajisikia vibaya kuomba apewe kitu ambacho mpenzi wake
hapendi kukitoa.
Hali hiyo isipotafutiwa ufumbuzi yule asie na tatizo ataanza kuwa mtu
mwenye hasira katika maeneneo mengine tofauti na ngoma ya wakubwa.
Hatari ni kwamba tatizo hilo linapokuwa kwenye uhusiano kwa muda mrefu
linasababisha mmoja kujitenga kihisia na kuonekana hana uchangamfu
uliokuwepo mwanzoni. Mpenzi anapojitenga kihisia kutokana na kero ya
kunyimwa anachokipenda na mtu anayedai kuwa anampenda inakuwa vigumu
sana kurudia hali ya uchangamfu ule wa mwanzoni.
Tafiti zinaonyesha kuwa asilimia 43 ya ndoa zinazovunjika mzizi wake ni
udhaifu au ujinga katika kucheza ngoma ya wakubwa na watafiti hao
wanasema kuwa idadi inaweza kuwa kubwa zaidi ya hiyo kutokana na wengi
kukwepa kukubali kuwa wameshindwa kucheza vizuri. Kiongozi wa utafiti
huo Dr. Sari Eckler Cooper anasema kuwa pale uonapo ndoa inavunjika
kutokana na usaliti ni kwamba yule aliechoka kutokana na kunyimwa mchezo
au kutoridhika na utamu wa ngoma ya wakubwa anaamua kusaliti ili
asababishe kuachana na yule anaemuona kuwa kimeo katika kucehza ngoma
ya wakubwa. Watu wengi wanadai kuwa jambo kubwa linalosaidia kudumisha
ndoa ni uvumilivu na mimi napingana na jambo hilo japo naamini kuwa
uvumilivu ni jambo zuri. Unapovumilia jambo lazima liwepo tumaini kuwa
hali hiyo itabadilika kwa kuona bidii ambayo mwenzio anaifanya kuleta
mabadiliko. Iwapo mpenzi wako alien a udhaifu Fulani anafahamu jinsi
udhaifu wake unavyokukosesha raha na asifanye bidii ya kuleta
mabadiliko huo ni ukatili mkubwa usiohitaji uvumilivu kabisa kutokana na
imani yangu hiyo kuwa lazima uvumilivu uwe na mpaka nilijikuta siku
moja nasema kitu ambacho hata mimi mwenyewe kilinishangaza.
Dada mmoja katika ofisi moja alisema “Ndoa ni kuvumiliana” na mimi
haraka sana nikasema “Kuvumiliana kumewekewa mbwa, mbwa wanapofanya
mapenzi wanafuatana na hata ukipiga mbwa jike na mbwa dume haachani
wanavutana pamoja na kubakia wemenatana hivyo”. Baada ya kutamka jambo
hilo ambalo lilikuja bila kupanga nilijikuta nimeanza kufikiria juu ya
ukweli wa lile nililosema. Mbwa wanajikuta katika hali hiyo lakini hali
hiyo haidumu siku nzima kwani baada ya muda fulani huachiana jambo
ambalo linatupa picha ya kwamba unapovumilia jambo lazima liwepo tumaini
ya hali kubadilika na kuwa kama ile ya mwanzoni kinyume na hivyo ni
gereza la mateso.
Upo uwezekano mubwa wa mwanamke kupungukiwa na hamu ya tendo la ndoa
baada ya kujifungua jambo ambalo linatoa mwanga kwanini raha ya ndoa
hupungua katika miaka 2 – hadi 5 ya mwanzoni. Kutokana na uchovu wa
kipingi cha ujauzito, wasiwasi wa siku ya kujifungua inapokaribia,
ukosefu wa usingizi baada ya kujifungua na kubadilika kwa maumbile ya
uzazi baada ya kujifungua vinamuathiri sana mwanamke. Mama anaponyesha
mtoto upo uwezekana wa kichocheo kiitwacho ESTROGEN kupungua na hivyo
kusababisha viungo vya uzazi kuwa na ukavu ambao mwanzoni haukuwepo.
Wanawake wanashauriwa kutumia mafuta ya K.Y Jelly kuondoa ukavu huo.
Kipindi hiki ni kipindi kigumu sana kwa wanaume wasioelewa hali halisi
baada ya mwanamke kujifungua. Inashauriwa mwanamke aanze kushiriki ngoma
ya wakubwa baada ya wiki sita toka siku aliyojifungua na wanaume
wanapashwa kuheshimu hili kuepuka ugomvi au chuki baina yao. Pamoja na
hilo ni muhimu kukumbuka kuwa baada ya kujifungua mwanamke hatakuwa na
hamu kiasi kile alichokuwa nacho mwanzoni na kwa baadhi ya wanawake
inaweza kuchukua mwaka mzima kuweza kurudia kasi ya mwanzoni. Halii hiyo
inasababishwa na kichocheo cha PROLACTION ambcho hutoka kwa wingi kwa
mama anayenyinyesha. PROLACTIN hupunguza hamu ya mwanamke kucheza ngoma
ya wakubwa kwa kupunguza mtiririko wa kichocheo cha hamu kiitwacho
ESTROGEN.
Hapa ningependa kutoa angalizo ambalo wengi wanhitaji kulisikia.
Mwanamke anapokaribia kujifungua mishipa ya damu iitwayo VEIN katika
viungo vya uzazi hupanuka kuliko kawaida yake na hivyo kufanya kuta zake
kuwa dhaifu sana. Kuna hatari ya kifo iwapo mwanaume kwa kutumia mdomo
wake atachezea maeneo ya viungo vya uzazi vya mwanamke miezi miwili
kabla ya kujifungua au miezi miwili kabla ya kujifungua. Mwanaume
akitumia mdomo wake bila kujua anaweza kusababisha hewa kuingia kwenye
mishipa hiyo ya vein na kusababisha damu kutofika kwenye ubongo wa
mwanamke na kusababisha kifo. Hali hiyo iitwayo AIR EMBOLISM mara nyingi
hutokea iwapo mwanamke atashiriki ngoma ya wakubwa kabla ya wiki 6
kuisha.
Jambo linguine la ajabu linalojitokeza pale mama anapojifungua ni kwamba
ile hali ya kunyonyesha mtoto mama anapoteza hamu ya kuguswa na mumewe
kwa kuwa tayari anakuwa amepata mguso wa ngozi kwa ngozi toka kwa mtoto
na kuona kuguswa na mumewe kama kero ya aina fulani. Wapo wanawake
wengine ambao hujisikia raha ya kimahaba pale mtoto anayonyonya chuchu
PENZI LINAPOGEKA KUWA KERO
Mahusiano ya kimapenzi ni kitu kizuri sana ndio maana mara ya kwanza mtu
anapoingia katika mahusiano ya kimapenzi anakuwa na furaha kubwa sana.
Naomba uzingatie kuwa nimesema kuwa mtu anapoingia katika uhusiano kwa
mara ya kwanza, yaani kama ni mwanaume huyo anakuwa ndie mwanamke wa
kwanza kabisa kwake na kwa mwanamke huyo ndio anakuwa mwanaume wa
kwanza kabisa. Katika ulimwengu tulionao sasa ni mara chache sana
utaona kuwa mwanaume ambaye hajawahi kuwa na mahusiano ya kimahaba NA
MWANAMKE anaanza na mwanamke ambaye na yeye huyo ndio anaekuwa mwanaume
wa kwanza.
Tatizo tulilonalo sasa utakuta mwanaume ambaye tayari ameshakuwa na
mahusiano na wanawake 2 anaanza uhusiano na dada ambaye hajakuwa na
uhusiano wowote au dada ambaye ameshakuwa na mahusiano na wanaume wawili
anaanza mahusiano na mwanaume ambae hajawa katika mahusiano ya
kimapenzi.Katika mazingira kama hayo lazima mtu atajikuta analinganisha
mpenzi aliene sasa na Yule aliemtangulia.
No comments:
Post a Comment