Ushawahi kujikuta katika hali ambayo unashindwa kujua utaanza vipi
kuongea na mwanamke? Ni mwanamke mzuri ambaye moyo wako unamtamani
lakini akili yako inashindwa kutengeneza mawazo ya jinsi utakavyoanzisha
stori na yeye. Unabakiwa ukimuangalia akikupita mbele yako, ama mbaya
zaidi anakuja kuchukuliwa na wanaume wasiokuwa na thamani yeyote kwa
maisha yake. Unabakia na majutio na mawazo ya "kama ningeweza kujiamini
mbeleni si ningem...." Well, tatizo hilo halijawahi kutokea kwako pekee
bali kwa kila mwanaume wakati flani katika maisha yake na hatutaki
lijitokeze tena mbeleni.
So chanzo cha wewe kutoweza kumtongoza huyu mwanamke ni kuwa akili yako ilikataa kutoa mazungumzo ambayo ungeweza kuyatumia kwa huyo mwanamke. Well, waonaje kwa mara moja tukubaliane na akili yako na tusitumie maongezi kuapproach mwanamke, na badala yake tutongoze kimya kimya?
Kutongoza kimya kimya ni mbinu rahisi sana, mwanzo ni rahisi kwa kuwa unapata kujua kama mwanamke anakupenda au la. So bila kupoteza wakati, hebu tuchambue mpango mzima.
Zama nami!
1. Kwa kutumia macho
Kila mtu anajua nishati inayotokana na kutumia macho. Macho ni kiungo ambacho wanaume wamebarikiwa nacho na akikitumia vizuri kinajeuka kama silaha nzito wakati ambapo unaitumia kwa mwanamke. Ushawahi kujiuliza ni kwa nini wakati mwingine mwanamke anashikwa na aibu/haya wakati unapomwangalia? Ama je ushawahi kumskia mwanamke akisema kuwa usimwangalie machoni mwake? Hii ni kwa sababu macho yanaweza kutumika kuongea maneno ambayo mdomo unaweza kushindwa kuongea.
Wakati utajipata ukimwangalia mwanamke, mwangalie machoni halafu utoe tabasamu. Kumuangalia kunaonyesha unajiamini. Kutabasamu unamwonyesha kuwa wewe ni salama na anaweza kuongea na wewe. Unaweza kusoma chapisho letu la awali ambalo linafafanua mbinu ya kutumia macho kuapproach mwanamke kwa kina.

2. Mfanye akugundue kupitia kutangamana kwako
Njia nzuri ya kusimama ili wanawake waweze kukutambua ni kupitia
utangamano wako na wengine. Kujizunguka na wanawake wengi (haswa wale
warembo) kutaashiria ya kuwa wewe ni aina ya mwanaume ambaye wanawake
wanapenda kuwa naye. Hii itawafanya wanawake wengine katika hio sehemu
kuwa na shauku ya kutaka kujua ni kitu gani ambacho kinakufanya wanawake
wapende kuwa na wewe. Hii automatically itawafanya wanawake kuwa na
umbea kukuhusu, kuvutiwa kwako, na hata kuingiwa na wivu wa kwa nini
haujawaingiza katika kundi lako.
Mbinu hii ni moja wapo ya sosholojia ya wanawake, kimaumbile wanawake
hupenda vitu ambavyo wanawake wengine hupenda. Hivyo kama wewe unamtaka
mwanamke flani na hutaki kutumia maongezi, anza kutangamana na marafiki
wake wote isipokuwa yeye, mwishowe utamwona akijileta yeye mwenyewe,
tena ujitayarishe na mapema kwa kuwa atakuja na presha ambayo kama
hukujipanga vizuri inaweza ikakulemea.
3. Matumizi ya banta bila kuongea
Banta ni mbinu ya kuonyesha ucheshi, mchezo na mzaha wakati wa kuongea
na mtu. Mbinu hii pia inaweza kutimizwa bila kutumia mazungumzo ili
umfanye mwanamke aweze kuvutiwa kwako.
Kwa mfano, kama ulishatumia mbinu ya macho kuwasiliana na mwanamke na
unataka kuendeleza shughli kwa kutumia banta, njia rahisi ni kumuonyesha
nyuso za ucheshi. Jifurahishe na uwe mcheshi - toa ulimi wako nje -
pinda macho yako - weka uso wowote ule wa kipuzi ambao unajiskia. Hii ni
njia rahisi ya kumfanya mwanamke atabasamu akiwa mbali, na itakuwa
rahisi kwako kumuapproach na kuendea na yeye iwapo ataonyesha dalili za
kupendezwa na wewe.
4. Mvutie na mwonekano wako
Ukitaka kumvutia mwanamke kiurahisi basi ni muhimu kubadilisha mwonekano
wako. Mbinu hii tuliieleza kwa kina katika chapisho la jinsi ya
kubadilisha mwonekano wako uwavutie wanawake. Kwa kawaida, wanawake
wanapenda kushufu wanaume ambao wanavalia kinadhifu.
Lakini hapa usichukulie makosa. Kubadilisha mwonekano hakumaanishi ya
kuwa unapaswa kuvalia nguo ghali ama za thamani ya juu. La hasha.
Kubadilisha mwonekano kunamaanisha kuvalia nguo safi, nadhifu na ambazo
zinaashiria hulka yako. Usijitese kuvalia nguo ambazo haziwiani na wewe
kwani kwa mwanamke ni rahisi kukugundua kama umejeuka mwigo.
5. Ishara ya mwili wako
Wanawake wanaweza kujua mengi kukuhusu kwa kuangalia miondoko yako ya
mwili pekee. Kama unataka kuonyesha ujiaminifu ambao utamfanya mwanamke
akutambue, basi ni lazima mwili wako uonekana vile unapaswa kuonekana.
Kuonyesha confidence katika mwili wako unapaswa kufanya yafuatayo:
i) Simama wima - mwanaume thabiti akisimama anakuwa hivi; masikio
yako yawe nyuma ya mabega yako, mabega yako yawe nyuma ya kiuno chako,
kiuno chako kiwe nyuma ya kiwiko chako.
ii) Kaa kwa kujitanua - wakati umekaa katika kiti, hakikisha ya
kuwa unachukua nafasi yote ambayo unaweza kuitimia. Egemea kwa kiti,
itanue miguu na mikono yako, kichwa kiweke kiangalie juu.
iii) Jinsi unavyokaa - Usisogee sogee kama huna sababu zozote, usikunje miguu wala mikono, usiangalie chini, usijikune kichwa ama kutafuna tafuna.
iv) Unavyotembea - Tembea na sababu, tembea kwa kujiamini, tembea na njia thabiti.
Kuweza kukontrol mwili wako inakusaidia kuonekana mtu mwenye nguvu, wa
kujiamini ambaye anapendwa na wanawake. [Soma: Jinsi ya kutumia mwili
wako kutongoza]
6. Kuwa na hadhi ya juu
Mpaka sasa hili chapisho linaongea kuhusiana na kuwasiliana na mwanamke
bila kuongea naye. So iwapo unataka mwanamke akunotice, wakati mwingine
inahitajika kuwa na jitihada za ziada. Kukaa sehemu moja kungojea
mwanamke akugundue haitakuwa ya fanaka kama vile ambavyo utaamka na
kujifanya uonekane wewe mwenyewe.
So utafanyaje mpaka mwanamke akunotice?
Tangamana na marafiki, jamiiana na kila mtu ambaye unamjua. Wakati umetoka matembezi au sehemu yako ya kujivinjari, ongea na kila mtu - wanaume, wanawake, wateja, wafanya kazi nk. Wanawake watauona uwezo wako wa kutangamana na kila mtu na watakuwa na interest ya kuongea na wewe. Ziada ni kuwa utakuwa unaonyesha ujiaminifu, urafiki, na uko na uwezo wa kujicontrol katika jamii - tabia zote ambazo wanawake wanaziona nzuri katika mwanaume. [Soma: Jinsi ya kupandisha hadhi yako kwa mwanamke]

7. Wafanye wanawake wakufukuzie
Kufanya wanawake wakufukuzie inaweza kuwa rahisi sana. Kile ambacho
unahitajika ni kutoka nje umakinike na kujifurahisha muda wote. Weka
tabasamu katika uso wako na ujiinjoy wewe mwenyewe. Hii itamfanya
mwanamke kukunotice na kutamani kuungana na wewe ili muinjoy pamoja.
No comments:
Post a Comment