"Wanasayansi
wamethibitisha mawasiliano ya watu wanaokutana kwa mara ya kwanza
hutegemea zaidi ishara za kimwili, ambapo asilimia 55% huwa ni kwa
kutumia ishara, asilimia 38% yakiwa maongezi ya kutumia sauti pamoja na
asilimia 7% ikiwa vitu ambavyo haviendani kabisa na unachokiongea."
#3; Anakua na ishara unazozifanya wewe.
Utafiti
uliofanywa na chuo kimoja kikuu nchini Marekani, imebainisha kama
ukitaka kujua iwapo mwanamke amevutiwa na wewe, inabidi uangalie zaidi
ishara kuliko maongezi, na hii kuhitimisha wanawake huongea tofauti na
wanachomaanisha. kiumeni.com imekuandalia ishara kumi zilizothibitishwa
na watafiti pamoja na wanasayansi ambazo mwanamke hufanya pindi
anapovutiwa na wewe akiwa anajijua au hakiwa hajijui ili kukuonyesha
kama amevutika nawe.
Jifunze ishara hizi na maisha yako ya kimahusiano yatabadilika kwa hali ambayo hautaitarajia.
#10; Anashika au kupikicha nywele.
Kwa
zaidi ya miaka 40, watafiti wamenyumbuisha tabia wanazozifanya wanawake
kukujulisha wamevutiwa na wewe, iwapo mwanamke akizishika shika nywele
zake kwa muda mfupi inaweza kuwa ishara ya kukupa taarifa ya kuwa
anafurahia uwepo wako, ila akiendelea kuzichezea kwa muda mrefu
inawezekana akawa katika hali ya kutokujiamini au hakuamini wewe.
#9; Anauma midomo yake.
Tabia
hii mwanamke huifanya ili kuhamisha fikra zako kuelekea kwenye midomo
yake, inaweza maanisha ukienda na ukiwa mchombezaji mzuri mabusu
yanaweza kuwa ya kufikia, inabidi uwe mwangalifu sana wakati wa
kuitambua hii tabia na akiwa anauma midomo yake kwa muda inamaanisha
amevutiwa nawe ila kuuma midomo mara kwa mara inaweza onyesha ndio
mazoea yake, kwa hiyo kuwa makini kutofautisha kati ya hizo tabia mbili.
#8; Anacheka cheka, kukusumbua na kukuangalia kwa macho mazuri.
Hii
tabia zipo pande zote mbili, hata wanaume pia huifanya ila kwa wanawake
wanaweza pia kuitumia ili kukujua nia yako kwao, kwa hio usiichukulie
kwa haraka sana inawezekana anakujaribu tu.
#7; Anakukaribia sana kimwili.
Ukaribu
tunao karibia watu inategemeana na mahusiano yetu kwao, ukimkaribia mtu
sana huwa mara zote ni katika hali ya upendo, kwahio mwanamke akikukaribia
sana inawezekana akawa anafanya hivyo ili upendezwe naye zaidi, inabidi
kabla hujafanya maamuzi yeyote hakikisha umehakikisha mkaribio wake
kwako sio wa hali ya kikawaida, na unaweza hakikisha kwa kusogea kidogo
ili kumtegeshea kama atasogea tena huku ukiwa na tabasamu usoni.
#6; Anachangia unachozungumza na kuongelea kuhusu mambo yake binafsi.
#6; Anachangia unachozungumza na kuongelea kuhusu mambo yake binafsi.
Baada
ya kufanya mazungumzo kwa muda na kunoga, jaribu kupeleka mambo mbele
kwa kuanzisha mada ambayo inahusu maisha yako binafsi ila hakikisha mada
isiwe ya ndani sana na isiwe inaelekea kana kwamba unataka kumjua kwa
undani na maelezo yake yasiwe yanamlenga, hii itamfanya ajisikie huru na
kutokuogopa, iwapo mambo yakienda vizuri na amevutika nawe utaona na
yeye anachangia kwa kutoa mada inayohusu mambo yake binafsi, watu huwa
wanaongea kuhusu mambo ya ndani kwa watu wanaowapenda na kujisikia huru
mbele yao.
Iwapo
maongezi haya mkiyafanya huku mnakula chipsi kwa pamoja itafanya mambo
yaende vizuri zaidi, kutumia vitu pamoja huongeza ukaribu na maelewano
zaidi.
#5; Anakua na urafiki wa kimaongezi wakati mnaongea.
Sahau kuhusu mistari ya kutongozea ulioifanyia
mazoezi, ikija kwenye kuangalia hamasa ya mwanamke kwako, huangalii
jinsi unavyomsifia, unaangalia mapokeo ya maneno unayomwambia, mwanamke
akikujibu hata kama kwenye hali ya kukataa jambo, akikujibu kwa sauti ya
upole na laini ujue amependezwa nawe, kwahiyo usiwahi kuondoka kutoka
katika mazingira hayo au sehemu hio, ila akikujibu kwa sauti ya ukali,
tafuta pakutokea.
Ili kuondokana na kupoteza muda kutongoza mwanamke
ambaye havutiwi na wewe, jaribu kwa kuanza na maswali rahisi ambayo
majibu yake ni rahisi, kwa njia hii utajua kama kapendezwa na wewe au
vipi, kama hajapendezwa na wewe utaona anakuondoa kwenye maongezi ila
aliyependezwa na wewe ataendelea na maongezi.
#4; Anakua katika mkao wa mwaliko kimaongezi.
Mwanamke
akiwa amependezwa na wewe huwa anakua amekaa mkao wa mwaliko wa
kimaongezi, akikuangalia anakua na macho ya kiurafiki na si ya ukali na
hata ukiwa mbali utajua kwamba pozi na macho yake vinakuita.
#3; Anakua na ishara unazozifanya wewe.
Mwanamke
akipendezwa nawe, atakua anajibu mapokeo ya ishara zako unazotoa, kwa
mfano ukitabasamu na yeye utamuona anatabasamu vile vile, ukicheka na
yeye atakufatiliza hivyo hivyo.
#2; Anapindisha kichwa kidogo na kutabasamu.
Watafiti
wamebainisha mwanamke akipindisha kichwa kidogo na kuachia sehemu ya
shingo yake kuonekana kidogo ikifuatiwa na tabasamu mara nyingi anakua
amevutiwa na anachokiangalia.
#1; Anachezesha macho.
Kukutanisha
macho ni kitendo cha ukaribu kwa binadamu, kurudia rudia au kuendeleza
kukutanisha macho huwa kuna maana kuu mbili, kwanza kuonyesha hali ya mguso kihisia, na pili kuonyesha hali ya jazba.
Ili
kujua kama analo hitaji la kuongea nawe, angalia jinsi anavyochezesha
na kukutanisha macho na wewe, utakuta mnakutanisha macho zaidi ya mara
kadhaa na kukiwa na tabasamu nyingi, kama ukiona mmekutanisha macho
halafu akaacha kukuangalia tena jua huyo hajavutika na wewe, na isiwe na
shaka sana maana mara nyingi kitu hichi huweza kutokea bila ya wewe
kukitambua.
No comments:
Post a Comment