Kuna watu wana Mikwara sana, ukiachana nae anaanza Maneno
ya shombo, wengine hudiriki kukwambia ''you cant live without me utarudi
tu'', unajiuliza huyu mtu ana Hisa kwenye mishipa yangu ya moyo au ana
mrija wa Oxygen yangu ya kutumia kesho?? Kama nilizaliwa peke yangu
kwanini nisiweze kuishi wewe ukiondoka??
Maneno ya mkosaji haya, usiyasikilize kamwe! Unapoamua
kufanya Maamuzi magumu usisikilize kingine chochote, Follow your heart.
Wengi wamegeuzwa watumwa kwa kuamini they cant live bila watu fulani,
kisa wamezoeana, au wamekaa muda mrefu kwenye mahusiano, unahisi kama
hutaweza... Hamna kitu kisichowezekana, Mungu ameumba kusahau, utapona
maumivu na utasonga! Hakuna destiny rahisi ya Kimapenzi bila kufanya
maamuzi magumu, lasivyo Jiandae kuwa mtumwa wa mtu fulani, binadamu
fulani ambaye naye amegundua wewe ni dhaifu na anatumia udhaifu wako
kukutesa maisha yote...
Amua leo, Uwe mtumwa wa mtu au utengeneze furaha yako kwa Kumove on kupata Lover of you life
No comments:
Post a Comment