Artikel Terbaru

Responsive Ads Here

Wednesday, May 17, 2017

KWA BAADHI YA WALE WANAOTAFUTA WATOTO USIKU NA MCHANA NA WALA HAWAJUI KWANINI HAWAPATI



Yamkini wewe ni mmoja wa watu wenye kiu ya muda mrefu ya kupata mtoto, yamkini umeshakwenda kwenye kila aina ya hospitali na kwa wataalamu wa tiba, yamkini umeshawahi kushauriwa hata kuwaona waganga wa jadi, umepewa dawa za kumeza, za kunywa, za kujipaka na hata zakumwekea mumeo au mkeo lakini bado hamjawahi kusikia hata kaharufu ka kichefuchefu au kutema mate kuashiria ujauzito. Yamkini mmeshafanya maombi sana, mmeshafunga sana, na kupita kwa kila mtumishi wa Mungu, wazazi wako, wakwe zako, labda hata na mwenza wako hajui tatizo nini, labda hata wewe mwenyewe umeshasahau chanzo. Ngoja nikushauri tu kidogo kwamba, kabla hamjahangaika sanaaa na kupoteza muda na fedha hembu muulize mke wako “Je umeshawahi kutoa mimba huko nyuma??? Na kama jibu ni ndio, ni mimba ngapi??? Na wewe mwanamke muulize mumeo, “Je umeshawahi kuwashawishi au kuwalazimisha wanawake wangapi watoe mimba zako?? Umewapeleka wangapi kwa madaktari ili wakatoe mimba? Au umewapa wangapi fedha ili wakatoe mimba zako?? Msisumbue watumishi wa Mungu na madaktari bure wakati mnajua mlichofanya kabla ya kuoana, dhambi haifunikwi kwa mchanga kama kinyesi, kumbuka wazungu wamesema “what goes around, comes around”. Jifunzeni kuzishuhulikia “pasts au backgrounds”zenu mbovu ambazo zinaweza kuyaathiri maisha yenu ya sasa, hata kama unajifanya leo ni mtakatifu kuliko malaika Gabrieli, baadhi ya uliyoyafanya jana yanaweza kuleta shida leo. Hata kama wanasema “mavi ya kale hayanuki” yako matokeo ya baadhi ya dhambi hukufuata nyuma yako kama vile inzi anavyofuatana na uvundo. Tafakari, chukua hatua. Haki elimu – Chris Mauki

No comments:

Post a Comment