Mpenzi msomaji wangu, kichwa cha habari hapo juu huenda kimekushtua
lakini huo ndiyo ukweli wa mambo! Nasema hivyo kutokana na kile
ninachokishuhudia sasa hivi kwenye ulimwengu wa mapenzi.
Kwa wale ambao wanapitapita maeneo yanayosifika kwa biashara ya ukahaba
watakubaliana na mimi kwamba hali ni mbaya sana. Mabinti wazuri sana
wanaonekana mida ya usiku wakiwa mawindoni.Wanajinadi kwa wanaume
wanaopita huku wakiwa wamevalia nusu utupu, lengo likiwa ni kupata pesa.
Katika wasichana hao ambao wengine hujiuza bila hata kwenda kusimama
barabarani au kukaa kwenye kumbi za sterehe na baa, wapo ambao ni wake
za watu na wengine wana wapenzi wao lakini wanajiuza kwa njia ya
mtandao.
Swali la kujiuliza ni kwamba, inakuwaje mpenzi wa mtu anafikia hatua ya kufanya biashara hii haramu? Wakati unajiuliza hivyo, ufahamu kwamba wengi wanaojiuza wana tamaa ya pesa! Wanahisi kutokana na ugumu wa maisha, wanaweza kuitumia njia hiyo kujikwamua!
Swali la kujiuliza ni kwamba, inakuwaje mpenzi wa mtu anafikia hatua ya kufanya biashara hii haramu? Wakati unajiuliza hivyo, ufahamu kwamba wengi wanaojiuza wana tamaa ya pesa! Wanahisi kutokana na ugumu wa maisha, wanaweza kuitumia njia hiyo kujikwamua!
Sasa kwa hali hiyo kaa chini na ujiulize, unavyomuona mpenzi wako
unahisi hana tamaa za kijinga linapokuja suala la pesa? Je, ni mtu
anayeweza kukuvumilia hata pesa inapokosekana? Je, ni msichana ambaye
hawezi kushawishika kirahisi?
Kama si mtu mwenye vigezo hivyo, ni rahisi sana kujiingiza kwenye biashara hiyo na wewe usijue.
Kuna mazingira f’lani ambayo yakiwepo kuna uwezekano mkubwa mpenzi wako akawa miongoni mwa wale wanaotumia miili yao kujipatia pesa.
Kuna mazingira f’lani ambayo yakiwepo kuna uwezekano mkubwa mpenzi wako akawa miongoni mwa wale wanaotumia miili yao kujipatia pesa.
Moja, kama mpenzi wako ana urafiki na wasichana ambao maisha yao
yanategemea kuwezeshwa na wanaume, hata huyo wako anaweza kuingizwa
huko.Wapo mabinti ambao wanajiuza lakini wana marafiki zao ambao ni wake
au wapenzi wa watu. Sasa katika ongeaongea yao unaweza kushangaa changu
anatoa ushuhuda kuwa biashara hiyo inalipa na ushuhuda huo ukimpata
msichana asiyejua kuchuja mambo, unaweza kushangaa naye anaifanya kwa
siri.
Mifano
ya watu hao ipo, wapo ambao walikamatwa wakijiuza tena wengine wakiwa
wana kazi zao lakini wakajitetea kwamba wasitolewe magazetini kwa kuwa
wapenzi/waume zao wakiona itakuwa aibu. Hiyo inaonesha wazi kwamba,
miongoni mwa watu wanaofanya biashara hiyo ni wale walio kwenye
uhusiano, ndiyo maana nikasema hata siku ukitonywa kuwa mpenzi wako
anajiuza, usikatae bali fanya uchunguzi kwanza.
Pili, kama wewe unajua kabisa kwamba mpenzi wako ana tamaa ya kupenda
kuvaa vizuri, kuwa na simu kali, kula chakula kizuri na kuishi sehemu
nzuri kisha wewe ukawa humpatilizi, ukijipindua kidogo tu unaweza kukuta
anatumia njia zake anazojua ikiwemo hii ya kujiuza kupata pesa.
Lakini pia ukiwa na mpenzi kisha ukawa mgumu kumsaidia katika yale ya
msingi wakati uwezo unao, unamshawishi kujiuza. Ndiyo maana niliwahi
kusema kwamba, ubahili wako unaweza kumfanya mpenzi wako licha ya
kukupenda akatafuta mtu kama siyo watu wa kumuwezesha.
Kutokana na hali hiyo nilisema kwamba, unapoingia kwenye uhusiano na
mtu, hakikisha unamuepusha na vishawishi vya kujiuza, kupapatikia
wanaume wenye pesa, kupenda starehe wakati uwezo haupo.Haya mambo jamani
yapo, wapo wake za watu ambao wanaachwa nyumbani na waume zao lakini
wana wanaume kibao ambao huwasiliana na kuwapa huduma kwa malipo tena
kwa siri kubwa.
Utashangaa hata ukiwa na hali ngumu kifedha, mnakula vizuri,
anajinunulia nguo za bei mbaya kila wakati na wala husikia akikulilia
kwa shida ndogondogo. Unadhani katika mazingira hayo siku ukiambiwa mkeo
anajiuza utakataa? Najua huwezi kukataa kutokana na mazingira ambayo
umekuwa ukiyaona. Hivyo ni jukumu letu sisi tulio kwenye uhusiano kuwa
makini na wapenzi wetu.
Tuna jukumu la kuwapa elimu juu ya tabia hii ya kutafuta pesa kwa
kutumia miili yao na kuwaeleza wazi kwamba, wengi waliokuwa wanafanya
kazi hiyo leo hii wamekufa na wengine wanaishi maisha ya tabu kufuatia
kuambukizwa virusi vya Ukimwi au wameanza kuugua maradhi hayo.
No comments:
Post a Comment