Kwa nini mapenzi ni tata? Unaweza kujiuliza swali hilo. Ni kwa faida ya
kila mmoja kwa sababu yanamhusu kila mmoja wetu. Ni matamu lakini ndani
yake hutokea kuwa na ukakasi kama siyo maumivu.Jiulize tena, kwa nini
mapenzi yanasumbua? Mapenzi ni maumivu ya kichwa na moyo. Watu wengi
waliomo ndani yake wanaweza kukupa ushuhuda wa mateso wanayoyapata
kwenye uhusiano wao. Je, baada ya kuteseka huwa wanajiapiza kutorudi
tena?
La hasha!
Wanajaribu mara nyingi, hawakomi. Unaweza kujiuliza ni kwa nini lakini
ukweli ni kwamba pamoja na maumivu ambayo mtu anaweza kuyapata kwenye
mapenzi, bado yanabeba hisia kubwa kabisa katika maisha ya kila
binadamu.
Maisha bila mapenzi hayajakamilika. Kutokana na hilo, uwanja upo wazi
kwako kujiuliza ni kwa nini kitu kitamu namna hiyo kikafanywa kuwa tata,
jumlisha na maumivu ya hapa na pale. Uvumilivu ukizingatiwa, huyeyusha
utata unaojitokeza hapa na pale.
Muhimu zaidi ni kwamba mapenzi hayatoshelezi kwa uwajibikaji wa
nusunusu. Yanahitaji nidhamu na utekelezaji wa moja kwa moja kutoka
moyoni. Yanayomhusu mwenzi wako ni vema uyabebe kama yako, hivyo ndivyo
uhusiano unavyotaka.
Mapenzi yanahitaji akili, utashi na fikra zako bila kusahau nguvu zote
katika kuzalisha matunda ya kila siku kwenye uhusiano ulionao. Utata
unaoonekana ni ule unaotokana na wenzi kutotimiza matarajio ya kila
mmoja.
Imetokea kuamini kuwa maneno ni mhimili wa kudumu kwa uhusiano na ngono
husuluhisha migogoro ya muda mfupi. Wapenzi wanaponuniana, endapo
watakutana faragha, hasira zote hupotea. Hata hivyo, kwa bahati mbaya,
ni zaidi ya kutosheka kimwili na utamu wa maneno mazuri.Kwa mfano, ndoa
nyingi zinakumbwa na matatizo ya watu kushindwa kuwa wakweli. Mwanaume
au mwanamke anaweza kusema ni kiasi gani mwenzi wake anamuumiza. Lakini
mwisho wa mazungumzo hawezi kukiri kasoro zake ambazo pengine ndiyo
chanzo cha kila kitu.
Utata zaidi katika mapenzi ni kuwa inapotokea watu wanajuana kwa undani
mno, hasa baada ya kuishi muda mrefu, ni hapo ndipo maneno hayawezi
kufaa kitu, wala mchezo wa faragha hautaleta maelewano kwa maana hakuna
kitu kigeni.
Lingine la utata katika mapenzi ni kwamba huwezi kuficha tabia yako muda wote.
No comments:
Post a Comment