Ushawahi kujiuliza kwa nini wanawake wengine ukianza kuwatongoza
wanakupa jibu zito ambalo unashindwa kulielewa la: "Mimi na wewe ni kama
marafiki"?
Jibu hili hupokewa na wamaume wengi ambao bado hawajakomaa katika nyanja ya kutongoza na kudeti wanawake.
Hili ni tatizo ambalo mara kwa mara hujitokeza iwapo hautaufuata
mpangilio stahili ambao unapaswa kuutumia unapoaproach mwanamke.
Unajiona ya kuwa unatongoza mwanamke, kila kitu unachofanya ama
unachotaka kutoka kwake anaitikia (isipokuwa muingiliano kimwili),
lakini ile siku unapoamua kuufungua moyo wako na kumwambia ya kuwa
unampenda anakuzima na kukatiza matumaini yako ambayo ulikuwa tayari
umeyaweka katika akili yako.
Kutaka kujua kwa undani swala hili (tayari sababu zake tulikuwa
twazijua) tuliamua kukusanya maoni kutoka kwa baadhi ya wanawake warembo
kutaka kujua ni kwa nini wanawakataa wanaume ambao wamekuwa wakijaribu
kuonyesha upendo wao kwa muda mrefu. Na majibu tuliyoyapata yalikuwa
mamoja, yaani walikuwa wakilenga swala moja kuu ambalo lilikuwa
likiwachosha.
Nalo ni...
Wanaume ambao hujionyesha kuwa ni watulivu na wasiokuwa na pupa.
Ok mbona wanaume aina hii wanawachosha wanawake na mwishowe kuwakataa?
Kulingana na maoni ya wanawake hawa ni kuwa wanaume aina hii huonyesha
tabia ambayo inawafanya automatically kuwaingizwa katika kategoria ya
'marafiki'
Hivyo kutoonyesha matamanio yako kama mwanaume kwa mwanamke ama
kuonyesha kuwa wewe ni mwanaume mnyenyekevu kunakuchongea wewe katika
azma yako ya kumshawishi mwanamke yeyote.
So makosa ya mwanaume aina hii ni yapi?
Ok hebu tuichukulie mifano ifuatayo...
Je wewe ushawahi kuaproach mwanamke na kumwomba namba yake ya simu kwa
kumwambia: "Hello, unaweza kuniazima namba yako ya simu? Labda siku moja
tunaweza kuwa pamoja..."
Ama unapomuagiza kutoka naye deti unamwambia: "Hi, kikundi changu
kinakutana siku ya Jumamosi, naonelea uungane nasi, itakuwa siku ya
furaha..."
So tatizo hapa linajitokeza kivipi?
Wanawake wanapenda mwanaume mwenye nishati, nguvu na uwezo wa kuamua
haraka haraka, mwanzo akiona mwanaume aina hii huwa anasisimka papo
hapo. Unamuacha na maswali ya kutaka kujua zaidi kuhusu maisha yako ya
undani.
So kuonyesha nishati aina hii utafanyaje?
Wakati mwingine ambapo utakutana na mwanamke unamwomba namba yake, toa
simu yako, mpatie na umwambie hivi: "Shika. Niwekee namba yako kwa simu
yangu. Ntapenda nikutoe out siku moja."
Kufanya jambo hili moja pekee kutakuwa kumekufanya ujitokeze kama
mwanaume mwenye kujiamini, mwenye nguvu, na nishati ambaye anapigiwa
upato na wanawake wengi. Na kamwe hatakuweka katika kategoria ya 'friend zone'
Ni rahisi ama?
Ok wakati mwingine unapoaproach mwanamke nataka uonyeshe nishati yako
kama mwanaume, nataka uonyeshe kuwa wewe si mwanaume wa kuingizwa katika
kategoria ya 'urafiki'. Mwanzo nataka uonyeshe ushupavu wako kwa
kuzitumia mbinu tatu ambazo zitamfanya mwanamke akuheshimu sehemu yeyote pale ambapo atakuona. Nataka udhihirishe ya kuwa wewe ni mwanaume alpha ambaye hatikishiki na jambo lolote lile.
No comments:
Post a Comment