1. Anakupigia simu mara kwa mara na kukuuliza siku yako imeendaje.
Anafanya hivi kirafiki na kwa upendo, haigizi. Anakupenda kweli.
2. Anakutembelea mara kwa mara, anakuwa karibu na wewe kipindi unaumwa,
hii inamaanisha kwamba yupo tayari kukuvumilia katika shida na raha.
Mpende mwanaume huyu.
3. Anawapenda ndugu zako kama ndugu zake. Anaongea nao vizuri na
kusaidiana mambo ya hapa na pale. Mtizame kwa jicho la tatu huyu
mwanaume!
4. Anaongea na wewe kwa adabu na kwa upole, anakukosoa bila wasiwasi
kama kuna mambo unaenenda visivyo. Anakuelekeza njia zilizonyoka..sio wa
kumuacha huyu!
5. Hakulazimishi kufanya mapenzi. Anakupenda sana kiasi kwamba hawezi
kukulazimisha jambo ambalo hauko na hiari nalo. Yupo karibu na wewe
wakati wote na sio tu anapokutaka kimapenzi, huyu ni bonge la bwana.
6. Anakusaidia fedha pale unapokua umekwama kabisa, yuko na jukumu la
kukusaidia kiuchumi. Anapenda kukupa kile ambacho amejaaliwa nacho. Hana
mkono wa birika, Huyu anakupenda!
7. Anazungumzia future yake na wewe, mipango ya baadae pamoja na wewe,
huyu anayo dhamira ya dhati kutoka moyoni mwake ya kukufanya uwe mkewe.
No comments:
Post a Comment