Ikiwa wale wanaokusudia kuoana hawataki kuwa na mashaka mengi wala kuwa
na mambo kadha wa kadha ya kuwanyima furaha baada ya kufunga ndoa,
imewalazimu kufikiria vyema na kwa moyo wote juu ya jambo hili na kwa
wakati huu kabla ya kuoana. Ikiwa hatua hii itafanywa kipumbavu, itakuwa
mojawapo ya mambo makuu mno yawezayo kuharibu mafao ya mvulana ama
msichana wawapo wamekwisha kuoana. Kwao maisha yataonekana kuwa kama
mzigo wa laana. Kaitka ulimwengu huu hakuna awezaye kumnyima mwanamke
furaha, ama kumharibia maisha na kufanya yamuelemee na kumchoma moyo
zaidi ya mumewe; na hali kadhalika hakuna mwenye uwezo wa kupooza
matumaini na jitihada za mwanaume na kuposha nguvu zake, kuharibu mvuto
wake na maendeleo yake zaidi ya mkewe. Mara nyingi ni tangu dakika ile
baada ya harusi ambapo maisha huanza kuwaelemea wanawake na wanaume
wengi. Ndoa ni jambo ambalo lina mvuto katika ulimwengu huu, na litakuwa
na mvuto katika ulimwengu ujao pia.
Wengi hawaelewi vyema muungano huu wa ndoa. Wengi wao hudhani ya kwamba,
muungano huu ni mojawapo ya njia ya kufikia upeo wa furaha; lakini
laiti wangefahamu kiasi kidogo tu cha uchungu walionao wale
waliounganishwa kwa kiapo cha ndoa ambacho kimewafunga kwa minyororo
wasiyothubutu kuikata, hawangeshangaa kwa maelezo haya. Ndoa nyingi
zinazofungwa huwa ni mkatale wa huzuni. Kuna maelfu ya watu
waliounganishwa katika ndoa lakini hawapatani.
Wale wanaofikiria kuoa ama kuolewa ni lazima wajishauri vyema kuhusu
hali na mwenendo wa ndoa wanayokusudia kuwa nayo. Ni lazima vijana
wafanye uchunguzi wa kutosha katika mambo yanayohusu kuchagua mpenzi na
kufanya uchumba. Ewe kijana mwenzangu, jihadhari ili kile unachodhania
kuwa ni dhahabu ama lulu safi kisije kikawa takataka tu. Jambo hili
halipaswi kufanywa haraka. Wakati ungali bado unaweza kupenda, jihadhari
usije ukapenda kama kipofu.
Fikiria sana uone kama maisha yako na yule unayemchagua kuwa mwenzi wako
wa maisha yatakuwa ya furaha ama ya kutopatana na kuhuzunisha baada ya
harusi. Wanawake na wanaume wengi wameoana kana kwamba jambo la pekee
lililowapasa kulijali ni kuwa wanapendana au la. Kuchagua mwenzi wa
maisha kwafaa kufanywa kwa busara ili kuwawezesha wazazi na watoto pia,
kuwa na hali nzuri kiroho, kiakili na kimwili.
Mambo ya kuzingatia katika kuchagua msichana wa maisha
Kijana wa kiume unapaswa uchague msichana ambaye atasiamama kando yake
na ambaye ataweza kuchukua sehemu ya mzigo wa maisha yake, mke ambaye
mvuto wake utamfanya mumewe na heshima na kumwezesha kuwa na mwenendo
mwema, na ambaye kwa jili ya upendo wake, atamfanya kuwa na raha
maishani mwake.
Ewe kijana wa kiume na mwanaume mwenzangu naomba ujishauri kwa uangalifu
mkubwa kuhusu mambo haya yafuatayo na bila shaka kama yakizingatiwa kwa
umakini yatakuwa msaada mkubwa kwako wewe mvulana mwenye nia ya dhati
ya kuoa;
Je huyo unayekusudia kumuoa atafanya nyumba yenu iwe ya furaha?
Je yeye ni mwangalifu awezaye kutunza mali, ama akishaolewa hatapoteza
mapato yenu tu bali pia atazitawanya mali zenu huku akionyesha upendo wa
juu juu tu?
Je huyo unayemtaka awe mwenzi wako ana hofu na kumcha Mungu?
- Je ana afya njema?
- Je ana bidii katika kazi?
- Je msafi wa kimwili na kiroho?
- Je ni mlevi?
- Je ni mtii, mnyenyekevu na mwenye adabu?
- Je anajiheshimu na kuvaa mavazi yenye heshima?
- Je ni mwaminifu?
- Je ni mtu anayetunza siri katika uhusiano wenu?
- Je ni mkristo, mpagani au mwislamu mwenzangu?
- Je mwenendo na tabia yake ikoje kwa wakati huu?
Nafahamu kwamba mvulana ambaye ametumbukia katika kisima cha mapenzi
atayadharau maswali haya kana kwamba hayana maana wala manufaa yoyote,
lakini hayana budi kufikiriwa kwa umakini na kwa ungalifu mkubwa zaidi.
Wakati wa kuchagua mke, tafakari na uelewe tabia na mwenendo wale, uone
kama atakuwa mstahimilivu na mwenye bidii. Uone kama atachoka kuwatunza
wazazi wako walo wazee wakati ule ambao watahitaji msaada wako. Uone
kama atakushawishi utengane nao na kukushawishi umpende yeye peke yake
na kusahau baba na mama ambao badala ya kupata binti watakuwa
wamempoteza mwana.
Mambo ya kuzingatia katika kuchagua mvulana wa maisha
Kabla msichana hajatoa mkono wake kwa mvulana na kuvishwa pete ya
uchumba, kwanza na ajiulize kama yule mvulana wanayekaribia kuoana
anafaa ama vipi. Mwenedo wake na tabia yake ya siku zilizopita ulikuwa
wa namna gani? Je maisha yake ni masafi? Je upendo akuonyeshao unatoka
moyoni na unaonyesha heshima na tabia njema ama ni upendo wa hivi hivi
tu? Je anao mwendendo ambao utanifanya kuwa na furaha? Mimi kama mke
nitaweza kuwa na furaha niwapo kwake? Je ataniruhusu kudumisha tabia
yangu na kunipa uhuru ama itanilazimu kutupilia mbali yote na kufuata
matakwa yake? Maswali kama haya yakizingatiwa kwa busara yatakuwa na
manufaa sana katika maisha yajayo ya msichana ambaye anatarajia kuolewa.
Kila msichana anayetamani kuwa na familia yenye furaha na amani, ambayo
haitakuwa na udhaifu wala huzuni katika siku za baadae na ajiulize
maswali haya kabla ya kutoa ukubali wake wa upendo.
- Je huyo unayemtaka awe mwenzi wako ana hofu na kumcha Mungu?
- Je ana afya njema?
- Je ana bidii katika kazi?
- Je msafi wa kimwili na kiroho?
- Je ni mlevi?
- Je ni mtii, mnyenyekevu na mwenye adabu?
- Je anajiheshimu na kuvaa mavazi yenye heshima?
- Je ni mwaminifu?
- Je ni mtu anayetunza siri katika uhusiano wenu?
- Je ni mkristo, mpagani au mwislamu mwenzangu?
- Je mpenzi wangu anaye mama?
- Je tabia ya mama yake ikoje?
- Je anatambua wajibu wake kwa mamaye?
- Je anajali upendo na furaha ya mama yake?
Ikiwa hajali wala hamheshimu mama yake, kweli ataweza kuonyesha heshima na upendo, wema na usikivu kwa mkewe?
Je harusi itakapokwisha atakuwa na huruma kwa makosa yangu ama atakuwa ananikosoa mara kwa mara huku akiwa mgomvi na mkali?
Katika kuyajibu maswali haya shauklu nyingi yaweza kupishia mbali makosa
na kasoro za mchumba wako, lakini upendo wa kweli hautaficha neno.
Katika kuchagua mwenzi wa maisha, msichana na achague mvulana mwenye
tabia na mwenendo safi wa kibinadamu, aliye na bidii, mwangalifu, mwenye
heshima na aliye mwaminifu na mnyofu.
Ikiwa umefanya uchumba na mtu ambaye huelewi vyema tabia yake, usidhani
kushika uchumba kutakulazimisha kuchukua kiapo cha ndoa na kuungana na
mtu ambaye humpendi na ambaye wala hutamheshimu maishani mwako.
Jihadhari sana unapofanya uchumba wenye masharti; lakini hata ukiwa ni
uchumba wenye masharti, ni bora mara kumi kuuvunjilia mbali huo uchumba
kabla ya kufunga ndoa kuliko kuja kuvunja ndoa baadae kama wengi
wafanyavyo.
No comments:
Post a Comment