Utafiti
wa Chama Cha Madaktari Bingwa wa Akina Mama (FIGO) mwaka 1990 ulionesha
kuwa sababu kuu ya mwanamke kutoshika mimba ni hitilafu katika mirija
ambayo kitaalam huitwa Tubal Factor ambapo asilimia 25-35 hutokana na
magonjwa ya mirija ya uzazi.
Katika
utafiti huo, iligundulika kuwa asilimia 30-40 husababishwa na hitilafu
ya kupevuka mayai kitaalam huitwa Ovulatory Factor. Sababu nyingine
zilielezwa kuwa ni hitilafu za ukuta wa uzazi, yaani Endometriosis au
mwanamke kuwa na uvimbe kwenye mji wa uzazi.
Ile
sababu ya matatizo yanayosababishwa na kupevuka kwa mayai au kutotolewa
kwa mayai au kutoka kidogo sana, hutokea baada ya vichocheo vinavyoitwa
Hormone ya Godotrophins Relising Hormone kutoka sehemu ya tezi la
kwenye ubongo ujulikanayo kama Hythalamus kunakosababishwa na tezi
kutofanya kazi vizuri.
Kwa
sababu hiyo, mayai hutolewa kidogo au kutotoka kabisa na kusababisha
baadhi ya wanawake kutoenda kwenye siku zao za hedhi wakati muda wa
kufanya hivyo haujafika.
Sababu
nyingine zinazofanya mwanamke kushindwa kushika mimba huwa ni kuziba au
kuwa na upenyo mdogo wa kusafirisha mayai kutoka kwenye tezi la mfuko
wa uzazi, lijulikanalo kitaalam kwa jina la Ovary.
Hali
hiyo ya kuwa na upenyo mdogo husababishwa na maambukizi ya bakteria
kwenye mirija pamoja na mji wa mimba na tatizo hilo kitaalam huitwa
Pelvic Infections. Mwanamke akiwa na tatizo hili atajisikia maumivu
makali wakati wa kufanya tendo la ndoa.
Wanawake
wengine hushindwa kupata mimba kutokana na kuwa na hitilafu kwenye mji
wa mimba, kama vile kuwa na uvimbe kwenye kizazi au vinyama kuota kwenye
mji huo wa uzazi Endometritis au kuwa na matatizo ya kuzaliwa nayo ya
mji wa uzazi kuwa mdogo sana.
Tatizo
lingine ni mwanamke kuwa na hitilafu kwenye shingo au mlango wa uzazi
kitaalam huitwa Cervical Factors, kama vile maumbile yasiyo ya kawaida,
jambo ambalo husababisha usumbufu mji wa kizazi kuwa mbali na uke,
hivyo kusababisha ucheleweshaji wa kusafirisha mbegu za kiume Sperms.
Tatizo lingine ni kuwa, kwenye mlango wa uzazi, huzalishwa utelezi mwingi ambao unaweza kuleta hitilafu katika kufanya kazi.
Sababu
nyingine ni mwanamke kuwa na matatizo kwenye uke kama vile kuzaliwa na
maumbile ambayo siyo ya kawaida kama kuwa na uke usioshikana yaani
Vaginal Septum pia kutokwa na uchafu mwingi Virginal Discharge.
Ili kujua tiba na ushauri wa kitaalam fuatilia wiki ijayo siku kama ya leo.
Mafindo findo
Leo kwenye
ukurasa huu tutaangalia tiba ya ugonjwa wa mafindo findo (Tonsils) watu
wengi huangaika na gonjwa hili ambalo huambukizwa kwa bacteria hasa
kipindi cha baridi, hutokea wakati mwingine kama mafua, kwani huathiri
koo, husababisha anayeumwa kushindwa kumeza chakula na hata mate, pia
upumuaji wa mgonjwa anapolala huwa ni wa tabu.
Maji ya chumvi
Kama
unasumbuliwa na tatizo hili uwe mkubwa au mdogo, tumia maji haya kwa
kuchanganya kijiko kimoja cha chumvi na maji ya vuguvugu, kisha sukutua,
rudia kusukutua mara kwa mara kwa ajili ya kupata nafuu.
Jinsi ya kutumia Limao kama tiba
Chukua
glasi ya maji salama ya kunywa, weka pinch ya Chumvi changanya na juisi
ya limao moja, kisha weka kijiko kimoja cha asali, baada ya kupata
mchanganyiko huo kunywa kidogo kidogo mara mbili kwa siku.
Bizari
Bizari ya manjano ina uwezo mkubwa wa kumaliza tatizo.
Utumiaji wake
Chukua
kijiko kimoja cha unga wa bizari weka kwenye glasi ya maji moto
changanya na chumvi kidogo. Ukishapata mchanganyiko huo sukutua mara kwa
mara hasa kipindi cha kwenda kulala, itakusaidia kuondoa maumivu.
Mdarasini
Mdarasini unasaidia kutibu tonsils kama utafuatilia kutumia kitiba ni mzuri sana
Jinsi ya kutumia
Chukua kijiko kidogo cha unga wa mdarasini, weka kwenye maji ya moto.
Changanya na vijiko viwili vya asali.
Kunywa taratibu, tumia mara tatu kwa wiki moja.
No comments:
Post a Comment