“Hivi wale rafiki zako wanafanya
kazi kweli?” Peter aliniuliza, nilinyanyua uso wangu na kuonyesha
mshangao kidogo kwani alikuwa akiwafahamu rafiki zangu na alikuwa
akifahamu kazi walizokuwa wakizifanya.
“Rafiki wapi hao?” Nilijifanya kutokumuelewa.
“Si rafiki zako wale ambao kila siku uko nao, Judy na nani yule mwingine, yule muongeaji sana…Happy…”
Tulikuwa tumekaa sehemu tumepumzika mimi na mume wangu. Peter mara nyingi hupenda kunitoa out mwisho wa wiki anapokuwa hayupo bize kitu ambacho sikuwanikikipenda sana kwani kilikuwa kikininyima fursa ya kufurahia maisha na rafiki zangu.
Nampenda sana mume wangu lakini kwa
wakati huo baadhi ya mambo aliyokuwa akiyapenda yeye mimi sikuwa
nikiyapenda hivyo hata katika ‘mitoko’ hiyo sikufurahia sana.
“Wanafanya kazi, si wote wako wizara ya fedha tunafanya….” Nilijibu
lakini kabla sijamaliza kuongea meseji ya Whatsapp iliingia katika simu
yangu, nilijikuta tu nafungua, ilikuwa meseji kutoka kwa Judy ikisema
“Tupo hapa nyuma yenu, naona leo umeamua kutoka na
mseyeee…unakunywa maji tu hapo”. Nilijikuta natabasamu na kugeuka nyuma,
kumbe mume wangu aliwaona akina Judy ndiyo maana akaamua kuuliza.
“Nawaona pale…” Alisema mume wangu baada ya mimi kugeuka.
“Si wamekuja kula kama sisi, kwani ni vibaya?’ Nilianza kuwatete
hata kabla mume wangu hajasema kitu. Nilijua alichokuwa akimaanisha
lakini nilijifanya kuzuga tu, sikutaka awaongelee marafiki zangu vibaya.
Wakati tukiendelea kula, waliingia wababa wawili wa makamo na
kwenda kukaa kwenye meza ya akija Judy, mimi sikuwaona wakiingia ila
nilistushwa na kelele za Judy wakati wana wa ‘hug..ana’ walikuwa
wakipiga kelele kana kwamba walikuwa wao tu, mule ndani, karibu wateja
wote waligeuka kuwaangalia na kuwashangaa kwa mambo waliyokuwa
wakiyafanya na wale wazee ambao walikuwa sawa na Baba zao.
Nilimuona mume wangu akibadilika
kabisa usoni, alionyesha dhahiri kukerwa na kile kitendo na kabla hata
hatujamaliza vinywaji alimuita mhudumu kuomba bili.
“Tunaondoka?” Niliuliza kwa mshangao.
“Sijisikii vizuri, nahisi nitakuwa na malaria…” Alijaribu
kudanganya lakini nilimuelewa, ingawa nilikasirika kwani nilitamani
kuendelea kukaa mule ndani, nilijifanya mke mwema na kumuambia pole
kisha kumuunga mkono. Wakati tunatoka Judy aliniita kwa sauti ya kelele
kelele akinitaka niende kwenye meza yao, nilimuangalia mume wnagu
nikaona kanikodolea macho ya hasira nikaamua kuzuga kwa kuwapungia tu
mikono.
“Nahawa ndiyo unasema ni marafiki zako!” Mume wangu aliongea kwa
kunung’unika kwa suti yachini, nilimsikia lakini nilijifanya kama
sijasikia.
********
Urafiki wangu na kina Judy ni wa muda mrefu sana tangu tukiwa
chuoni, hata wakati nakutana na mume wangu alinikuta nao na urafiki
uliendelea mpaka wote tulipobahatika kuajiriwa sehemu moja lakini
vitengo tofauti. Kama mimi Judy alikuwa ameolewa na Happy alikuwa na
mchumba wake ambaye walikuwa wanasumbuana kila siku. Mwanzoni mume wangu
alikuwa akiwapenda na kuwaheshimu lakini ghafla alibadilika na kila
mara alikuwa akinionya kuhusu wao jammbo ambalo lilikuwa likinikera
sana.
Kila mara nilipotaka kutoka na
kuwaambia kuwa natoka na kina Judy alikuwa akikasirikia na kunipa maonyo
ya hapa na pale. Uzalendo ulinishinda na siku moja nikaamua kumuuliza
Happy nini kilitokea. “Maana shemeji yenu kila siku nikimuambia natoka
na nyinyi ni maneno hayaishi utafikiri nimemuaga naenda kwa Mchepuko!”
Nilimuuliza Happy.
“Yaani acha tu ndugu yangu…” Alianza kuelezea,
“Nini tena ndugu yangu?”
“Inamaana shemu hajakuambia, au unanichora tu hapa?” Aliuliza kwa wasiwasi.
“Kaniambia nini? Kwani mlifanya nini? Au mshaharibu tena? Unajua mnanniharibia?” Nilianza kulalamika.
“Wewe unajua bwana, haiwezekani kitu kama kile asikuambie!” Happy alirefusha mjadala kitu ambacho kilianza kunikera.
“Niambie bwana! Yule mwanaume huwa hana mambo ya umbea, isitoshe si
unamuona alivyo mpole, yeye kila siku ni kusema angalia na marafiki
zako!” Niliongea kwa hasira kidogo. Happy alikuwa naanitibua na nilikuwa
na hamu kubwa ya kujua nini kilimfanya mume wangu kuwabadilikia wakati
aliwajua miaka kibao nyuma.
“Basi ni hivi….” Happy alianza kuelezea.
“Mwenzako si nilipataga danga moja hivi. Kama kawaida mzee mzee flani hivi amazing…”
“Mhhh!….” Niliguna huku nikijiweka sawa kupokea umbea.
“Basi Bwana, huyo Baba mimi sikujua kuwa anafanya kazi wapi, lakini
alikuwa mgeni na alikuja hapa kibiashara na kama unavyoijua viwanja
vyangu, Kempisk, New Africa na wine yangu ya kuzugia. Mzee kaniona
kajisogeza na kwakuwa alikua na mkwanja sikulaza damu, tukapeana
mawasiliano na kama kawaida nikazuga mshamba mshamba kumbe na msoma tu.
Tukaongea tu kawaida na siku ile nikaondoka, huwezi amini namuaga kanipa
laki mbili ya Tax nikasema yeesss…
Basi bwana akaniambia tukutane kesho
yake, kesho yake kanipigia simu kaniambia kuwa atakuja na rafiki yake
hivyo kama na mimi nina rafiki yangu basi nije naye. Kama kawa
nikamchukua Judy na kwakuwa walitaka mzigo mpaka asubuhi Judy kamuaga
Mumewe nina umwa na sina mtu wakunisaidia, shem kamleta mpaka nyumbani
kaniangalia nimelala sijiwezi basi kamuacha kwangu”. Tulicheka kwa
nguvu, huku nikitingisha kichwa.
“Mna mambo nyie…” Nilisema kisha akaendelea.
“Basi bwana tukafika tukanywa na kula, yaani alikuja na kijana wake
‘mhandsome’ huyo anasema ni mfanyabishara mwenzake mkenya, mimi
mwenyewe nilimtamani ila kwakuwa nilishashikiliwa na mzee nikaamua
kumuachia Judy. Basi wakati tunashikana shikana pale hamad ndiyo shem
anaingia. Hatuna hili wala lile ikabidi tuuchune tu. Basi kumbe wale
watu walikuja kufanya biashara na walikuwa wakutane na shem pale, shem
alikuja na yule kaka mrefu, John yule wanayefanyanaye kazi. Sisi
tukazuga pale tukatambulishwa na kujifanya hatujuani nao wakauchuna sasa
kilichomkera shem nadhani ni kule kushikana shikiana kwani tulishalewa.
Hakusema chochote lakini tangu hapo hata tukikutana anakuwa mkimya tu”.
Alimazlia kuongea na kunipa picha kamili.
“Ndiyo maana, sasa anafikiri na mimi nafanya hayo maupuuzi yenu!” Niliongea huku nikitingisha kichwa.
“Mumeo nayeye mshamba tu! Samahani lakini angejua unavyompenda!
Mapedeshee unavyowatolea nnje angekuheshimu maisha!” Happy alimaliza
kuongea wote tukacheka na kugonga.
“Nampenda sana siwezi msaliti, angalau nimzalie hata kamtoto kamoja
afurahi maana ana wivu sana”. Niliongea huku nikishika tumbo, miaka
miwili ya ndoa ilikuwa imepita na baada ya kuhangaika nilifanikiwa
kupata ujauzito ambao ulikuwa na miezi miwili.
*******
Baada ya kuambiwa ile story kidogo nilianza kumuelewa mume wangu
ingawa sikuacha urafiki na kina Judy bali nilibadilisha mbinu tu.
Nilijua alihisi kuwa kama Judy ana mume na anaweza kuchepuka tena bila
kujali kufumaniwa basi inawezekana na mimi hufanya hivyo hivyo, kwani
mara kadhaa huwa ninatoka nao sehemu za starehe bila kuongozana na mume
wangu na kwakauwa alikuwa akiniamini aliniruhusu bila kinyongo chochote.
Ili kumpunguzia wasiwasi nilipunguza
kutoka na kina Judy na hata nilipokuwa nikitoka nao sikumuaga tena kuwa
natoka nao, nilikuwa nikimpigia simu mdogo wangu na kumuambia anipitie
kama tunatoka naye kisha namrudisha na kumuacha chuoni kwani alikuwa
akisoma IFM. Kwa kufanya hivyo mume wangu akawa hana wasiwasi tena na
alifurahia mimi kuacha kampani na akina Judy.
Mara kadhaa yaani bila sababu yoyote
alikuwa akija na kunikumbatia na kuaniambia nakupenda huku
akinikumbusha “Nafurahi umeachana na wale mashoga zako…” Aliongea bile
kuniambia kwanini lakini kiuhalisia usoni alionyesha tabasamu
lililoashiria furaha ya kweli. Namimi nilifurahi kwani niliweza kumpa
amani ya roho na kurejesha amani ndani ya nyumba huku bado nikiendelea
kufurahia urafiki na kina Judy.
Waliosema za mwizi ni arubaini
hawakukosea, weekend moja tana siku ya jumapili, Juddy alinipigia simu
na kutaka tutoke usiku wake, sikumkubalia kwani ilikuwa Jumapili na
sikuwa nikijisikia vizuri, wakati huo ujauzito wangu ulishafikia miezi
mitano tumbo lilishakuwa kubwa hivyo sikutaka kutoka toka. Ingawa mume
wangu alikuwa amesafiri lakini bado sikuona haja ya kutoka tena usiku wa
Jumapili wakati kesho yake nilihitaji kazini.
Nilimkatalia Judy lakini wapi
hakunielewa, jana yake yeye na Happy walipata wanaume ambao waliwanywea
pombe na kuwachuna vyakutosha bila kuwapa ‘mzigo’, watu hao walitaka
kukutana tena kwa mazungumzo hivyo walijua kama wataenda wawili lazima
watataka mechi kitu ambacho hawakuwa tayari kukifanya, walichohitaji wao
ni hela tu, hivyo kwa kwenda na mimi ingesaidia wao kuondoka salama.
Judy alilalamika sana mpaka nikaona
kero hivyo nikaamua kumsindikiza na kwakua mume wangu hakuepo basi
hakukuwa hata haja ya kumpigia simu mdogo wangu, nilimuaga tu mfanyakazi
wa ndani kuwa naenda kwa Mama kisha nikaondoka, njiani nilimpigia simu
mume wangu nakumuambia nazima simu ili nilale kwani nilikuwa sijisikii
vizuri, akanitakia usiku mwema nikazima simu na kwenda kula maisha.
Tulifika nikiwa nimeongozana mimi,
Juddy na Happy, tulikutana na vijana wawili wamakamo hivi kama mume
wangu, kidogo nilipata amani kwani awali nilijua kuwa tutakutana na
wazee ambao ndiyo aina ya wanaume akina Judy hupenda kwakuwa hutoa hela
sana. Baada ya kusalimiana na kutambulishana, walianza kuagiza kunywa na
kula, huku wakipiga stori za ya mambo ya jana.
Wale vijana walikuwa wastaarabu
sana, kitu ambacho pia kilinifurahisha, kwani tofauti na rafiki zangu
ambao walilewa na kuanza kuwashika shika wale vijana wao walikuwa
watulivu wakiongea mambo ya maisha, hawakuonyesha hata dalili kuwa
waliwahitaji kimapenzi. Muda ulikuwa unakwenda kwa kasi na ilipofika saa
sita usiku nilianza kuwasihi rafiki zangu tuondoke lakini hawakuwa
tayari kuonndoka, bado walikuwa wakinywa na kufurahia wakitaka kuendelea
kubaki.
Nilitaka kuondoka na kuwaacha lakini
kwa namna walivyokuwa wamelewa nilijua wangefanya mambo ya ajabu, hivyo
niliamua kuaga mimi na kuwaomba wale akaina kaka waturuhusu tuondoke.
Hawakuonyesha hata kuwa na wasiwasi, waliniambia tumalizie vinywaji
tulivyokuwa tunakunywa watupeleke nyumbani kwani hatukuja na gari, mimi
huwa sipendi kuendesha usiku na nilijua wenzangu watalewa kushindwa
kuendesha.
Nilikubaliana nao, lakini kabla ya
kumalizia kinywaji, mmoja wa wale wakaka alinisogelea na kuniinamia kama
anataka kuninong’oneza kitu, bila hiyana na mimi niliinama kumsikiliza,
hii ilinifanya kuondoa macho yangu mezani. Kweli alininong’oneza
akiniuliza kama Judy alikuwa mke wa mtu kwani mbali na kuvua pete ya
ndoa lakini kidole kilikuwa na alama ya pete, nilimjibu ndiyo nikitaka
azidi kuona hamna haja ya kuondoka nao.
Basi alirudi na kukaa bila kusema
chochote, nilichukua kinywaji changu na kuanza kumalizia harakaharaka,
nilipomaliza niliwaomba wale akina kaka waturuhusu kuondoka, wakaomba
nao wamalizie vinywaji vyao hivyo nikawa nimekaa tu nawasubiri
wamalizie. Walimaliza vinywaji vyao na kutuambia tuondoke, wenzangu
walisimama ila kila nilipojaribu kusimama, nilishikwa na kizungu zungu,
miguu ilikosa nguvu na kushindwa kunyanyuka kabisa. Sikujua ilikuwa ni
nini kwani sikunywa pombe kabisa na muda mchache uliopita nilikuwa
najisikia vizuri. Wale wakaka kuona vile walinisaidia kunyanyuka na
kunikokota mpaka kweny gari tukaondoka.
Nilipoingia kwenye gari tu
nilishikwa na usingizi na sikuzinduka tena mpaka asubuhi nilipoamka na
kujikuta nipo kwenye chumba na kitanda kigeni kabisa. Nilikuwa gest
nimelala kitandani uchi wa mnyama, niligeuka pembeni na kukuta Judy naye
amelala pembeni yangu akiwa uchi wa mnyama kama mimi, pembeni yake
kulikuwa na condoma nyingi zimetumika na katika shuka kuliku ana damu
damu ambazo hazikuwa nyingi sana.
Kila kitu mule ndani kilikuwa
shaghalabaghala, nguo zetu zikiwa zimetupwa chini, nilinyanyua mkono
kujaribu kumuamsha Judy lakini hakuamka, nilinyanyuka taratibu kutafuta
nguo ya kuvaa, mwili ulikuwa mzito na niliposimama tu nilianza kusikia
maumivu sehemu za siri na sehemu za haja kubwa. Nilijaribu kuwaza
kukumbuka kilichotokea usiku ule lakini nilishindwa, sikuwa na
kumbukumbu kabisa.
Nilikuwa nakumbuka tu kuingia kwenye
gari na wale vijana lakini sikukumbuka kuingia gest, lakini kichwnai
nilishapata picha ya kilichokuwa kimetokea. Wakati nikiwa najikongoja
kuokota nguo zangu ili nijistiri niliona kikaratasi kilichokuwa mezani
ambacho juu yake kiliwekewa shilingi mia ili kisipeperuke. Nilijisogeza
taratibu huku nikiugulia maumivu na kwenda kukiokota, nilikichukua na
kuanza kukisoma.
“Washenzi nyie! Mlifikiri mtakula
tena hela yetu kijinga jinga, sisi watoto wa mjini kama nyie!”
Kiliandikwa kile kikaratasi, wakati huo Judy nayeye alishaamka. Huku
nikiwa na mawazo nilienda kukaa kitandani, nguo zangu nimezishikilia
mkononi hata sikuvaa, kichwa kilikuwa kinauma, kwa maumivu ya kawaida na
maumivu ya mawazo kuhusu kilichotokea.
“Tuko wapi?” Judy aliniuliza huku nayeye akijishangaa, akili ilishamrejea.
“Hata mimi sijui…”
Nilimjibu kwa kifupi, kichwa changu kilikuwa kizito nikiwaza mambo
mengi. Nilimuona Judy akinyanyuka nayeye akiwa anatembea kwa
kuchechemea, ilikuwa aibu, sikuweza hata kumuangalia, niliangalia tu
chini nikiwa sijui hata nini chakufanya. Wakati huo bado tulikuwa
hatujajua kuwa Happy yuko wapi kwani mara ya mwisho nakumbuka tulipanda
naye gari na wale wakaka wawili
*******
Simu zetu zilikuwa zimezima chaji
hivyo tulishindwa kumtafuta Happy na kuamua kuvaa harakaharaka na kutoka
kwa aibu. Tulipita mapokezi bila kusema chochote, tukapanda bajaji
iliyokuwa imepaki jirani na ile gest na kuondoka. Kwa hali niliyokuwa
nayo nisingeweza kwenda nyumbani moja kwa moja, pia Judy asingeweza
kwenda nyumbani kwani yeye mume wake alikuwepo.
Tuliamua kwenda kwa Happy kwani
alikuwa akiishi peke yake, bahati nzuri tulimkuta na kama sisi aliamka
asubuhi akiwa hajui nini kilitokea jana yake. Tofauti nikuwa hakukutana
na meseji, na alipojaribu kutupigia simu, simu zetu zilikuwa
hazipatikani. Hatukuwa na chakufanya zaidi ya kuoga na kila mtu kuanza
safari ya kuelekea kwake. Bado simu ilikuwa imezima na nilijua Peter
alikuwa amenitafuta kwa muda mrefu na ninavyomjua alikuwa amempigia Dada
wa kazi kujua kwanini simu haipatikani.
Nilifika nyumbani na kumkuta Dada
anafanya usafi na kama nilivyo tarajia kitu cha kwanza alichoniambi
baada ya salamu nikuwa Peter alipiga simu kuniulizia kwani simu zangu
zote zilikuwa hazipatikani. “Ukamuambiaje” Niliuliza huku nikitetemeka
kwa wasiwasi, kichwnai nikiwaza “Kama akimuambia sijalala humu
itakuwaje…” niliwaza huku nikisubiri jibu leke kwa hamu.
“Sikumuambia chochote, mimi nilimuambia tu asubuhi uliondoka na
kusema unaenda kwa Mama labda simu zilizima cha….” Bila kujijua
nilijikuta na ruka, kumvamia na kumkumbatia kwa kama dakika mbili hivi,
jibu lake lilikuwa limesuluhisha kila kitu, bado nilikuwa na maumivu ya
kimwiloi lakini angalau nili[ata faraja kidogo.”
“Sitakusahau mdogo wangu, niambie ni kitu gani chochote unataka…”
Niliongea huku nikitabasamu tu, binti wa watu hata hakuwa na shida na
chochote, alikataa na kuniambia niliondoka jana kwenda kwa Mama akasema
asubuhi.
Sikujali kuhusu kukataa kwake,
ilimradi alishanisaidia kwangu ilitosha, niliingia ndani nikaweka simu
kwenye chaji, ilipoingia chaji kidogo tu nikaiwasha kumpigia mume wangu.
Ziliingia meseji nyingi mfululizo za Peter akiulizia hali yangu kwani
jana yake nilimuambia nalala mepema kwakuwa sikuwa nikijisikia vizuri.
Alihisi labda nimezidiwa, nilimpigia na tukaongea sana, nilimuomba
msamaha kwa kutokubeba chaja.
“Wewe leo umekuwaje, yaani asubuhi
hata text?” Aliuliza kwa sauti ya upole, machozi yalianza kunitoka,
nikweli haikuwa kawaida yangu kutokuwasiliana ma mume wangu asubuhi
anapokuwa mbali, nilikuwa msumbufu sana kuhakikishaa amevaa nguo
nilizompangia kuvaa, amekunywa chai na mambo mengine. Niilimdekeza sana
Peter kiasi kwamba asingeweza hata kuvaa boxer bila kuniambia kuwa
amevaa ipi, kila akisafiri nilimpangia ngupo za kuvaa tangu anaondoka
mpaka kurudi nikimuambia na siku za kuvaa.
“Nisamehe mpenzi, jana sikua
najisikia vizuri na asubuhi Mama nayeye kanichanganya…hata sijui
nimekuwaje siku hizi…sijui ni hiii mimba…yaani…” Nilianza kuongea mambo
mengi kwa lengo la kumchanganya na kweli nilifanikiwa. Peter alikuwa
akiongea vizuri mpaka nikajikuta nalia nikikumbuka kitu klilichotokea,
sikutaka anisikie nikilia hivyo nilimuomba nipumzike kwani nilikuwa
nimechoka sana, hakuleta kipingamizi alikata simu na kuniacha kupumzika.
*******
Maumivu sehemu zangu zasiri yalikuwa yamepungua, niliamka
nikijisikkia vizuri nikimshukuru Mungu kuwa yale yote yamepita. Muda
wote huo nilikuwa sijawasiliana na kina Judy kujua nini kilikuwa
kimeendelea na kusema kweli sikutaka kufanya hivyo yaliyokuwa yametoke
yalinifanya kujifunza na nilitaka kuanza ukurasa mpya bila wao. Hata
kama tutakutana kazini lakini urafiki wetu ungeishia huko huko na si
baada ya hapo.
Niliongea na Peter asubuhi na mchana
nili mmiss tena na kumpigia, tukiwa katikati ya mazungumzo kama ambavyo
hupenda kufanya aliniuliza “Mwanangu aanendeleaje?” Nilimjibu
anaendelea vizuri huku nikilishika tumbo na mara kadhaa hupenda kusema
nipe niongee naye na mimi kuweka simu tumboni, ingawa hasikii chochote
lakini huwa inampa furaha, alikuwa akifanya hivyo tangu nigundue ni
mjamzito hata kabla mimba haijaanza kuonekana.
Siku hiyo aliniambia na mimi
nilifanya vile kama kawaida, lakini baada ya kukata simu nilistuka kitu
kimoja. Tangu jana nilikuwa sijasikia mtoto akicheza, ingawa sikulitilia
maanani sana kwani akili yangu ilikuwa imevurugika, wakati huu
nililitilia maanani. Nilianza kuwa na wasiwasi lakini nikijipa moyo kuwa
atacheza, mpaka natoka kazini nafika nyumbani bado, hapo wasiwasi
ulizidi nilitamani kumpigia mama kumuuliza kwanini lakini nilihofia.
Nilipanda kitandani nikiwa na
wasiwasi kwani bado mtoto alikuwa hachezi mpaka siku tatu zilipita ndipo
nilipoanza kusikia maumivu makali sana tumboni kiasi cha kushindwa hata
kunyanyuka. Nilimuamsha Dada ambaye alimpigia Mama simu, akiwa na Baba
walikuja kunichukua na kunipeleka hospitalini, nilifika huko nikiwa na
maumivu makali sana baada ya vipimo niliambiwa kuwa mtoto alikua amefia
tumboni.
Nilishajua sababu, inawezekana kile
kitu walichoniwekea kwenye kinywaji ilikuwa kama sumu ambayo
ilisababisha kifo cha mwanangu (kwakuwa sikunywa pombe nilishajua
waliniwekea madawa ili nilewe). Nilikaa mule hospitalini kwa siku tatu
na kuruhusiwa, mume wangu alikuja siku ile ile baada ya kupata taarifa.
Alijitahidi sana kiunifariji akiniambia ni mipango ya Mungu, wiki nzima
mimi nilikuwa ni mtu wa kulia kwani nilijua ujinga wangu ndiyo ambao
ulisababisha yote hayo.
Nilisali sana kumuomba Mungu
anisamehe, kila nilipomuangalia mume wangu hasa alivyokuwa akinijali
basi nilizidi kuchanganyikiwa, nilikuwa na mume mwema sana ambaye
alinijali na nilikuwa nimemkosea sana. Mwezi mmoja baada ya kupona
kabisa nikiwa nimesharejea kazini na nikiwa nimeshaanza kusahau tukiwa
chumbani mume wangu aliniambia
“Nimejaribu kuvumilia lakini siwezi kuendelea kuishi hivi…”
Aliongea kistaarabu kabisa maneno ambayo yalinichanganya sikuwa
nikielewa sababu yake lakini hata kabla ya kuuliza aliendelea kuongea.
“Nilidhani nitaweza kusahau lakini hapana, sidhani hata kama nitaweza kukugusa na kushiriki tena na wewe tendo la ndoa….”
Aliongea huku akitoa simu yake na kunifungulia lundo la picha
akiniomba niziangalie. Nilianza na screenshort za group la Whatsapp
lililokuwa likijumuisha watu waliosoma na mume wangu sekondari. Kaka
mmoja alituma meseji kuwauliza wenzake waliokuwa Dar kuwa anatoka Mwanza
anakuja Dar ni wapi atapata Malaya wazuri.
Akaendelea tu kuuliza ndipo baadhi
walaipojitolea wakimuuliza kama ana pesa, ilionekana kama utani lakini
baadaye alipost na kusema kuna Malaya wamewapata lakini wamewalia pesa
zao halafu wakawazingua kuwapa ‘mzigo’ lakini kesho yake wanakutana nao
na watawaonyesha. Kesho yake walipost kuwa wamekuja lakini wako watatu
na watawafanyizia wote. Niliendelea kusoma zile screenshot huku
nikipatwana kizungu zungu kwani nilijua nini kitaendelea.
Nilishindwa kuendelea nilipoona
picha zetu tukiwa uchi wa mnyama, kila kitendo walichokuwa wakitufanyia
walipiga picha na kuzituma kwenye group, sura zetu zilikuwa zikionekana,
mume alichukua zile picha na kuleft lile group kwani rafiki zake
walikuwa wakichangia mambo ya ajabu bila kujua kuwa waliyekuwa
wakimzungumzia ni mke wa rafiki yao kwani sikuwa nikifahamiana na rafiki
zake wengi hasa waliosoma nao zamani.
Niliishiwa na nguvu kidogo nipoteze
fahamu, nilitamani kulia lakini huwezi kuamini machozi hayakutoka.
Nilimuangalia tu mume wangu bila kusema chochote nikiwa nimeduwaa kama
nimepigwa sindano ya ganzi. “Nilishakusamehe muda mrefu, lakini siwezi
kukugusa kila nikiwaza kuhusu mtoto wetu nachanganyikiwa kabisa”
Aliendelea kuongea kwa sauti yake ya upole. Sikuile sikuweza kusema
chochote, sikuweza hata kuomba msamaha mpaka siku iliyofuata.
Nilimuomba msamaha na yeye
alinikumbusha kuwa alishanisamehe kwasababu anajua kilichotokea. “Najua
kabisa wewe si Malaya, najua unavyonipenda na siku ukinisaliti nitajua
pia, lakini utoto wako ndiyo unakusumbua, nilishakuambia mara nyingi
kuachana na wale watu sasa unaona kilichotokea. Siwezi kuishi na wewe
kama mume na mke kwa sasa, lakini pia siwezi kukuacha uondoke kwani bado
nakupenda hata nikioa mwanamke mwingine itakuwa ni kazi bure bado uko
moyoni mwangu…”
Aliongea huku akibubujikwa na
machozi kama mtoto mdogo, mbele yangu alizifuta zile picha na tangu siku
hiyo maisha yaliendelea huku kila mmoja akilala chumba chake, tulianza
kuishi kama marafiki mule ndani, hakunichunia, kuninyanyasa wala
kunikumbushia makosa yangu, mbele ya jamii tuliendelea kama mke na mume.
Tuliishi hivyo kwa miezi mitano na tulivumiliana mpaka tuliporudiana
tena.
Tulienda kanisani na kubariki ndoa
yetu upya na sasa tunaishi maisha mazuri ya furaha bado nahangaika
kutafuta ujauzito ila naamini Mungu atanipa. Nimeandika kisa changu
kwakuwa nafahamu ingawa Peter kanisamehe lakini ndoa yetu haitakuwa kama
awali tena, tayari imeshaingia doa na mimi binafsi nimeshindwa
kujisamehe kutokana na niliyoyafanya. Ni nadra sana kukutana na mwanaume
kama Peter ni mmoja katika milioni.
Niwasihi tu kwa wanawake wenzangu
kuwa ukishaolewa au ukishafikisha umri flani kuna baadhi ya marafiki
ambao unapaswa kauchana nao. Acha kujipa moyo kuwa mimi sifanyi
wanayofanya, kumbuka ukiongozana na mtu aliyejipaka kinyesi hata kama
umsafi kiasi gani inzi watawazunguka wote tu. Si kwamba uachane na
marafiki wazamani pale unapoolewa lakini kama hawajakua bado wana utoto
achana nao na endelea na maisha yako. Kama nilivyosema hapo awali kuna
Peter wachache sana hapa duniani wakuweza kukusamehe kitu kama hiki.
*****MWISHO*****
No comments:
Post a Comment