Hapo nyuma nilikuwa nikiambiwa kuwa Wazee ni dawa na hazina
hasa katika kutupatia Maarifa sisi Vijana na Wajukuu zao nilikuwa
sitaki kuamini na kuna wakati hata nilikuwa nikimwona tu Mtu Mzee au
Bibi basi nawapuuza tu nikiamini kwamba hawana jipya tena.
Hali hii ilibadilika taratibu baada ya kuanza sasa kupenda
kukaa na Wazee mara kwa mara ili niweze kuchota hekima na busara zao na
kwa kweli tokea nianze kurudisha imani yangu kwa Wazee naona nimefaidika
mno katika kupata Elimu dunia ambayo wengi wetu hatuna na tumebaki tu
kujikita katika Elimu zetu hizi za Kitaaluma tukidhani kuwa pekee ndizo
zitatukomboa Kifikra.
Pamewahi kuwa na nadharia kwamba akina Babu na Bibi wao
huweza kujua Mtoto mchanga aliyezaliwa leo kama ni Mjukuu wao kweli au
labda Mtoto wao amebambikiwa huyo Mtoto na Mama yake kutokana na usaliti
wake ndani ya Mahusiano yao.
Niliamua kufanya mazugumzo yangu ya Kiudadisi kabisa na
Wazee wa Mikoa mbalimbali ili tu niweze kujua kama kuna njia yoyote
mbadala ( ukiachia ile ya kufanya DNA ambayo wengi wetu ndiyo tumeizoea )
ya Kiutamaduni ya kuweza kujua kama Mtoto aliyezaliwa na Mpenzi au Mke
wangu ni wangu au nimebambikiwa.
Ndugu zanguni wana JF majibu niliyoyapata kutoka kwa hao
Wazee wote yalinifanya nizidi kuamini kuwa kumbe tukiwatumia vizuri hawa
Wazee bila kuwadhihaki, kuwadharau na kuwapuuza basi wanaweza kuwa
sehemu yetu kubwa sana ya kupata maarifa na hata kutatua changamoto zetu
zingine za kimaisha ambazo nyingi zimekuja kutokana na mfumo wetu huu
wa Kimaisha ulioratibiwa na utandawazi ambao kimsingi umetuharibu na
unaendelea kutuharibu.
Leo naweka hapa hadharani jinsi ya Wewe Mwanaume mwenzangu
ambaye una Mtoto au hata upo mbioni kumpata Mtoto kuweza kujua kama huyo
Mtoto aliyezaliwa ni wako kweli Kibailojia au umebambikiwa tu. Na
nitangulize samahani kama kuna ambao nitawakwaza juu ya huu ukweli wa
DNA ya Kiutamaduni ila nia yangu ni kuwaokoa tu Wanaume wenzangu juu ya
hii kadhia ambayo imesababisha mitafaruku mingi mno katika Mahusiano na
Ndoa.
HUU NDIYO UKWELI WA DNA YA KIUTAMADUNI
Ewe Mwanaume mwenzangu uliye na Mtoto hapo ulipo awe bado
mdogo au tayari ameshakuwa Mtu mzima chukua mkono wowote uwe wa Kulia au
wa Kushoto wa Mtoto unayeamini kabisa kuwa ni wako kisha kwa umakini
kabisa huku ukiwa umetulia angalia pale katikati ya mkono ( katika palm )
linganisha ile mistari iliyopo na ya Mwanao kisha ukimaliza linganisha
tena mistari iliyopo katika vidole vyake na vya Kwako.
Kwa mujibu wa hawa Mababu na Mabibi ( Wazee ) wanasema kuwa
endapo Wewe Baba ukilinganisha hizo alama nilizokuelekeza hapo juu na
kuona kuwa hazifanani na zako basi automatically jua ya kwamba huyo
Mtoto siyo wako 100% na kwamba Mpenzi wako / Mkeo amekubambikia tu hivyo
cha msingi tu ukishajua huu ukweli piga moyo konde, msamehe na maisha
yaendelee.
Wamesema kwamba hata iweje Mtoto wako wa damu yako kabisa
akizaliwa ni lazima tu alama zilizopo katika Mikono yake zitafanana na
Wewe na wala haziongopi. Na ndipo hawa akina Babu na Bibi wakaenda mbele
na kusema kuwa hiyo mbinu ndiyo iliweza kuwafanya wao huko nyuma wasiwe
wasaliti na wawe wakweli kwani katika Makabila mengi hiyo mbinu
ilishasambazwa na iliendelea kutumika. Na ili kulithibitisha hili ndiyo
maana Bibi yoyote au Babu akipelekewa Mjukuu akimbeba tu kisirisiri
atawahi kuuangalia mkono wa Mjukuu wake na hasa vidole vyake kisha
atajua kuwa Mtoto wao kazalisha au kazalishiwa na wenzake.
MWISHO
Andiko langu hili kamwe halina kusudio la kuharibu
Mahusiano yoyote yale bali naomba tulitumie tu kama sehemu ya kujipatia
maarifa ambayo nina amini wengi wetu ( Vijana na Mabinti ) wa leo
tulikuwa hatuna na kama itatokea umekuta umezalishiwa ( umebambikiwa )
basi ninachokuomba tu samehe, piga moyo konde na songa mbele na ule
msemo wa Wahenga kuwa siku zote Kitanda hakizai haramu.
Kwa Dada zangu Wapendwa najua huu uzi utawaudhi na kuwauma
ila tuvumiliane tu na pengine huu uzi unaweza ukawa msaada mkubwa sana
Kwenu hasa katika kuwafanya mbadilike na muache kuwabambikia Wanaume
zenu Watoto ambao siyo wao kwani hata Takwimu za mara ya mwisho za
Mkemia Mkuu wa Serikali zinasema kuwa 49% ya Wanaume wa Kitanzania
wanalea Watoto wasio wao ( wamebambikiwa ) hivyo mtusamehe na mtuonee
huruma sisi Wanaume.
No comments:
Post a Comment