Kuoana ni ile hali ya kufiti,kuwa kwenye kipimo sawa kuendana na hitaji lako au hitaji la kitu ikiwemo hisia,mitazamo,tabia,nk
Kuna tofauti kubwa kati ya KUOANA na KUFUNGA NDOA.
Watu
wengi hufunga ndoa wakidhani wameoana, kuoana ni hali,kufunga ndoa ni
kitendo,ndio maana huwa kuna siku maalum ya kufungishana ndoa lakini
hakuna siku maalum ya KUOANA.
KUOANA maana yake ni MATCHING,KUENDANA
Ni rahisi
kwa watu wanaooana kufunga ndoa na kudumu kuliko wanaofunga tu ndoa
pasipo kumatch-kuoana.Ni rahisi kufunga ndoa na mtu yeyote lakini ni
vigumu KUOANA NA MTU YEYOTE.
Kuoana ni sawa na neno saresare,kama wewe unavaa kiatu namba 40 na kinakutosha basi ujue mguu wako umeoana na kiatu ulichonunua.
Katika
kuchanganya maana ya KUOANA NA KUFUNGA ndoa wapo waliojikuta wamefunga
ndoa kwa bahati mbaya.Pengine tunaweza kujiuliza,je nitajuaje kama
NAOANA NAYE ILI NIFUNGE NAYE NDOA?AU NIREKEBISHE NDOA YANGU?
Ungana nami katika SEMINA ZA SIRI ZA MAISHA
No comments:
Post a Comment