Unaweza dhania kuwa kutuma ujumbe mfupi kwa mwanamke ili umsisimue
haifai. Lakini kusema kwa hakika, inawezekana kumtumia mwanamke SMS
ambayo inaweza kumsisimua na pia kupata atenshen kutoka kwake. Hii
inaweza kufanya kazi vizuri iwapo umeingiwa na kibaridi cha kuongea na
mwanamke moja kwa moja.
Kabla ujumbe ufupi kuvumbuliwa, wanaume walikuwa wakifuata mbinu
nyingine kuonyesha kuwa wamevutiwa na wanawake waliowapenda. Walikuwa
wakituma barua, kuambia rafiki wa rafiki zao ama kuwafuata na kuwapigia
mbinja majumbani mwao. Lakini kwa bahati nzuri, hivi sasa kuna SMS,
ambazo zina uwezo wa kutuma ujumbe mfupi hapo kwa hapo kwa mwanamke ili
kurahisisha kazi yako ya kutongoza.
Kabla hujaanza kumvutia mwanamke, ni lazima kwanza umfanye akutambue kwa
njia chanya kwanza. Mwanzo haupaswi kutumia SMS kumsisimua mwanamke
mpaka ile siku ambayo utapata kumsoma na kumjua zaidi. Lazima ujipatie
muda ili ujenge connection kati ya nyinyi wawili ili iweze kufanya kazi.
Kufanya hivi kutatoa picha ambayo itajijenga katika akili yake wakati
munatumiana jumbe za kimapenzi. Kama ulimpendeza sana ile mara ya kwanza
alipokupatia namba yake ya simu, basi itakuwa rahisi kwa mpangilio wako
uende sambamba kama vile unavyotarajia.
Pindi utakapoingia katika level nyingine ya kuliwazika na huyu mwanamke
ambaye unamrushia mistari, mwonyeshe vile ambavyo umependezwa na yeye
kwa kumsifu. Hakikisha kuwa unakuwa mpole katika SMS zako pia. Kama yuko
darasani au kazini, usimtumie jumbe mpaka ule wakati ambao yuko huru na
makini wa kujibu texts zako.
Kama hujui ni wakati gani atakuwa yuko free, unaweza kujaribu kumtext
wakati uo huo ambapo amekupatia namba yake ya simu (hakikisha una
makinika kama utaamua kumtumia jumbe wakati uo huo ili usionekane kuwa
una uhitaji mwingi). Vizuri zaidi wakati unapomtumia huo ujumbe unapaswa
umsifie kwa jambo ambalo umeliona wakati ambapo ulikuwa naye awali.
Mfano unaweza kumsifia kitu ambacho ulikiona kama vile nguo nzuri,
tabasamu lake, macho, mawazo yake nk. Jaribu kuhepa kugusia umbo lake
wakati huo.
Kama umekuwa mkitumiana jumbe kwa muda sasa na mumetoka deti mara moja
au mbili, unaweza kuanza kuingiza na kugusia maswala ya mapenzi katika
SMS zenu ili kuanza kupasha misuli kwa mambo ambayo unamwandalia usoni.
Kutokana na mistari ambayo umekuwa ukiisoma kwa mitandao ama kuiskia kwa
marafiki zako, unaweza kuanza kumtext mwanamke huyu mara moja moja huku
ukitulia ukiskilizia kama atakujibu kwa kukubaliana nawe ama kukupinga.
Ukiona kama kila ujumbe anaoujibu anajibu kwa njia chanya, basi ni
wakati wa kwako usichelewe tena bali uhakikishe ya kuwa unatumia mbinu
ambayo utaingiza mawazo yako kwa akili yake na hatokusahau milele –
huwezi jua, labda meseji utakayomtumia baadaye itakuwa ndio meseji ya
kumfanya ajeuke kuwa mpenzi wako.
No comments:
Post a Comment