Hivi
unajua kuwa watu tunatumia muda mwingi kufikiria kuhusu mahusiano?
kwamba unatamani ungekuwa kwenye uhusiano ikiwa huna mwenza, ungekuwa
nje ya uhusiano ulio nao kwa sasa kwa vile huna raha, ungebaki kwenye
uhusiano uliouacha kwa sababu bado unampenda mpenzi wako au kuboresha
uhusiano ulio nao ambao unaelekea kubaya.
Mahusiano
yanachukua/gharimu sehemu kubwa sana ya muda na nguvu zetu, mahusiano
ni muhimu ktk maisha yetu, mafanikio yetu, furaha/raha zenu. Mahusiano
yanagusa kila kona ya maisha yetu kuanzia kazini, nyumbani, familia na
mapenzi.
Uhusiano wenyewe unamaana kuwepo pale kwa
ajili ya mwenzio, kuchangia na kusheherekea undani wa furaha ya ajabu na
ya kipekee mioyoni mwetu (nani anataka kuwa mpweke jamani eeeh?).
Nyumbani
na kwenye familia uhusaino unamaana kufurahia ukuaji wenu, ukaribu
wenu, kupena matumaini, kukosoana, kurekebishana, ushirikiano wenu n.k.
Kazini/Shuleni uhusiano unamaana kusaidiana, kurekebishana, kupena matumaini, kukosoana, kupongezana yanapookea mafanikio n.k.
Kwenye mapenzi uhusiano unamaana kusheherekea “u-mutual”(nipe- nikupe), kupeana mapenzi yasio na kikomo, kushirikiana kila kitu kuanzia mate mpaka miili yetu, kukosoana, saidiana, rekebishana, jifunza n.k.
Kwenye mapenzi uhusiano unamaana kusheherekea “u-mutual”(nipe- nikupe), kupeana mapenzi yasio na kikomo, kushirikiana kila kitu kuanzia mate mpaka miili yetu, kukosoana, saidiana, rekebishana, jifunza n.k.
Kitu kinachonigusa kuhusu mahusiano ni kuwa hatukufundishwa tulipokuwa shuleni japo kuwa tulihitaji sana kujua jinsi ya kuanzisha uhusiano mzuri na wakudumu kwa muda mrefu ktk maisha yetu, yaani kama vile tulivyofundishwa Kiingereza, Hisabati, Historia, Sayansi, Sanaa na Michezo (well wangefundishaje wakati wao wenyewe hawajui).
*Kwenye
somo la lugha ya Kiingereza kuna neno "Elation" ambalo linamaanisha
furaha na ni mzizi wa kile ninachokizungumza hapa ambacho ni uhusiano
(rELATIONship).
*Kwenye somo la
Hisabati tulijifuza “Eros Equation”….unakumbuka? Sasa basi maana
nyingine ya neno Eros ni upendo/mapenzi, na mapenzi ndio kiungo kikubwa
cha mahusiano yetu. Ngoja nikupe mfano wa somo hili ambalo nilikuwa sio
mzuri sana,
Find solution;
Tukio(mapungufu yake)+Unalichukuliaje (unafikiria nini cha kufanya)= Suluhisho (uzoefu wako, mapenzi yako, uoga na furaha yako).
Tukio(mapungufu yake)+Unalichukuliaje (unafikiria nini cha kufanya)= Suluhisho (uzoefu wako, mapenzi yako, uoga na furaha yako).
Hapa
unachotakiwa kufanya ni kutafuta suluhisho kwa kutumia kanuni ya
MAGAZIJUTO…..Ondoa mabano, gawanya, zidisha, jumlisha kisha toa…ili
uweze kufurahia uhusiano wako na kuongeza mapenzi kwa mpenzi wako.
Nitakuja kumalizia swala la uhusiano kwenye somo la Historia, Sayansi, Michezo na Sanaa.....sinauhakika na somo la siasa.
Nakutakiwa mwanzoo mwema wa wiki.
No comments:
Post a Comment