Upo na MPENZI/MWENZA wako kwa sababu gani?
Kuna msemo “All is fair in love and war” –
ni kwa msemo huu ambao unaweza elewa maana yake – maana ingekuwa kila
mmoja ana uwezo wa kusoma akili ya mtu wake kujua yupo nae kwa ajili
ipi, nadhani ingekuwa balaa zaidi ya faida. Na hili ni kwako pia
msomaji… Are you true to yourself? Umewahi jiuliza honestly upo na
mpenzi wako kwa sababu ipi/zipi.
Mapenzi ni mchezo wa ajabu saana.
Wanadamu hutaka awe na wa karibu wake hasa Mpenzi kwa sababu tu kuwa
anapendwa na anapenda pia. Haijalishi mpenzi huyo ni kitu gani
kiliwaunganisha na kuwa wapenzi, iwe ni mapenzi ya dhati juu yake, iwe
kwa ajili ya hitaji Fulani toka kwake, iwe kwa sababu ya muonekano wake –
mwisho wa siku kwa wale waliopo katika mahusiano ya muda mrefu
hujifunza na hatimaye kutambua kuwa mapenzi ni kiungo kimoja wapo tu cha
viuongo vingi vya kuwa katika mahusiano na mtu wako huyo. Kuna viungo
vingine huwepo na pengine kuwa hata na nguvu zaidi kuliko hata kiungo
cha ‘Penzi’ katika mahusiano hayo.
Mapenzi ni muhimu katika mahusiano, ila
bado nafasi yake ni ndogo ukifananisha na viungo vingine. Mahusiano siku
zote suala si kuangalia Mapenzi tu sababu pamoja na kuwa mapenzi ni
muhimu bado yana nafasi ndogo tu katika kujenga mahusiano thabiti
yaliyojaa furaha na amani. Unaweza usiwe umempenda kwa dhati mtu wako
ila ukaridhika na kumkubali bila kujalisha yupo vipi ama ni wa hali
gani; hilo likafanya kuwa na Amani katika mahusiano yenu alimradi na mtu
wako awe hivyo pia. Kuna watu ambao wapo pamoja na hawana mapenzi yale
ya dhati na wana amani na furaha tokana na kuheshimiana, kujaliana na
kuthaminiana, na hali hapo hapo kuna wale ambao wana mapenzi ya dhati na
mapenzi yao yana matatizo mazito ambayo wanashindwa kabisa kuyaweka
sawa kwa wao kuwa na amani katika penzi lao hilo.
Kwa muktadha huo, haiepukiki kuwa na
sababu mbali mbali ambazo huwafanya watu kuwa na watu waliowachagua kuwa
nao katika mahusiano. Mapenzi ikiwa moja ya sababu ya baadhi kuwa
katika mahusiano, bado kuna sababu nyingine nyingi ambazo huwa ni sababu
za msingi kwa baadhi kuwa na wapenzi wao. Hivyo sababu za kila mmoja
kuwa katika mahusiano zimetofautiana from couple to couple na mara
nyingi hata mtu na mpenzi wake pia.
Baada ya kusoma hapa, ni vema ukajiuliza
ndani ya nafsi yako upo na mpenzi wako kwa ajili ipi, ukipata jibu na
kusoma haya yanayofuata utakuta linaweza kuwa limegusiwa hapa, or ikawa
pia kuna sababu zingine zaidi ya nilizo ainisha hapa, ukasaidia kutoa
mawazo ya kipi kinaongezeka katika sababu hizi hapa.
UTEGEMEZI
Hii ni kwa wale ambao mara nyingi hana
uwezo wa kujitegemea. Na kama ana uwezo wa kuitegemea ni kwa maisha ya
kiwango ambacho ni cha chini na asingependa maisha hayo. Hivyo ina maana
unakuwa upo na mpenzi wako sababu yeye ndie anayekuweka mjini, unajuwa
kuwa bila yeye maisha yako yatakuwa hayana muelekeo au hata kutokuwa na
guaranteed secure future. Saa ingine hata humpendi, ila humchukii na
kichwani zipo za kukutosha kutambua kuwa bila yeye huna lolote, mbele wa
nyuma. Utegemezi huu upo wa aina mbili;
Utegemezi wa Kiakili (kutokujiamini) –
Mtu huyu anakuwa na low self-esteem anahitaji kila mara kuambiwa na
kusifa na mtu wake ili yeye kuweza kujiona wa maana.
Utegemezi wa kusaidiwa (kutokujiweza) – Haya maelezo yanajitosheleza mwanzo wa kipengele hiki.
VIHAMASISHI
Hii inatawaliwa zaidi na mazingira –
mazingira yanakuwa ndiyo chanzo cha kuwa pamoja. Mfano kufanya kazi
pamoja mara nyingi na saa ingine kujikuta katika mazingira ya
kuhamasisha sex. Kwa wengine inaweza kuwa kosa la mara moja na wasirudie
tena na hali kwa wengine ikawa mwanzo wa mahusiano. Inaweza tokea pia
kwa wale ambao ni marafiki wa karibu ambao kila mmoja hufurahia uwepo wa
mwenzie tokana na kuwa na mengi ambayo wanagongana kimtazamo, mawazo,
misimamo n.k na kisha kujikuta mwisho wa siku mpo katika mahusiano.
Kunaweza kuwa na mifano mingi zaidi ya hii kwa misingi kuwa mazingira
hamasishi kwa mahusiano ama ngono ni mengi sana.
INSECURITY
Hujiamini… hujitambui… na wala hujijui
bado. Na kama wajua basi huamini utambuzi wako. Unaona kana kwamba huyo
mpenzi wako ni your lucky charm, hata kama unafanya kazi na una
maendeleo hasa kama uliyapata ukiwa naye unaona kama vile bila yeye
haitawezekana kuendelea. Unaona kama vile huwezi mpata mpenzi mwengine
aliye bora kama huyo… aidha kimuonekano, ki maisha, ki maslahi,
kimaendeleo n.k. Unaona kama vile kuwa nae ni bahati sana lasivyo
utampata beneath huyo mtu.
UFAHARI
Hii mara nyingi hutegemea nafasi, jina,
wasifu kwa mpenzi wako. Kama vile kuwa na jina kubwa… kazi nzuri… Maisha
mazuri… anaheshimika katika jamii… anakubalika na wengi, anatamaniwa na
wengi, ana mvuto na mengine kede kede. Mhusika anakuwa si kwamba
kampenda mtu wake, ila tu anakuwa kapenda zaidi kuwa jamii itaona yupo
nae na kwamba yeye ndiye mwenye bahati ya kuwa nae kama mpenzi wake.
Wahusika wa kundi hii huwa katika mahusiano haya kwa sababu ya
‘Ubinafi’. Mfano anaweza akatoka na mtu maarufu ili kupata umaarufu pia
wa haraka, anaweza toka na mtu ambae watu huona ni
mzuri/mrembo/mtanashati ili tu aonekane kana kwamba yeye ni bora kuliko
wote hapo kwa kumpata huyo mtu. Anajua kabisa humpendi ila anakufaa kuwa
mpenzi wako katika macho ya jamii.
KUKATA TAMAA
Hili ni sana kwa wale walio hangaika sana
katika ulimwengu wa mapenz. Kila ampatae tokana ma viwango vya aina ya
watu ambao anavutiwa nao (saa ingine bila hata viwango hivyo) mwisho wa
siku anaumizwa. Kila mpenzi ambae kawahi mpata amemtenda na kumuumiza
moyo, mwisho wa siku anapata mtu ambae walau ana mwelekeo na ingawa ana
madhaifu ila ni ya kibinadamu hivyo huona ni kheri aridhie na kutulia
kwa huyo mtu kuliko kuendelea kutendwa tena. Anakuta toka awe na huyo
mtu kapata uhafueni sana, hivyo inatokea anaridhika hivyo hivyo hata
kama si ambae angependa kuwa nae.
GUNDI ASILIA YA NDOA
Hii ipo sana kwa wale ambao ni wanandoa;
yaani mtu na mwenza wake.. wamejijenga pamoja. Wana watoto, rasilimali
na maisha yao yapo so tangled pamoja tayari. Lile wazo ama kitendo cha
kutengana ni kuyavuruga kabisa maisha kwa kiasi kikubwa sana. Mara
nyingi watoto na mali ndiyo force kubwa. Wanandoa wote wanaweza tambua
kuwa hawapendani kabisa wapo radhi hata wahame vyumba kila mmoja awe na
chake (hata kama kitanda) lakini mwisho wa siku wanaheshimiana, mbele ya
jamii wanajulikana kama mtu na mkewe huku ndani haviivi kabisa.
KULAZIMISHWA
Aidha ulilazimishwa kuwa nae… au unaweza
kuta ni wa kurithi. Kuna kabila na mila ambazo hadi leo inatakiwa
utafutiwe mtu wa kuoana nae… labda katika ukoo ama kwa wakaribu wa
familia. For instance dada kaolewa kazaa watoto wawili then anafariki na
soln inaonekana ni bora aolewe mdogo wa marehemu. OR kaka anafariki
then kaka ama mdog wa marehemu anaoa mke wa marehemu kwa njia na nia ya
kurithi.
COMPATIBILITY
Hampendani, ila heshima kwa saana. Wote
mmeweza na kufaulu katika ku compromise. Yale ambayo mwenzio hapendi
umeweza epusha na wala hujaona tofauti yoyote with the justification
kuwa sio ya msingi sana kuendelea na vivo hivo kwa mwenzio. Mmekutana
tabia, maybe wote ni wacheshi/wapole, wote hupenda privacy yake mwenyewe
na huheshimu ya mwenzie… vitu kama kufuatiliana, kuchunguzana,
kushikiana simu, kupelelezana au kuchokonoana hakupo. Watu hawa mmoja
wapo anaposafiri akakaa huko hata kwa kipindi kirefu mawazo kama
kusalitiana hata hayawatembelei kichwani kwao (hata kama kweli
wanafanya); hawa complicate maisha, kama hawapo pamoja simu mara moja or
mbili kwa siku… more out of obligation than love. Hawa mmoja wao hata
awe na mpenzi mwengine anajua kabisa hawezi kuwa as perfect as huyo
alokuwa committed kwake.
MAPENZI YA DHATI
Hapa ni kwa wale wenye mapenzi ya kweli,
wale ambao kama mioyo yao ni dhaifu huweza kujiua na kuua kabisa katka
jina la ‘Penzi’. Anaona bila huyo mtu wake hakuna mwingine hapa duniani
hata umwambie nini, hata umshawishi nini na hata utumie jitihada gani!
Hapa ndipo pale msemo wa “Hakunaga’ unajitosheleza kabisa.
Ni kwa misingi hiyo kupenda kwa dhati
kunaweza fanana toka mmoja na mwingie ila mwisho wa siku kila utakae
mwambia akueleze nini maana ya mapenzi kila mmoja atakupa jibu lake.
Maelezo tofauti kabisa ila mwisho wa siku yote yakibeba uzito wa jinsi
gani mtu fulani katika maisha yake humfanya ajisikie raha, ajisikie
tofauti, ajisikie wa pekee, ajisikie vyovyote vile katika muelekeo war
aha zote zilizopo hapa duniani…
Ubaya tu wa haya mahusiano, ni rahisi
sana kutodumu, ingawa kuna wale wenye bahati huwa yanadumu, na kuna wale
wenye bahati tokana na ubinadamu, mtabadilika, mapenzi yatapungua ila
mwisho wa siku yatarudi katika mstari.
Mwisho napenda niongezee sababu kawaida
si moja, sababu inaweza kuwa zaidi ya moja – ingawa sababu moja hubeba
uzito kuliko sababu zingine ambazo zipo. Lakini vyovyote iwavyo,
pendaneni, thaminianeni, heshimianeni na jengeni mahusiano kujenga Amani
na furaha kati yenu…
Usikose kukutana namimi katka makala ijayo….
No comments:
Post a Comment