Habari
za wiki hii mpenzi msomaji. Mimi namshukuru Mungu kwa kuweza
kunikutanisha na nyinyi kupitia safu hii ambayo pamoja na mambo mengine
nazungumzia juu ya mada mbalimbali ambazo zinagusa maisha yetu ya kila
siku.
Wanaume
wengi wanapofikia hatua ya kuoa si kwamba wanakurupuka tu na kuoa
mwanamke yeyote mwenye sura nzuri, bali huchukua muda wao mwingi
kuchunguza mambo mengi juu ya wake ambao wanadhani kwamba wanaweza kuwa
pamoja kwa kipindi chote cha maisha.
Wanawake
wengi wanajisahau na kudhani kwamba kitu kinachoweza kuwafanya
wakapata wachumba ni uzuri hivyo kupoteza muda wao kujichubua na
kujiremba ili wawavutie wanaume bila kujua kwamba kuolewa ni zaidi ya
uzuri.
Hali
sasa hivi imebadilika ni tofauti na kipindi cha nyuma ambapo ukiwa na
sura nzuri na umbo la kuvutia basi una asilimia 100 za kuolewa.
Utafiti
ambao nimeufanya unaonesha kwamba zaidi ya uzuri wa tabia na umbo,
kuna kuna sifa nyingine za msingi ambazo mwanamke anatakiwa kuwa nazo
ili aweze kuwa katika mazingira mazuri ya kupata mchumba wa kumuoa
kiasi kwamba asipokuwa nazo ataishia kuchezewa tu lakini haitatokea mtu
kumtakiwa kwamba anataka kumuoa.
MWEYE MAPENZI YA KWELI
Lengo
kubwa la mwanaume kuoa ni kutaka kupata mapenzi ya kweli kutoka kwa
mwanamke na ikiwezekana waweze kupata watotoa ambapo watoto mara ndio
wamekuwa furaha ya ndoa. Wapo wanawake wengine ambao wanonesha wazi
kutokuwa na mapenzi ya kweli bali wanakuwa na mapenzi ya kuzuga.
Wanachotaka wao aidha kupata umaarufu tu kwamba yuko na mtu fulani ama
kuweza kupata pesa alizonazo mwanaume lakini sio kwamba ana mapenzi ya
dhati kutoka moyoni mwake.
Mwanamke
asiye na mapenzi ya dhati utamgundua tu, muda mwingi utamuona macho
yake yako kwenye mfuko wa mwanaume. Akiona kwamba mfuko umetuna utaona
anaonesha mapenzi ya hali ya juu lakini pindi hali inapokuwa kubwa mbaya
kifedha mapenzi yanaanza kufifia.
Kwanini
wanaume wanapenda wana wake wenye mapenzi ya dhati kutoka mioyoni mwao
na si kutokana na fedha walizonazo? Hii inatokana na ukweli kwamba
maisha siku zote yanabadilika, kama waswahili wanavyosema, kuna kupanda
na kushuka.
Sio
kwamba kila siku utakuwa na maisha mazuri na kama itatokea hivyo basi
ushukuru mungu.Hivyo basi mwanamke wa kuoa lazima afahamu hivyo na awe
tayari kuonesha mapenzi yake ya dhati wakati wote wa maisha yao na si
kwa kipindi fulani tu cha neema.
Si
hivyo tu pia asilimia kubwa ya maisha ya ndoa yanatawaliwa na
mapenzi, kwa hiyo nyanja hiyo inakuwa ya msingi sana kwa wanaume wengi
kuiangalia ili wasije wakajikuta wanaoa mwanamke ambaye baada ya muda
mapenzi yanakwenda likizo hali ambayo inaweza kuwafanya wasiishi maisha
ya raha mustarehe.
WENYE TABIA NZURI
Tabia
njema ndio silaha ya maisha, ukiwa na tabia nzuri kila mtu atakupenda,
hiyo ni katika maisha ya kawaida. Lakini linapokuja suala na kuoa
tabia inakuwa kitu cha awali sana kungaliwa na hiyo inaweza kuwa na
ukweli kwa sababu wapo wasichana wazuri wenye mvuto wa aina yake na
maumbile mazuri, lakini wanakosa wanaume wa kuwaoa, ukiuliza kwani
utaambiwa anatabia mbaya.
Naweza
kusema hilo ndilo limekuwa tatizo kubwa kwa baadhi ya wanawake kukosa
wanaume wa kuwaona. Hakuna mwanaume hata mmoja kati ya wale ambao
nimejaribu kuongea naye ambaye ameonesha kulidharau suala hilo la tabia.
Si
hivyo tu wapo wanaume ambao wameingia kichwa kichwa na kuoa kwa
kuangalia sura tu bila kujali tabia, matokeo yake baada ya siku chache
yanatokea machafuko ya aina yake hali ambayo imepelekea kuvunjika kwa
ndoa kutokana na tabia mbaya alizonazo mwanamke.
WENYE UCHU NA MAENDELEO
Hivi
karibuni kumekuwepo na mabadiliko ya aina yake kwa wanaume, wengi sasa
hivi hawapendi kabisa kuoa mwanamke ambaye hana kazi yaani 'golikipa'.
Kama atakuwa hana kazi basi awe na uchu wa maendeleo kwa kujituma
kufanya kazi mbalimbali za kimaendeleo kama vile kilimo kwa wale walio
vijijini na biashara ndogondogo kwa wale ambao wako mijijini na hata
vijijini.
Ile
dhana ya kusema mwanamke ni mama wa nyumbani wa kukaa na kujipodoa
akimsubiria mwnaume arudi amstarehesha, sasa hivi imepitwa na wakati.
Wanaume wengi wanapenda wanawake ambao ni wahangaikaji, wenye ndoto za
maendeleo katika maisha yao. Hata kama watakuwa si wafanyakazi lakini
wawe wenye kutoa ushauri kwa waume zao juu ya jinsi gani wafanye ili
wafanikiwe.
WASIOPENDA MAKUU
Kuna
wanawake wengine wanakuwa na tabia za ajabu sana kiasi kwamba yaweza
kuwa kero kwa wanaume. Wapo wanawake ambao wanapenda makuu bila kujali
hali halisi ilivyo. Kuna wanawake naweza kusema wana tamaa, kila
wikiendi utamsikia "leo tunakwenda wapi dear?"
Akimuona
rafiki yake kanunua simu ya laki tatu na yeye utamsikia akisema, ‘na
mimi naomba uninunulie simu kama ya Grace’. Ukienda naye Pub
anakuambia, "mimi sinywi pombe za chupa natumia za kopo tena Heineken’.
Yeye hajali kiasi cha pesa mwanaume alicho nacho na usipotekelezea
anachukia na anaweza hata kupunguza mapenzi.
Wanawake
kama hawa wako katika mazingira magumu sana ya kuweza kupata wanaume
wa kuwaoa. Mara nyingi katika maisha fedha huzungumza, kama mwanaume
atakuwa na pesa ya kutosha itakuwa rahisi sana kwa mwanamke kupata kila
atakachopenda lakini si kwa kumwambia mimi nataka kitu fulani.Mwanaune
mwenyewe utamsikia akisema, ‘unataka nikununulie simu ya aina gani, au
leo unataka twende wapi?’ hapo ndipo utakuwa na nafasi ya kusema, ‘mimi
nataka uninunulie simu kama ya fulani ama leo nataka twende sehemu
fulani.’
Wanaume
ni warahisi sana wa kuwapatia wale ambao wanatarajia kuwaoa chochote
ambacho watahitaji kama tu pesa haitakuwa tatizo. Kitu ambacho
kinawaudhi wanaume wengi ni ile tabia ya mwanamke kupenda mambo makubwa
bila kuangalia uwezo uliopo kwa mwanume.
Kuna
wanawake wengine wao si wasemaji kabisa, yeye anasubiri leo amemletea
hiki, anapokea na kushukuru, kesho akiambiwa twende beach anakubali. Au
wengine wanasubiri mpaka waulizwe wanataka nini, ndio wanasema.
Sisemi
kwamba uwe mkimya tu hata kama una shida ya kitu fulani na unafahamu
kwamba ukimweleza mwenza wako anaweza kukusaidia, hapana! kama unaona
kwamba uwezekano wa kupata kile ambacho unakihitaji upo mweleze kwa
utaratibu naamini atakuelewa na kukutimizia.Tabia ambayo hawaipendi
wanaume wengi ni ile ya kulazimisha ufanyiwe kitu fulani wakati
inawezekana uwezekano haupo.
WAVUMILIVU
Wapo
wanawake ambao sio wavumilivu kabisa katika maisha.Tunajua kwamba
maisha siku zote hayatabiriki, yanaweza kutokea matatizo ya kiafya ama
kifedha.Huu ndio wakati wa kuona uvumilivu wa mtu.Kama mwanamke
anatarajia kwamba siku zote ni za raha tu na pindi matatizo yanapotokea
anachukua uamuzi wa kumtoroka mwanume, huyo siyo mwanamke wa kuoa.
Wangapi
leo hii huwatoroka waume zao pindi inapotea kuumwa, kufilisika ama
kupatwa na tatizo lolote ambalo kwa namna moja ama nyingine yanaweza
kuwafanya maisha yao kutingishika?
Uvumilivu
kwa mwanamke utakuwepo kama tu atakuwa na mapenzi ya dhati kama
nilivyozungumza hapo awali. Mwanamke mweye mapenzi ya dhati ni lazima
atakuwa mvumilivu na atakuwa tayari kuishi katika maisha ya aina yoyote,
yawe ya raha ama ya starehe.Hawa ndio wale ambao wanaume wengi
wengependa kuwa nao maishani mwao.
Licha
ya kupenda kuoa wanawake amabo wana tabia hizo nilizozitaja hapo juu,
wanachukizwa sana na wanawake ambao wanavijitabia vidogo vidogo ambavyo
kimsingi havikubaliki katka jamii.
Tabia
hizo ni kama wambea, wasio wakweli na wawazi, wasioridhika, wagumu
kusamehe na wapesi wa kuchukia, wagomvi na wenye roho ya kwanini.
Utafiti huu umefanyikwa kwa baadhi ya wanaume ambao wanatarajia kuoa
wanawake ambao wanaoishi katika maeneo mbalimbali jijini Dar-es-Salaam.
Kwa maana hiyo basi hiyo iwe changamoto kwa wanawake. Wajue kwamba wanaume wanafurahi kuwa na wanawake wa aina gani. Hata kama utakuwa umeshaolewa, kama kuna wakati kunakuwa na kutokuelewana baina yenu, chunguza yawezekana kwamba unakosa mojawapo ya tabia ambazo nimezitaja hapo juu. Waweza kubadilika kwani inawezekana.
Kwa maana hiyo basi hiyo iwe changamoto kwa wanawake. Wajue kwamba wanaume wanafurahi kuwa na wanawake wa aina gani. Hata kama utakuwa umeshaolewa, kama kuna wakati kunakuwa na kutokuelewana baina yenu, chunguza yawezekana kwamba unakosa mojawapo ya tabia ambazo nimezitaja hapo juu. Waweza kubadilika kwani inawezekana.
No comments:
Post a Comment