Katika
kipindi cha urafiki au uchumba ukisikia mwanaume anasema “huyu mwanamke
hana future” kwake anamaanisha huyu mwanamke sio wakumtegemea kwenye
masuala ya kimaendeleo huko mbeleni tukianza maisha, kiu ya mwanaume
huyu ni kuona mwanamke anaye mchumbia anauwezo wa kujitegemea na
kujisimamia, sio kuwa mke tegemezi, hapa “future” kwa mwanaume
inamaanisha uimara wa maisha ya baadae. Kwa upande wa pili ukisikia
mwanamke anasema “huyu kaka hana future” anamaanisha huyu kaka sio
muoaji, hofu ya dada huyu ni kujikuta anatumia muda mwingi kuendelea
kwenye mahusiano halafu mbeleni huyu kaka akasepa, au asiwe na mawazo ya
kuoa na kuwa na familia. Hapa neno “future” kwa mwanamke linamaanisha
kuwepo au kutokuwepo kwa utayari wa kuanza maisha ya pamoja “kuoana”.
Hali hii au mtazamo huu uko vile vile hata pale mzazi wa kiume “baba”
anapomuuliza kijana wake kuwa “huyo mchumba wako ana future?” au mzazi
wa kike “mama” anapomuuliza binti yake “huyo kijana ana future?” –
Chris Mauki.
Thursday, May 18, 2017
UTOFAUTI WA MTAZAMO BAINA YA MWANAUME NA MWANAMKE KWENYE MAHUSIANO
About Unknown
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment