Kuna mdada mmoja nilisoma naye chuo miaka fulani hapo nyuma, sasa jana
katika pilikapilika zangu mjini, tukakutana ghafla maeneo fulani, kwa
hiyo tukaanza kusalimiana na tukaona ni vizuri tusogee pembeni kwenye
mgahawa fulani tukakaa. Basi tukawa tunapiga story za
kawaida na kila mmoja akimwuuliza mwenzio yuko wapi na anafanya nini
sasa. Katika kukaa naye kwa muda mfupi usiozidi nusu saa, kila baada ya
sekunde kama 3 hadi tano nasikia simu yake (Sumsung galaxy S5) ikilia
ndii, njee, ngaa, etc., huku akiishikilia na kucheza nayo muda wote!
Sasa ikabidi nimwuulize mbona simu yako haiishi milio? Akajibu ni msgs -
watu wananitumia msgs kutoka social networks mbalimbali.
Nikamwambia mmmhh, social networks gani hizo mpaka simu iwe busy muda
wote? Akaniambia mie nipo (tena kwa madaha) karibu social networks zote
halafu nina marafiki wengi sana, akaanza kunionyesha (sio kwamba
sizijui, ila yeye alihisi mie ni mngoroko na sijui chochote kuhusu
social networks), nami nikawa curious kufuatilia, maweeeeeeeeee! Mdada
karibu kila social network unayoijua yupo na ni very active, halafu
amejiunga na magroup kibao, singles, lovers without limit, love addicts,
sijui magroup gani yaani basi:
No comments:
Post a Comment