Si utundu na ujanja wa mwanaume tu
unaomwezesha mwanamke kupata utamu wa kufika kileleni (mshindo, orgasm,
coming) bali mwanamke pia anahusika.Kufika kileleni ni nini?
Ni kiwango cha juu kabisa cha utamu, hisia, raha, msisimko wakati wa tendo la ndoa wakati ambapo misuli ya uke au uume hukaza.
Kwa mwanaume huambatana na kutoa manii (ejaculation).
Wengine wakifika kileleni hupiga kelele
sana, wengine huongea maneno ovyo ovyo hata matusi, wengine huzimia
kabisa, wengine huwakwida wapenzi wao kama vile kibaka, wengine hutulia
kimya na kupitilia za usingizi na wengine ukiwauliza wanasema mahali
walikuwa ni kama vile walikuwa hewani, wengine kama vile walikuwa
wananamwona Bwana (Yesu) n.k ilimradi tu ni raha na utamu na ni kweli
Mungu alitupa zawadi ya ajabu na hii ni kujulisha kwamba Mungu alituumba
tena kwa namna ya ajabu.
Pia wengine huita kufikia mshindo, wengine huita coming n.k
Pia wapo ambao kwa tendo moja la ndoa huweza kufika kileleni zaidi ya mara moja.
Je mwanaume na mwanamke wote hufika
kileleni sawa?Kwa wanaume kufika kileleni ni suala ambalo ni automatic,
halina mjadala, kitu cha msingi kwake ni kujitahidi asifike mapema
kileleni ili amfikishe mke wake pale anatakiwa kufikishwa, kwani mara
nyingi mwanaume akifika kileleni hupoteza uwezo wa kuendelea na tendo.
Katika nchi zilizoendelea kama USA na Canada utafiti mwingi unaonesha kwamba
Asilimia 15 % ya wanawake hufika kileleni mara zote.
Asilimia 48 % ya wanawake mara nyingi hufika kileleni.
Asilimia 19 % ya wanawake ni kawaida kufika kileleni lakini si mara nyingi
Asilimia 11 % ya wanawake ni nadra sana kufika kileleni na
Asilimia 7% ya wanawake hawajawahi kufika kileleni na hawajui ni kitu gani.
Hapa ni wanawake kutoka nchi zilizoendelea ambako elimu kuhusu mapenzi ni kubwa sana.
je, kwetu nchi zilizogoma kuendelea hali itakuwaje?
Ukizingatia wanaume wengi bado hawajajua nini wanawake wanahitaji ili kufikishwa kileleni?
Pia kuna baadhi ya wanawake ambao hata wasipofika kileleni hawana shida wanaridhika tu bora maisha yanaenda.
Nini Kitu muhimu kuhsu mwanamke kufika
kileleni?Wanawake wanaweza kuendelea kupata utamu hata baada ya kufika
kileleni hivyo ni jukumu la mwanaume kuhakikisha anabaki ndani ya uke
hadi anahitimisha tendo zima (conclusion) angalau kwa dakika 10 au 15
ndo ukimbie kuoga au kupiga usingizi siyo kumwacha kiumbe wa watu kwenye
mataa akuugulia kwsa kumuondolea utamu na raha.
Tendo la ndoa huwa ni la kuridhisha sana
hasa pale mume anapomfahamu vizuri mwanamke na kile anahitaji kwa
kumfanyia utundu wote wa kuchokonoa sehemu zote ambazo zinaweza
kumhakikishia kwamba atafika kileleni.
Lakini pia mwanamke anasehemu kubwa sana ya yeye kujihakikishia anafika kileleni si mwanaume tu ni suala la wote.
Je maadui wakubwa wa mwanamke kufika kileleni ni nini?Kukeketwa (Female Genital Mutilation).
Kukeketwa ni kitendo cha kukata sehemu ya uke hasa kisimi kwa wanawake.
Katika Afrika kuna nchi 28 ambazo hufanya hicho kitendo cha kikatili, na pia nchi kama Yemen na Indonesia bado wanafanya.
Ingawa wanawake waliokeketwa huweza
kurudia hali ya kuweza kufika kileleni, walio wengi huathiriwa sana na
hiki kitendo na kuwasababishia kushindwa kufika kieleleni.
Dini, jadi na utamaduni:
Kuna baadhi ya mitazamo na malezi ya
dini, jadi au tamaduni huwapa wanawake mtazamo mbaya, finyu na usio na
maana kuhusiana na tendo la ndoa.
Katika dini, jadi, na tamaduni nyingi
ukiacha jando na unyago, elimu ya mwanamke kuhusu mwili na uzazi
havifundishwa wala kutamkwa matokeo yake wanawake wengi hawaijui miili
yao, kiasi ambacho unakuta kijana wa kiume anamuoa binti hajui chochote
kuhusu mwili wa huyo mwanamke na mwanamke mwenyewe hajui chochote kuhusu
mwili wake mwenyewe, akiguswa chuchu anakataa kwani ni kwa ajili ya
mtoto, hapo utategemea afikishwa kileleni kweli?
Kisaikolojia.
Hili huchangia kwa asilimia 95 kwa matatizo yote yanayosababisha mwanamke asifike kileleni.
Adui mkubwa anayetisha sana wa mwanamke kutofika kileleni ni akili (mind.)Hofu labda ya kuachwa,
mashaka, kutojiamini, kukasirika,
donge moyoni, kisirani au
mahusiano kutokuwa mazuri huweza kusababisha mwanamke kutofika kileleni.
Kushindwa ku- concentrate kwenye tendo lenyewe na kupata hisia halisi (sensations).
Kuwa na mawazo ya kitu kingine wakati wa tendo la ndoa
Mawazo hasi (Negative) kuhusu tendo la ndoa, pia Kuwa mchomvu.
Kibailojia
Kama vile kuwa na mfumo ovyo wa mzunguko wa damu kwenye maeneo ya viungo vya uzazi pia huchangia.
Anaweza kuwa na uvimbe au kisukari pia huchangia.
pia hitilafu za viungo baada ya kufanyiwa upasuaji hasa sehemu ya uke.
Umri (Menopause)
Kuna wakati mwanamke kuanzia miaka 48 –
52 hupata mabadiliko ya upungufu wa homoni na huo upungufu husababisha
sehemu ya uke kuwa kavu wakati wa tendo la ndoa.
Kuwa na uke mkavu huchangia katika ufanisi wa tendo la ndoa kuwa mdogo na hatimaye kushiondwa kufika kileleni
Si kweli kwamba mwanamke akizeeka uwezo
wa tendo la ndoa unakuwa mdogo, muhimu ni kutumia vilainisho kama gel au
KY jelly na libeneke linaendelea kama kawaida.
Kutumia madawa (Medicaments).
kama unatumia dawa za kuzuia msongo wa
mawazo pia huchangia ile hamu ya tendo la ndoa (libido) na matokeo yake
kukosa kufika kileleni.
Pia kuna dawa za uzazi wa mpango hupunguza hamu ya tendo la ndoa hasa zile ambazo huingizwa mwilini (sindano)
Pia dawa za kupunguza pressure hupunguza uwezekano wa kufika kileleni.
Pombe, madawa ya kulevya na sigaraAlkoholi na madawa ya kulevya hupunguza sana hamu ya tendo la ndoa.
Huathiri mfumo wa Fahamu unaohusika na mzunguko wa hisia za mapenzi kati ya ubongo na uke.
Kama inavyoathiri (alkoholi) mwanaume kudindisha vilevile huathiri mwanamke kufika kileleni.
Mwonekano, urembo na umaridadi:Kwa
mwanamke jinsi anavyoonekana na jinsi mwanaume anavyoonekana kuna sehemu
katika hisia za mapenzi (emotions na feelings).
Kama yeye mwenyewe anajijua kwamba
hayupo vizuri kimwonekano (urembo, usafi, harufu) na pia kama mwanaume
hayupo sawasawa basi anakuwa ameathirika sana kiasi ambacho hawezi
kufika kileleni.
Pia wanawake wana uwezo mkubwa kunusa
harufu kuliko mwanaume hivyo harufu yoyote mbaya kwake huwezi kumpeleka
nje kabisa ya njia ya kwenda kileleni.
MazingiraKama eneo au chumba mlichopo
hakina usalama kama vile anahisi mtu anachungulia au anaweza kuingia,
kwa mwanamke hiyo ni issue kwani hawezi kufika kileleni kwa sababu ya
usalama wake.
Je kuna jinsi ya kuondoa tatizo la
kutofika kileleni?Kujiruhusu mwenyewe kupenda tendo la ndoa na zaidi
kupenda kufika kileleni kwa hamu kubwa.
Kuwa responsible kwa mambo yote yanayohusu ufanisi wa tendo la ndoa.
Kujipa elimu na maarifa kuhusu elimu ya
mapenzi kwa mwanaume na mwanamke, viungo vinavyohusika na kila kitu
kinachiweza kukupa tofauti katika ufanisi uimarishaji wa tendo la ndoa
kama unavyosoma hapa sasa hivi.
Kuwa na mawasiliano wakati wa tendo la ndoa hasa kuhusiana na maeneo yote ambayo unasisimka pale ukiguswa au kuchezewa.
Kufanyia kazi kila tatizo lolote la kisaikolojia na kupata solution kabla ya tendo la ndoa.
No comments:
Post a Comment