Mwanamke aliyeolewa ni msaidizi wa mume
wake, kuhakikisha amempikia mumewe,amemfulia, na mumewe akitoka kazini
akili zake zote ziwe kwake, amuhudumie kwa kila kitu akisimama katika
nafasi yake kama mwanamke aliyeolewa. Pia mwanamke
aliyeolewa ni nguzo ya familia yampasa kuwa mtu anayemwomba Mungu kwa
Imani yake kila wakati na pia kuwalea watoto vizuri na kuhakikisha
usalama wao,
Siku hizi smartphone zinatuponzaa
wanawake, kila saa tuko mitandaoni, mara kutafuta umbea, mara kuupload
picha zisizo na mantiki et umepita kwa mangi umenunua kachips umepiga
picha chaap umepost, mara kuandika status za vijembe watsapp, mara
kutukana kwenye mitandao,
mwanamke umeolewa una account 20
insta,magroup yasiyo na maana ndo usiseme, mume karudi kazini wewe huna
habari umetundika miguu uko busy na simu housegirl ndo amuhudumie mumeo
chakula, we unafanya kuagiza tu nipe hichi mnawishe baba mikono kweli
jamani?, smtms hadi unapika chakula kinaungua kisa ukobusy na simu.
Mara umepigiwa simu na mwanaume gani
sijui anaongea upuuzi wewe ni kuchekacheka tu .Shost anakupigia simu
nusu saa mnaongea tu upuuzi,hadi mwanaume anaboreka akikusubiria umalize
kuongea aseme nawe jambo.
watoto wala huna habari nao hujui kwamba
wamekula,hujui yupi ana homa, ni housegirl ndo anakuja kukuambia mama,
Debora joto lake leo liko juu.mama mtu hujui kama joto la mtoto liko juu
ila unajua picha ya mwisho leo wema sepetu kaweka insta kweli????
Halafu unajiita umeolewa wakati hujui majukumu yako kama mke??.
Aisee Wanawake mlioolewa badilikeni,
simaanishi kwamba msitumie smartphone ila muwe na kiasi, hii ya mke wa
mtu kiiila saa uko mitandaoni pasipo na sababu ya msingi
acheni,waachieni single Girls.
No comments:
Post a Comment