Tathmini ya utafiti kutoka chuo kikuu cha Exeter nchini
Uingereza, inaonyesha kuwa kiwango cha mbegu za uzazi za wanaume
huathiriwa kwa kuweka simu za mkononi kwenye mifuko ya suruali.Hata
hivyo ,mwanasayansi wa maswala ya uzazi na shahawa,anasema kuwa ushahidi
huo bado hauna uhakika wowote hivyo basi simu yake bado inaendelea
kukaa mfukoni mwake.Uchunguzi huo uliochapishwa katika jarida la
'Environment International' ulilaumu mnunurisho wa kielectromagnetiki
kuwa chanzo kikuu kinachoathiri mbegu za wanaume.Wataalamu walichanganua
utafiti tofauti kuonyesha uborawa shahawa wakihusisha wanaume 1,492.Hii
ilijumuisha kupimwa kwa shahawa zilizowekwa wazi kwa mnunurisho wa simu
za rununu, kwa maabara na udadisi wa wanaume katika kliniki za
uzazi.Kiongozi wa uchunguzi huo Dkt.Fiona Mathews aliambia BBC kuwa
kutokana na uchunguzi huo,mmoja tu ndio ulionyesha uhusiano kati ya
utumizi wa simu na kudidimiakwa ubora wa shahawa."Nafikiri kwa mwanamume
wa makamu hakuna haja ya kuingiwa na hofu,iwapo unajua una uwezekano wa
kuwa na shida ya kizazi basi itakuwa jambo la busara kutoweka simu
mfukoni ,pia kugeuza mtindo wako wa kula."Mbegu za uzazi za wanaume
zinasemekana kuathirika kutokana na simu za mkononiAlikubali kukosolewa
na wanasayansi wengine huku akiunga mkono kuwa kuna umuhimu wa kufanya
uchunguzi zaidi.Dkt,Mathews alimaliza kwa kusema"hili ni jambo la
kusisimua lakini hatusemi kwa uhakika kuwa kila anayebeba simu mfukoni
atakuwa na shida ya kizazi."Dkt.Allan Pacey kutoka chuo kikuu cha
Sheffield anasema kuwa wazo hilo la kudidimia kwa shahawa na
kuharibu"DNA" linatokana na mnunurisho wa kielectromagnetiki
zinazopatikana kwenye simu na pengine joto aidha moja kwa moja kutoka
kwenye simu au mnunurisho.Dkt huyo anayefanya uchunguzi wa shahawa bado
hajashawishika akisema ushahidi huo hauna msingi na ataendelea kuweka
simu mfukoni.Aliambia BBC,"kumekuwa na shauku kwa mda kama kuweka rununu
mfukoni kunaweza changia kudidimia kwaubora wa shahawa na nguvu za
kiume kivyovyote."Kumekuwa na habari zisizokuwa na msingi lakini kwa
maoni yangu uchunguzi uliofanywa hadi kufika sasa haujakuwa wa kutosha
kwa sababu wachunguzi aidha hawakuhifadhi shahawa vile inavyofaa ama
wamedadisi matumizi ya simu kati ya wanaume bila kuzingatia mambo
mengine kama mitindo yao ya maisha."Tunayohitaji ni uchunguzi kufanywa
ambapo utumizi wa simu unazingatiwa vile vile tabia zinazoathiri maisha
yao.Hadi pale tutakapo tafakari hayo,nitaendelea kuweka simuyangu katika
mfuko wa mkono wa kulia wa suruali yangu""
Saturday, June 10, 2017
SIMU ZA MKONONI ZAATHILI MBEGU ZA KIUME
About Unknown
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment