Kuna shosti leo kanitumia hii na wanawake wengine wote humu..
yenye kunahitaji kusafishwa kila
siku,Uke unahitaji kusafishwa kwa hali ya juu zaidi mara baada ya siku
za hedhi au tendo la ngono,Uke wapaswa kuwa mkavu wakati wote ute
unakuwepo ukeni ni uchafu usiopaswa kuwa pale Uke haupaswi kuwa na
harufu hata kidogo. Harufu ni ishara ya uchafu au ugonjwa!
Kinachofanyika kutokana na imani hii ni kwamba uke husafishwa kila
siku nje na ndani. Hasa ndani kwa kutumia vidole na:
•Maji ya kawaida, labda vuguvugu
•Maji ya iliki
•Maji ya mchele
•Asali
•Rose water
•Vidonge vya kufyonza uchafu
•Maji yenye dettol
•Maji ya vinegar...
Ukweli ni kwamba:
•Uke ni mfumo unaojisafisha wenyewe kwa ndani na ni sehemu moja ya
mwili wako ambayo ni safi kuliko maelezo, safi kuliko midomo yetu.
Habari ndio hiyo.
•Mfumo huu husafisha damu ya hedhi na shahawa wenyewe, hauhijaji
msaada wa aina yeyote
•Uke wenye afya una bacteria, lactobacilli, ambao ni kawaida kuwepo
humo. Hawa hupambana na vijidudu visivyopaswa kuwepo huko kulinda uke
na mfumo wa uzazi kwa ujumla.
•Uke wenye afya sio mkavu, muda wote una ute usiokua na rangi (kama
maji), mwepesi na unaonata. Uzito, wingi na mnato wa ute huu hutegemea
na mabadiliko ya mwili wa mwanamke. (Jifunze tofauti ili ujue muda
inapaswa kumuona daktari)
•Uke wenye afya una harufu, ambayo ni nzuri, murua na isiyokera J.
Kama harufu itakua kali na inayokera (kama yai bovu) basi uke wako
hauko katika afya njema na unahitaji kumuona daktari.
Madhara ya kusafisha uke kama ilivyoainishwa hapo juu:
Ni kitu kimoja tu kinachopaswa kuingia kwa kibibi……ambacho ni babu
toshaaaaaaaa, vidole na vingine vyote vilivyoinishwa hapo juu it’s a
no no situation na….
Unaporuhusu kitu chochote kisichotakiwa kuingia ndani ya uke wako,
unatoa nafasi ya kuharibu mfumo wake wa asili, na unajua ukishadisturb
mfumo wowote, athari zake ni chain reaction.
•Vidole vyako vinaweza kuwa na vijidudu (kumbuka uke ni msafi kuliko
vidole vyako) vijidudu hivyo vikashamiri na kuwashinda nguvu
Lactobacilli. Ukapata vaginal infections za kila namna.
•Kitendo hiki chaweza kupeleka vijidudu kwenye njia ya mkojo
ukasababisha UTI – Urinary Tract Infection
•Unawaua/kuwaondoa Lactobacilli na kuacha uke wako wazi na hatarini
kwa mashambuizi ya kila aina. Hakuna walinzi!!
•Mfumo wa uke usipofanya kazi vizuri ndio utaona ute mwingi kuliko
inavyotarajiwa au mkavuuuu kabisa.
•Uchafu wowote mwingine unashindwa kusafishwa naturally unalundikana
matokeo yake ofcousre infections na harufu mbaya.
•Amini usiamini ni sababu mojawapo inayoleteleza saratani ya shingo ya uzazi.
•Mashambulizi mengine yanasaabisha utasa (infertility)
•Ute unakauka, na pale unapouhitaji (tenda la ndoa) hautakuwepo na
kusababisha michubuko ambayo inaongeza fursa za maambukizi ya magonjwa
ya ngono.
He? Sasa tusafishe vipi uke kuhakikisha una afya njema?
•Safisha nje tu kila siku unapooga au unapojisikia kwa maji safi na
mikono misafi. Nje ya uke kunahusisha mashavu na katikati yake.
•Waweza kutumia sabuni isiyokua na kemikali kali, japo haishauriwi pia
but Hakikisha sabuni haipenyi ndani kabisa
No comments:
Post a Comment