mimi ni mfanyabiashara,ambapo nilianza na biashara hizi juakali tangu
miaka ya 2009 baada ya kustop chuo nilikokua nasomea bachelor of human
resources kutokana na sababu za ujana zaidi.
Basi baada ya kufanya biashara hizi za juakali huku nikijihusisha na
shughuli zingine za hapa napale njee ya Tanzania katika kitongoji kidogo
kinachoitwa falcon hatimaye nikapata mtaji kidogo
ulionirudisha bongo kufungua biashara
basi nilipofika bongo nikaona ngoja nichukue coaster moja niifanye kwa shughuli za kukodisha.
Basi moja kwa moja niende kwenye mada sasa mana sipo kutoa historia mwisho mniokote mabwe pande.
Nikaanza rasmi kazi hii ya kukodiasha gari yangu aina ya coaster wakati
huo ninayo moja nasafari yangu ya kwanza ilikuwa kwenda marangu.
Hapa sasa ndio penye mambo safari inaanza pale upanga ndugu wameaga
wamemaliza huku mimi na kijana wangu tukiwa tumekaa kwenye gari
tukiwaacha wamalize taratibu zao tupakize mwili (kiroba) tuanze safari
kuelekea kilimanjaro. Basi wakati tumejilalia kwenye gari wakaanza
kuingia wadada wazuri wasafi wanaonekana wana pesa wakaingia kuwahi siti
na wengine wanabadilisha nguo na sisi tukiwa humo. zikaingizwa katoni
za bia na na pombe kali nyingi. mara kiroba kilikuwa tayari kuingizwa
kwenyw gari tukasaidiana na wafiwa kuingiza mwili ndani ya gari. baadae
waendaji wakaingia kwenye gari mlango ukafungwa ac ikawashwa na gafla
story zikabadilika kwenye gari huku wale wa nje wakitupungia mkono kama
ishara ya kututakia safari njema. Story zilizokuwa zinapigwa ndani ndizo
zilizonishangaza kwani ni sikuwa na uzoefu na ni siku chache tangu
ninunue hii gari,basi wakaanza kuuliza Jack Daniel yangu iko wapi
mwingine anaeuliza konyagi yaani ilikuwa kila mtu na kiburudisho chake
huku gospel zikiendela kwenye tv tatu za ndani ya gari.
Hatimaye bagamoyo wakaomba kuchimba dawa sheli huku wengine wakiwa
tayari wamelewa basi tukashuka wote hapo nje full kukumbatiwa mnapewa
sifa sijui za uongo na kweli, mwingine anakuganda mpige story na yeye tu
huku akikuona unaongea na mwingine anakununia flani hv.
Safari inaendelea hadi tunafika hotelin sasa pale ndio pombe ndio
zinanyweka in large scale na watu kulewa hoi.hapa sasa ndio kuna vioja
mwingine anapete mkononi anakuja anakukumbatia kimahaba na busu juu huku
anakuuliza unakunywa nini nikununulie(wadada mkisafirishaga misiba
sijui mnapataga wapi rundo la hela namna ile) basi ikifika saa tano
usiku tunaendelea na safari kuelekea njia panda himo ambapo ndio kituo
kikuu cha kupumzika. basi baada ya kutoka hotelin unajikuta tayari
ushadendeka na wawili bila hata kujijua na mbaya zaidi wengi wanaofanya
hivi ni wananafasi nzuri kimaisha, wengine ni maafisa wa jeshi wengine
unaona kabisa msibani aliletwa na shangingi la kifahari. basi pale
tumiendelea na safari taa za ndani zinazimwa na hakuna anaekumbuka kama
ndani kuna maiti tena maana utakuta wale wamelaliana hawa wanadendeka
mimi mwenyewe naongeleshwa na jinsia za kike tatu tofauti. hadi tukafika
njia panda tukapumzika baadae saa moja asubuhi tukaanza safari ya
kupanda marangu,maajabu tulipofika pale msibaa ukaanza tena vilio kwenye
gari hatari.basi mnashusha maiti mnatulia pale kama robo saa hapa sasa
ndio kila mtu anachukua namba zenu eti wakimaliza kuzika mje kuwafuata
wakalale sehem nzuri. Wakimaliza kuchukua namba sisi tunashuka njia
panda himo kutafuta vyumba vya kulala pale double M lodge.
Basi tukifika double M tunachukua vyumba huku tukiwawekea booking baadhi ya wafiwa waliotuambia tuwaweke vyumba
Naama saa tisa imefika wafiwa wanaanza kupiga simu tuwafuate baadhi waje
kulala kwenyw lodge, hapa sasa ndio patamu, tunawafuata kisha tunarudi
nao njia panda himo bia zinanyweka kupoteza mawazo ya kufiwa huku
wengine wakiwaponda waume zao waliowaacha dar kuwa hawawatoshelezi
kimapenzi, nadhan mnaeza kuvuta picha wadada wakikutana pamoja huku
wakiwa tayari wameshalewa hapa nakwambia mnakuwa na wadada wengine wenye
majina makubwa mjini lakini hapa hutaamini kama ni yeye ndio
yanayomtoka maneno hayo mdomoni. basi sikukaa mda mrefu mwenzangu
akaambiwa amsindikize mfiwa mmoja kubeba katoni za vinywaji kumbe
wameenda kumalizana hukohuko, basi sasa hapa nimebakiwa peke yangu na
sijui niongee na yupi nimuache yupi maana unakuta wengi wako kwenye ndoa
na tayari wote wameingia kingi.
nadhani leo niishie hapa
ila visa ni vingi kuna siku mwenzangu alienda kulala na mtoto wa marehem masaa mawili baada ya kumzika baba yake kule mafinga.
pia hii tabia ya ngono wakati wa kusagirisha misiba iko kwa mikoa yote
ya Tanzania ukienda mbeya musoma bukoba... na hakuna msiba nilioshuhudia
warembo wengi kama msiba wa yule dada aliyeungua gorofani na mpenzi
wake kwenye apartment yake mikocheni tukamsafirisha kibosho.
Pia nilichojifunza mabint wengi wa mikoani hawajawahi kufika dar hivyo
wakijua mmetoka dar ni kama wanakuwa na kichaa fulani kuhakikisha
mnalala wote
karibuni tusikilize bambi bambi ya jidena
Chanzo JF
No comments:
Post a Comment