KARIBUNI wapenzi wasomaji wa safu hii ya mahusiano ambayo huwajia kila
Jumanne na Jumamosi, ikilenga kufahamishana hili au lile kuhusiana na
mambo ya mapenzi, wengine wakiita mahaba.
nigeukie mada ya leo ambayo inajadili suala zima la uhusiano baina ya ngono na mapenzi ambayo ilianzia Jumamosi iliyopita.
Leo nimewaletea maoni ya wasomaji wangu kuhusiana na mada hiyo kama ifuatavyo:
Juliana Mgulu wa Same, Kilimanjaro: Kwa upande wangu, siamini
kuwa ngono ni silaha ya mapenzi na kamwe sitaamini kwasababu muhimu mi
naelewa ilo tendo la ndoa si tendo la wachumba, mi nimesimama katika
imani na mbona niko katika mahusiano muda mrefu na ninafurahia uhusiano
wangu.
Rama wa Kimara kwa Komba, Dar es Salaam: Kwangu ngono ndoyo silaha ya mapenzi.
Doa Vitras wa Dar es Salaam: Unaweza ukawa na mwenzio na msifanye
ngono na mambo yakawa sawa, siku zote ngono ni haja ya kimwili na si
ugonjwa ukamfanya mtu akafa, mapenzi ni hisia na si matamanio ya mwili.
Mujuni wa Ubungo, Dar es Salaam: Kama mnapendana kwa dhati, tendo la ngono lazima ndio kiunganishi.
Nuru Shariff wa Tabata Matumbi, Dar es Salaam: Ngoni sio silaha
ya kukupenda mtu. Hisia za mtu anayekupenda utazijua kwa vitendo vyake
na si tabia. Ngono si mapenzi, wangapi wapo kwenye madanguro na
kujirusha na watu, ina maana wanawapenda?
Bakari wa Kondoa: Ngono ni tendo lakini mapenzi ni zaidi ya
ngono, kama wawili wana mapenzi toka moyoni, ngono si lolote si
chochote. Ngoni ni sawa na kiu ya maji, ukinywa tu basi inakatika.
Mapenzi ni mwili na roho.
Raymond Matenga: Kuwa na mwanamke au mpenzi anayekukatalia kufanya tendo la ngono eti mpaka muoane ni sawa na kusubiri meli uwanja wa ndege.
Maleck wa Sinza, Dar es Salaam: Mtu mwenye mapenzi ya kweli
atakuwa tayari kwa chochote kwa mwenza wake kama anakuwa hataki, basi
ujue anaye wake sio wewe. Ukiangalia hali ya sasa huwezi ukawa
unamuhudumia mwenzio halafu haja zako hakutimizii, huyo hakufai.
Atambue kuwa manjonjo yake na mahaba atakayonifanyia tukiwa faragha,
ndio zitanifanya name ninogewe nimng’ang’anie. Sasa kama hataki
nitajuaje kuwa ni mwanamke aliyekamilika? Au atanijuaje kuwa mume
aliyenaye yupo sawa? Aliye na malengo nawe atakufanyia utakavyomuomba.
Tatizo la madada zetu wa siku hizi wana tamaa sana, pesa mbele kuliko
utu ndio maana kuna anayemfaidisha kimwili na wengine wa kuwachuna. Hata
mimi nimeachana na mwenzangu kwa jambo hilo, hataki kukutana na mimi
kila muda ni mtu ambaye hana muda, siwezi kutoka.
By Lydia wa Same, Kilimanjaro: Ngono sio silaha ya mapenzi
kinachotakiwa ni upendo wa dhati, kama mtu hujampenda kutoka moyoni ni
bora ukamwambia kuliko kumpotezea muda.
Baba Rooney wa Mbalizi Mbeya: Si kweli kuwa mpenzi ambaye hakupi
mapenzi ndio hana mapenzi na wewe. Mbona wapo ambao anakupa mapenzi
lakini hana maepnzi na wewe?
Sylvia Lucas wa Maduka Tisa, Mwanza: Ni kweli mtu akikataa kukutana kimwili huyo hakupendi, yupo anayempenda anakupotezea muda tu.
Athanas K wa Mbande, Dodoma: Ngono ni silaha kubwa katika mahusiano na ndio msingi wa halisi wa mapenzi kwa wawili waliokubaliana.
Wewe unamoani gani?tafadhali tuandikie hapo chini ,zingatia lugha nzuri
No comments:
Post a Comment