Habari yako,
Kutokwa jasho ni jambo la kawaida na jema kiafya ila jasho linapokuwa limezidi hasa maeneo ya usoni huwa kero kubwa. Watu wengine huweza kuahirisha kuhudhuria mambo ya kijamii kutokana na tatizo la kusweat sana usoni.
Kusweat kupita kiasi huweza kusababishwa na mambo mbalimbali ikiwemo baadhi ya magonjwa ( kisukari, shinikizo la damu kutokuwa sawa, hormone/ vichocheo vya mwili kutokuwa sawa na maambukizi mbalimbali ya maradhi), pia saa nyingine husabibishwa na mishipa ya fahamu kugusika kirahisi hata joto linapopanda kidogo sana au unapokuwa na hisia hasa za wasiwasi au stress.
Mtu anaweza kuvumilia kutokwa jasho sehemu zote za mwili lakini usoni huwa ni kikwazo. iwapo unapata shida hii muone daktari ili aweze kugundua chanzo hasa chanzo cha shida hiyo pia uwe wazi iwapo hiyo hali hukupata mchana na usiku pia ili suluhisho lipatikane.
Upande mwingine iwapo hauna shida ya kiafya ila unasweat tu usoni jaribu njia hizi;
Tumia poda (talcum Powder) usoni kuweka uso uwe mkavu
Poda inasaidia kunyonya unyevu na mafuta juu ya ngozi hivyo unaweza kupaka powder kabla ya kuanza kupaka make up.
Epuka lotion nzito na zenye mafuta mazito(heavy creams)
Saa nyingine tunapaka mafuta yanayofanya mtu usweat sana usoni, ukigundua umezidisha kusweat usoni angalia mafuta unayopaka usoni, jaribu kuacha ili uone kama utapata tofauti.
Unaweza kufunga barafu kwenye kipande cha nguo au kitambaa kisha fanya kama unakada au kupaka usoni. Hii itasaidia kupunguza hali ya matundu ya ngozi kufunguka pia inapooza uso wako ili usipata lile joto linalokuletea jasho usoni. Fanya hivi mara mbili hadi tatu kwa siku.
unaweza kusaga tango kidogo uwe kama uji mzito, paka usoni kaa nalo mpaka likauke unaweza kufanya hivi mara mbili kwa siku mpk shida ipungue au iishe.
unaweza kuiweka juice hii hata siku nne katika jokofu (friji)
- Wengine hushauri mtu anywe juice ya nyanya, apake alovera gel n.k
- Pia inashauriwa kupunguza matumizi ya chumvi hasa chumvi ya kuongeza ongeza baadae.
- Jitahidi kunywa maji
- Punguza matumizi ya chai na kahawa, hizi huweza kuchngamsha joto mwilini na kupelekea kutokwa jasho jingi usoni na sehemu nyingine
- Dhibiti ulaji wa viungo vyenye jamii ya pilipili
- Punguza uzito iwapo u mnene sana.
xoxo
No comments:
Post a Comment