Artikel Terbaru

Responsive Ads Here

Wednesday, August 30, 2017

Mahusiano: Usijidanganye, huwezi kumshika mpenzi wako kwa kumpa nyuma (**TIGO**)...maneno matamu mkiwa faragha ndiyo silaha yako..!!



USIJIDANGANYE: Huwezi kumshika mpenzi kwa “kumrusha ukuta”  Mwanaume gani usiyeridhika na mapenzi ninayokupa…? Nimefikia hatua ya kukupa hata mapenzi kinyume na maumbile ili usitoke nje lakini bado, hivi ni kipi ulichokikosa kwangu?” alisikika akipayuka mwanamke huyo.Maneno aliyokuwa akiyatoa yule mwanamke yalinichoma sana. Nikabaini siri moja ambayo nahisi ipo kwa wanawake wengi walio kwenye ndoa na hata wale walio kwenye uhusiano wa kawaida kwamba, wanafikia hatua ya kutoa aina hiyo ya penzi eti ili wapenzi wao wasiwasaliti. Jamani hii inaingia akilini kweli?

Unafikia hatua ya kuhatarisha maisha yako kisa unataka kukamilisha ile sentesi ya kwamba unampa mumeo kila anachokitaka? Huo ni ulimbukeni na kama wapo wanaoendelea kufanya hivyo, wanajitafutia matatizo yatakayowafanya waje kujuta baadaye.

Ni kweli washauri wa masuala ya mapenzi wanaeleza kuwa, ili uweze kumshika vilivyo mpenzi wako unatakiwa kuhakikisha unampatiliza katika kila anachokitaka lakini hawakuzungumzia ishu ya wewe kukubali mapenzi kinyume na maumbile. Hawakurusu hilo kwa kuwa wanajua madhara ya kufanya hivyo. Sasa iweje leo ukubali kufanya dhambi hiyo eti kwa kuwa mpenzi wako kataka na unampenda?

Katika ulimwengu wa sasa wapo wanaume wa ajabu sana. Hawa ni wale ambao si wastaarabu. Wao hawaangalii madhara yanayoweza kuwapata wenzao bali wanaangalia kujifurahisha wao tu. Mbaya zaidi baadhi ya wanawake nao wamekuwa mbumbumbu.

Eti kwa kuogopa kuachwa au kusalitiwa wanasema bora wafanye hivyo. Jamani, ifike wakati tufikirie kila tunalolifanya katika maisha yetu ya kila siku. Zipo mbinu nyingi za kumridhisha mpenzi wako na wala asifikirie kukuacha wala kukusaliti bila hata kumkubalia afanye hivyo.

Pia unatakiwa kufahamu kwamba, unaweza kumpa mpenzi/mume wako mapenzi hayo lakini bado akakusaliti tu. Sasa kwa nini ujidhalilishe?

No comments:

Post a Comment