Artikel Terbaru

Responsive Ads Here

Friday, August 11, 2017

Mwanaume Ukitumia Aina Hii ya Chai Utakuwa Mwanaume Haswa!


Katika blogu hii nimetoa takriaban mada sita (06) zinazohusu vyakula na aina mbalimbali ya mazoezi ambayo mwanaume akizingatia hakika hatokuwa na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume. Mada hizo ni pamoja na: Ongeza Nguvu za kiume kwa Viagra za Asili, Vyakula Vinavyoongeza Hamu na Nguvu ya Kufanya Tendo la Ndoa, Fahamu Aina 7 ya Vyakula Vinavyoongeza Nguvu za Kiume, Vijue Vyakula Hatari kwa Kupunguza Nguvu za Kiume, Fanya Mazoezi Haya kwa Wiki Tatu Kuongeza Nguvu za Kiume na Zifahamu Nutrients na Madini Muhimu kwa Nguvu za Kiume.

Leo nakuletea mada nzuri kuhusu namna ya kutengeneza chai ya viungo vya chakula ambayo mwanaume akiitumia atakuwa na hamu ya kufanya mapenzi na atakuwa na nguvu kubwa za kiume. Chai hii inaboresha shahawa za mwanaume kwa kiwango kikubwa kwa maana ya kuondoa tatizo la mbegu za kiume kuwa na umbo lisilofaa (sperm abnormalities), kuongeza wingi wa mbegu za kiume ndani ya shahawa (sperm count) na kuongeza kasi ya mbegu za kiume kuogelea ndani ya uke wa mwanamke (sperm motility). Chai hii itamfanya mwanaume kuwa rijali haswa kwani atakuwa na hamu kubwa ya kufanya mapenzi (libido), ataweza kuanza na kumaliza tendo bila kuishia njiani hali ambayo inawakera wanawake, inafanya uume kuwa mkubwa na inafanya uume kusimama haswaa kibabe na kufanya mashambulizi maridadi kunako sita kwa sita.

Kabla sijakueleza namna ya kuandaa chai hii napenda niwambie wanaume wenzangu kuwa matumizi ya chai na kahawa yenye caffeine sio nzuri kwao kwani huchangia kupunguza nguvu za kiume na kuzorotisha ubora wa shahawa. Wengi tumekuwa tukitumia chai au kahawa yenye caffeine bila kujua madhara yake kwetu wanaume. Watafiti nchini Italy waligundua kwamba hatari ya mwanaume kuwa na mbegu za kiume zisizo na ubora (unhealthy sperm) huongezeka kadri mwanaume huyo anapozidi kutumia chai au kahawa zaidi kwa siku. Hatari hii pia huwakumba wanaume wanao tumia kilevi (alcohol). Kadhalika wanaume wanaovuta sigara wanakabiliwa na hatari ya kupoteza ubora wa shahawa na upungufu wa mbegu za kiume. Aidha uwezo wao wa kufanya mapenzi (sexual performance) hupungua.

Bila kukuchosha kwa maelezo marefu napenda kukushauri wewe mwanaume kupunguza kabisa au kuachana na unywaji wa chai au kahawa yenye caffeine, uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe usiofaa. Badala yake tumia chai hii ya viungo vya chakula. Ifanye iwe ndiyo chai yako kila siku asubuhi na jioni. Mimi binafsi nimeachana na chai au kahawa yenye caffeine. Natumia chai ya viungo na situmii sukari ya kawaida, natumia asali kwenye chai yangu ya viungo. Nimeona mafanikio makubwa sana na nimeona leo nishiriki pamoja na wewe siri ya mafanikio yangu.

Chai ya viungo, changanya viwango sawa vya unga wa viungo hivi: Tangawizi (ginger), kitunguu swaumu (garlic), unga wa haradali (mustard), pilipili manga, mdalasini, sweet basil, coriander na  kungumanga (nutmeg). Viungo hivi vinapatikana kwa urahisi sokoni au supermarket. Matumizi yake: chukua kiasi cha mchanganyiko wa viungo hivyo weka kwenye maji ya moto na weka asali badala ya sukari. Hata ukikosa sweet basil na coriander sio mbaya lakini hivyo viungo vingine ni MUHIMU SANA!



Ukitumia hii chai hutodanganywa na watu wanaonadi dawa za kuongeza nguvu za kiume, kuongeza hamu ya tendo au kurudia tendo na ubora wa shahawa kwa maana kwamba hutopoteza pesa yako kununua dawa zao! Isitoshe jiulize Je, hizo dawa au tiba zinazouzwa na watu hao ni salama? Zimehakikiwa na watalaamu wa Chakula na Dawa katika nchi unayoishi? 

No comments:

Post a Comment