Artikel Terbaru

Responsive Ads Here

Friday, September 1, 2017

UNAIJUA Dawa ya asili ya fangasi Ukeni???





Fangasi ukeni ni muwasho sehemu ya ndani ya uke ambao unaweza kuambatana pia na kuvimba kwa uke. Leo sitaongelea sana juu ya nini kinasababisha hizi fangasi sehemu ya uke bali tutaona dozi kamili ya asili inayoweza kutibu kabisa tatizo hili linalosumbuwa wanawake wengi miaka sasa.
Tumia dawa hizi 3 zote kwa pamoja ili kupata matokeo mazuri na usiache kuleta mrejesho hapa namna unavyoendelea:
1. LEMONADE
Lemonade inaandaliwa kwa kutumia limau na asali na mdalasini ya unga kidogo, nayo inaandaliwa hivi:
* Chukua asali nusu Lita
*Chukua limau kubwa 12, zikate katikati kila moja. Tumbukiza ndani ya sufuria na weka maji Lita 3, chemsha mpaka limau ziive (zisiive sana), ipua utowe zile nyama nyama za ndani za liamau moja baada ya nyingine, ganda la nje tupa na uchuje kupata juisi ambayo itakuwa na ujazo wa lita 2 na nusu hivi.
Kwenye sufuria nyingine kubwa changanya ile asali nusu Lita na hiyo juisi ya limau Lita 2 na nusu, ongeza maji Safi ya kawaida Lita 2 ili kupata lemonade ya ujazo wa lita 5
Kunywa robo Lita kutwa mara 2 kwa siku 10 hadi 11 hivi.
Unaweza kuongeza vijiko vikubwa vitatu vya mdalasini ya Unga ndani ya hii juisi ya LEMONADE
2. MAZIWA YA MTINDI
Mtindi au bidhaa zitokanazo na maziwa ya mtindi, ni tiba ya kuaminika ya fangasi wa ukeni. Unaweza kutumia njia yeyeote kuweka maziwa ya mtindi au yogati kiasi kidogo labda kijiko kidogo cha chai ukeni wakati wa kulala na asubuhi unajisafisha kama kawaida.
Pia inashauriwa kula tu huu mtindi kiasi cha kutosha kila siku.
Uke wenyewe una uwezo wa kuondoa mabaki yote ya mtindi na kubakisha kiwango kikubwa cha bakteria wazuri (lactobacillus) pamoja na hali ya tindikali yenye uwezo wa kuzuia kujitokeza na kukua kwa fangasi. Bakteria hawa wanaopatikana katiaka mtindi hukusanywa viwandani na huuzwa kama bidhaa ijulikanayo kwa kitaalamu kama “Supplements of Acidophiles”.
3. KITUNGUU SWAUMU
Kitunguu swaumu kina sifa na uwezo wa kuua bakteria na hata virusi mwilini.
*Chukuwa kitunguu swaumu kimoja
*Kigawanyishe katika punje punje
*Menya nusu yake (punje 8 au 10 hivi),
*Menya punje moja baada ya nyingine
*Kisha vikatekate (chop) vipande vidogo vidogo na kisu
Meza kama unavyomeza dawa na maji vikombe 2 kila unapoenda kulala na asubuhi ukiamka tu.
Fanya hivi kila siku kwa wiki 2 hadi tatu. Mama mjamzito chini ya miezi 4 ni vema asitumie, kwa ujumla tu mjamzito uwe makini utakapotumia kitunguu swaumu kwa namna hii kama wewe ni mjamzito.
4. MAFUTA YA NAZI
Kama fangasi hao wa ukeni wanajitokeza hadi sehemu kidogo ya nje ya uke na unapata muwasho pia, hakikisha unapakaa mafuta ya asili ya nazi yaliyotengenezwa nyumbani. Hii dawa tosha kwa fangasi wowote juu ya ngozi.
MAMBO MHIMU YA KUZINGATIA:
Fangasi hii inaweza ikachelewa kupona au ikawa inajirudia hata baada ya kupona kama hutazingatia yafuatayo:
*Kunywa maji mengi kila siku kuanzia glasi 8 hadi 10
*Punguza vyakula vyenye wanga
*Acha kutumia sukari na badala yake tumia asali
*Acha vinywaji baridi, acha pia chai ya rangi na kahawa
*Acha matumizi ya pafyumu hasa maeneo ya huko
*Acha kutumia vidonge vya uzazi wa mpango, hii ni kwa sababu vidonge hivi vinasemwa huwa vinasababisha kushuka kwa kinga ya mwili na kukufanya mrahisi kupata maambukizi ya fangasi.
*Epuka mapenzi kinyume na maumbile
Kama una swali au unahitaji ushauri wowote comment hapo chini sasa hivi nitakujibu

No comments:

Post a Comment