Artikel Terbaru

Responsive Ads Here

Friday, September 1, 2017

Wanawake Hebu Tujitahidi Sasa Kujishusha Kwa Wanaume Wetu Ili Kunusuru Hali



Nianze moja kwa moja kwenye mada. Ni kweli maisha ya sasa ya mahusiano na ndoa kwa ujumla hapo tete sana.

Sasa wanawake wenzangu, si vibaya tukakaa chini na kufikilia nini chanzo. Japokuwa sisi wanawake tunavumilia mengi kwenye mahusiano na ndoa kwa ujumla, lakini tuna jukumu na nguvu kubwa kunusuru mahusiano yetu na kuishi kwa amani na furaha.

Tujitahidi yafuatayo:

1. Tusiwe watu wa gubu
Wanaume wengi hawapendi mwanamke mropokaji, mjuaji, mkorofi. Tujishushe!

2. Tupende ndugu wa mume
Hili nalo ni changamoto sana. Mara nyingi sana huwa tunajisahau, tunaona ndugu wa mume ni maadui zetu. Mama mkwe si adui, hapana tuwapende. Hata wao wakiwa miiba kwetu tujishushe wataona aibu na tutaenda sawa.

3. Heshima 
Hakuna kitu kizuri kama Heshima, nawaambia. Mwanaume yeyote anapenda kuheshimiwa kwani 'naturally' iko hivyo. Mwanaume ni kichwa cha nyumba, yatupasa kuwatii na kuwaheshimu.

Inapotokea Mungu kakubariki na kipato zaidi ya mume au mwenza wako, hiyo isiwe tiketi ya ujeuri, kuchelewa kurudi nyumbani wala vurugu.

4. Uaminifu
Hii ni kubwa kuliko yote. Asikudanganye mtu, uaminifu ni kitu kikubwa sana. Uaminifu unapopotea mwanaume anakuacha! Mwanaume anaweza akakuvumilia yoooote but faithfulness is one among those things men need from you!!

5. Mapenzi 
Hapa naongelea mapenzi kwa ujumla jinsi unavyomhandle mpenzi au mume. Mfano:- katoka kazini, hata akiwa mbali umemuona mpokee chochote alichobeba hata gazeti. Mvue viatu, ikiwezekana mchumu kidogo(" pole mpenzi Wangu kwa kazi"). Hiyo itamfanya ajisikie vizuri sana na kuondoa stress. Hawa waume, wapenzi wetu msiwaone hivyo, wanaumiza sana kichwa kwa ajili ya future zetu na watoto hivyo tuwaenzi.

6. Mapenzi ya kitandani
Hii ilitakiwa iwe ya kwanza. Iko hivi, kitu cha kwanza mwanaume anachofuata kwa mwanamke yeyote ni hiyo starehe, mengine yanasindikiza tu. Sasa ewe mwanamke mwenzangu unayelemaa kitandani, hujibidishi, hukatiki viuno, umelala tu, unaiua ndoa yako au mahusiano yako mwenyewe.

Jitahidi uwe mchezaji hodari. Ukiwa uwanjani hapo sahau yote hakikisha anaomba maji ya kunywa. Naelewa wapo wanaume waliojaaliwa na wasiojaaliwa nikimaanisha mihogo ya Jang'ombe na vibamia. Kama ana kibamia siku hizi kuna utaalamu mwingi nasikia, kibamia kinaweza nenepa(fuatilia). Usiache kumfurahisha kitandani eti ana kibamia wala usimwonyeshe kama hakikukuni bali jitahidi hivyo hivyo huku moyoni ukiapa kumtafutia dawa ya kuinenepesha( zipo sana) uvivu tu wa kufuatilia.

7. Usafi 
Asikuongopee mtu, mwanaume yeyote hapa duniani anavutiwa na mwanamke msafi kuanzia chumbani, nje ya nyumba na mwilini. Mfanye mumeo awahi kurudi nyumbani, kila wakati nukia marashi au spray au perfume. Vitu hivi siku hizi vinapatikana tena at an Affordable price.

8. Ubahili
Sawa najua, mwanaume kama kichwa cha familia ni wajibu wake atunze, ahudumie nyumba. Jamani hata kama mada zangu nyuma nimewatetea sana wanawake wenzangu lakini kutokana na hali ya maisha ya sasa, na hasa kama ewe mwanamke una kibarua chochote, tafadhari sana wekeni mezani mnachopata kwa jili ya kuboresha maisha yenu. Usimkomoe mwanaume, lenu ni moja.

9. Kumsikiliza mpenzi/mume
Kila wakati mume au mpenzi anapotaka kuongea na wewe hebu hayo masimu yazime, acha kila kitu msikilize. Imekuwa kawaida sana mume anaongea wewe upo busy unachati, hivi ndugu yangu unajipenda kweli wewe au ndo umefika tena hapindui? Ukiachwa oooh nimerogwaaaa, Wapiii umejiroga mwenyewe. Respect ni muhimu.

10. Ibada
Mwanamke mwenzangu, unapopitia magumu yooooooote kwenye ndoa au mahusiano Usimwache Mungu. Mahusiano au ndoa huzaa familia na familia hutoka kwa Mungu. Sali sana kwa imani yako.

Nakwambia ukweli, ipo nguvu kubwa katika kumtegemea Mungu. Hebu anza leo kuomba, kuhudhuria ibada na kusoma biblia mambo yote yatanyoooka.

Amen!

No comments:

Post a Comment