Nikiwa safari kuelekea Nairobi nilifanikiwa kuonana na mama mmoja Mchaga aliyefanikiwa sana. Ana hoteli Arusha, Moshi na pia ana export kahawa.
Nilijiuliza sana huyu mama amewezaje?
Ikabidi nianze kumchimba.
Aliponiambia wanaume ni Malighafi, nilishtuka sana. Nikaomba anidadavulie ....
G: Unasemaje ? Wanaume ni malighafi? Sikuelewi? Una maana gani?
M: Usinielewe vibaya, kwanza inabidi ujue maana ya malighafi. Nadhani unajua malighafi ni nini. Malighafi ni bidhaa inayohitaji kuongezewa thamani ili upate faida zaidi. Au unahitaji kuisindika kabisa ili iwe na thamani kwa faida yako.
Mimi kama mwanamke kwangu mwanaume ni malighafi inayotakiwa kuongezewa thamani kwa faida yangu.
G: Sijakuelewa kabisa mama.
M: Sisi wanawake tuna nguvu isiyo kawaida. Mungu akikupa mwanaume, ni kama malighafi ...unatakiwa kuongeza thamani, kumtengeneza unavyotaka kisha unamtumia kuwa unavyotaka. Mwanamke anaweza kumwamsha mwanaume aliyelala na kumfanya kuwa Rais, au mwanamuziki mkubwa halafu anaweza kumtumia kuwa anavyotaka. Wanawake wa siku hizi, wakipewa mwanaume wanataka awe amekamilika yaani finished product ili wamtumie. Huo ni ujinga. Wanawake tumeumbwa kuhamasisha. Tumeumbwa kumpandisha mwanaume. Mwanaume ni kichwa lakini kwenye familia mwanamke ni moyo.
G: Bado sijakupata kabisa.
M: Ngoja nikupe mfano. Mume wangu mimi alikuwa mwanafunzi wa chuo nilipokutana naye, mlevi na asiyejielewa kabisa. Lakini kuna kitu cha tofauti nilichogundua...alikuwa na akili. Kwangu ilikuwa ni malighafi yenye utajiri. Nikapiga mahesabu yangu, nikaingia kwenye mahusiano. Nikampa anachokitaka akapagawa. Kisha nikashika usukani. Nikatafuta njia akaacha pombe, akawa msomaji sana mpaka akafaulu chuo kikuu. Amemaliza uinjinia, nikampelekesha akanioa. Ninamjua wapi pa kumgusa. Alipomaliza chuo, nikamwambia sitaki awe mwajiriwa akagoma. Uoga. Nikamwacha, mshahara ulipoanza kuingia nilishika mimi .... Nikimpa anatumia pombe. Nikaanza kuchukua akiba yeye bila kujua, nikanunua mashamba, viwanja, nikaanzisha mgahawa. Nikamwita kama mgeni rasmi kuja kuzindua. Nikampeleka kwenye mashamba niliyonunua. Akapagawa. Nikahamisha akili yake yote, kwangu.
Tukaanza kushirikiana pamoja mpaka tukasimamisha hoteli. Mume wangu alikuwa hapendi biashara lakini baada ya kumbadili akapenda biashara kunizidi. Unajua nini kilitokea. Aliacha kazi na kuweka nguvu kwenye hoteli ndogo, tukafanikiwa mpaka hoteli kubwa ikajengwa.
Mashamba zaidi yakanunuliwa. Watoto wetu wanasimamia biashara zetu. Mume wangu ni mpambanaji hatari kwasasa. Unajua kwanini? Kwangu alikuwa ni malighafi, nikaamua kuongeza thamani.
G: Aisee!! Eeh?
M:Wanawake wa siku hizi wanatafuta wanaume walioongezewa thamani, ili wawatumie. Ukiona mwanaume yupo juu fahamu kuna starring nyuma ya pazia aliyesababisha. Mwishoni wanatumika wao kama vyombo vya kujistarehesha na kutupwa. Mwanamke unatakiwa kuwa na akili mara nne ya mwanaume, na usijivune kama una akili. Ukikuta mwanaume ana akili na unajua unaweza kumtengeneza chukua na ongeza thamani.
Ukichukua kilichoongezwa utapigwa tu. Utaachwa. Wewe unayesubiri mwanaume wako atengenezwe na wengine ili ule vya dezo. Ukitendwa, ukitupwa na kuchakazwa, usilie. Ongeza thamani ya malighafi yako.
Mfano kama mimi mchaga nikiolewa na mwanaume ndani ya miaka mitano hamjajenga, asihukumiwe mwanaume. Mwanamke ndiyo kimeo. Kama ukishindwa kumbadili mwanaume awe unavyotaka either hujapendwa, au wewe ni mvivu mpenda dezo, au hujui nguvu ya mwanamke kwa mwanaume au mwizi au mbinafsi au umejisahau kuwa ndoa ni ujasiriamali kama ujasiriamali mwingine.
Mwanamke ni msababishaji, uliza matajiri wakubwa duniani. Uliza watu wakubwa maarufu, uliza akina Napoleon, uliza akina Obama, uliza akina Albert, uliza utajua....nyuma yao kuna nguvu inayosababisha mambo makubwa.
COPIED FROM SOMEWHERE..!
No comments:
Post a Comment