Artikel Terbaru

Responsive Ads Here

Saturday, March 24, 2018

Inauma sana: Mke wa jirani yangu anachepuka

Juzi nikiwa nimekosa usingizi mnamo mida ya saa saba usiku nilisikia mwanamke akilalamika kimahaba baada ya muda wakaanza maongezi.

Sasa basi nikaja kugundua ni mwanamke ambaye ni jirani yangu ambaye ana mtoto wa miezi 8 mume wake anafanya kazi Kigoma yeye mwanamke yupo Kibaha ambapo yeye anasimamia hii nyumba niliyopanga na duka la vifaa vya ujenzi.

Nikajiuliza maswali inamaana mume wake amerudi? Najua huwa akija nilazima aje kutusalimia wapangaji wake, basi bwana kulivyopambazuka mida ya saa kumi na mbili jioni nikamuuliza mtoto wa huyo mama kimtego kwamba ulikuwa unataka kitabu cha story kwani hujawahi kumwambia baba yako?

Mtoto akanijibu mpaka akirudi mwezi wa kumi na mbili atakapo pata likizo, kimoyo moyo nikajua kumbe mama yake amelala na mchepuko yaani nilijisikia vibaya mno, sasa juzi kati nikamuita huyo mama akashituka kweli kweli nikamwambia nataka kujua bili ya maji ndio nikamuona anatulia.

No comments:

Post a Comment