Artikel Terbaru

Responsive Ads Here

Saturday, April 21, 2018

ABOUT LOVE# Usiruhusu Mumeo Afanyiwe Masaji na Mwanamke Mwenzio....Check Ou

Inabidi sasa wanawake tuanze kuwapa somo wenyewe manake inaonekana hamfundishani kabisa. Sababu kila kukicha Mambo ni yale yale.
Wanawake mmekuwa na tabia mume akikueleza anajisikia vibaya,mwili unamuuma haraka unamwambia nenda hospitali au unakwenda kumnunulia panadol apunguze maumivu, Mnakosea kabisa.
Kumbe daktari au nesi au mtabibu ni wewe mwenyewe, hebu nikupe siri moja wala usiniulize mchaichai nitaupata wapi, kwani uko mwingi sokoni na kwenye maduka ya dawa za asili. Chukua nazi zako, zikune halafu chuja taratibu mpaka upate tui zito, pika mafuta ya nazi, ule muda ambao tui lako liko jikoni chukua majani ya mchaichai changanya kwenye tui hilo wakati linachemka changanya na mdalasini pamoja na hiriki, acha tui lichemke mpaka ligande. Likishaganda unatoa mafuta mazuri yanayonukia kisha chuja na uweke kwenye chupa safi.

Muinue mumeo kamuogeshe, ikiwezekana hata kumbeba mbebe, mwanaume si mzito hata akiwa na uzito wa tani tano huwezi kushindwa kumbeba,mbona mkiwa kwenye mahaba uzito huuoni? Mume anafanyiwa kila linalowezekana ilimradi liwe halali kwa Mwenyezi Mungu. Mwanaume ni bahati, hawapatikani kilahisi. Hakikisha mume unamshikilia asikuponyoke. Siku hizi wanaume tumekua adimu hadi tunagombaniwa, walio na moyo mwepesi wanajichoma visu wengine wanakunywa sumu, unabaki unajiuliza kwani anayo ya dhahabu? Mwanaume ni zawadi kutoka kwa Mungu. Na siri ya tungi aijuaye kata.


Sasa mbebe mumeo kisha kamuogeshe na baada ya hapo mkaushe kwa taulo laini siyo kwa kanga na usimsugue, taulo lina manyoya yake ambayo ni malaini na ni maalum kwa ajili ya kufutia maji, kanga inasugua ngozi si salama sana pia kwa sababu inatoa rangi.


Baada ya kukausha maji chukua mafuta yako umpake mwili mzima kisha fanya masaji taratibu, baadhi ya wanawake wanawapeleka waume zao kwenye vituo vya masaji wakafanyiwe masaji ya mwili, hivi kwa nini mumeo akashikweshikwe na mwanamke mwenzako wakati ufundi wewe unao?

Kama huna ndiyo huu nakupa.

Mpapase taratibu mumeo huku unamfanyia masaji, fika mpaka kwenye milima ya gorani, teremka taratibu kwenye bonde la Sinai, hapo sasa utakapofika kwenye bonde hilo sidhani kama maumivu yatakuwepo, lazima atataka chakula cha usiku hata kama itakuwa mchana atataka cha usiku tu Mlishe usimnyime chakula. Mimi nawasaidia Mahusiano yasiwashinde. Unashangaa mwenzio anadumu kwenye mahusiano unaanza kusema kaenda kwa mganga kumbe hujui anayo mfanyia Mpenzie. Chukua hatua. 


Watakucheka watu ukiachwa, Mara Nyingi Huko Kwenye Vituo vya masaje Mwanaume akiwa anafanyiwa hiyo masaje na Mwanamke ikilolea atataka na papucha...Shauri Zenu

No comments:

Post a Comment