Ngono kinyume na maumbile au wengine husema Ngono kwa njia ya haja kubwa,
ni hali ya kingono ambayo mhusika huingiza uume katika njia ya haja
kubwa kwa lengo la kufanya mapenzi kwa njia hiyo ili kujiridhisha hisia
zake.
Watu ambao wanajishughulisha na kushiriki katika ngono
ya njia hii ya kinyume na maumbile wapo katika hatari kubwa ya kiafya,
kwa sababu njia ya haja kubwa inazungukwa na mishipa/neva nyingi sana
zipo eneo hilo ambalo kazi zake si maalumu kwa tendo la ngono kwa
kuingiziwa kitu ambacho hakistahili eneo hilo.
Ambapo kwa
utafiti uliofanyika Nchini Tanzania uliohusisha wasichana na wanawake wa
rika kuanzia miaka 15 na kuendelea na iliyohusisha kada tofauti katika
jamii kama wanafuzi, wafanyakazi, wahudumu wa baa, wauguzi, makahaba na
kina mama wa majumbani katika maeneo tofauti. Watu waliojitokeza ni 903
wakiwemo pia wanaume walihusika katika tafiti hiyo.
Utafiti
huo ulisema wanawake 44 kati ya 166 waliohojiwa walisema kuwa wamewahi
kufanya tendo la kujamiiana kinyume na maumbile ambao ni sawa na
asilimia 27 huku asilimia 73 ya waliohojiwa walidai kufahamu njia hiyo
ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile, katika Utafiti huo ulifanywa na
Irene Mremi kutoka Taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu Nchini
Tanzania.
Pia, Inakadiriwa kuwa asilimia 90% ya wanaume
wanaofanya ngono na wanaume wenzao (mashoga) huwa wanajihusisha na ngono
kinyume na maumbile.
JE, NGONO KINYUME NA MAUMBILE NI SALAMA?
HAPANA, Ngono kinyume na maumbile si salama kwa sababu ina madhara mengi kiafya kama yafuatavyo;
MOJA, Njia ya haja kubwa haina vilainishi/lubrication asilia kama jinsi Uke ulivyo.
Hivyo
wakati wa tendo la ngono husasani wakati wa uingizaji wa uume huwa
inasababisha kuchubuka kwa tisu/ngozi laini ndani ya njia ya haja kubwa
hiyo, na hivyo kupelekea michubuko ambayo bacteria, virusi na hata
vimelea vingine kuweza kupenya wakati wa majeraha hayo ya michubuko na
hivyo kuingia katika mfumo wa damu kupitia majeraha hayo.Hii inaweza
kusababisha kuenea kwa magonjwa ya zinaa pamoja na VVU.
Tafiti
zinaonyesha ya kuwa Ngono kwa Njia ya haja kubwa ipo katika hatari
kubwa ya maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa zaidi ya asilimia 30%
kuliko watu wanaotumia njia ngono kwa njia ya Uke.
Vile vile
mtu anakuwa katika hatari kubwa ya kupata virusi vya human
papillomavirus (HPV ) ambavyo huweza kumpelekea mtu anayejihusisha na
ngono kinyume na maumbile kupata muwasho katika eneo hilo la haja kubwa
na hata kupelekea kupata kansa.
PILI, Tishu ndani ya njia ya
haja kubwa, haijakingwa na kulindwa kwa ngozi ngumu kama ilivyo sehemu
za nje za mwili. Tishu zote za nje ya miili yetu zina ngozi ambayo ni
seli zilizokufa ambazo hutusaidia kutukinga dhidi ya maabukizi ya
vimelea na vile vile hutulinda na vitu tofauti katika mazingira.
Hivyo
ndani ya njia ya haja kubwa hakujakingwa na ulizi huo wa asili wa seli
hizo ili kuweza kuhimili, hivyo kuifanya iwe katika hatari kubwa ya
kusuguliwa na hivyo kuchanika ambayo hupekea kusababisha maambukizi kuwa
rahisi kutokea.
Pia ngozi ndani ya njia ya haja kubwa iko
tofauti na ile ya ukeni ambapo ngozi ya ukeni huweza kuhimili ile
misuguano pasipo kuweza kusababisha michumbuko kwa sababu ya vilainishi
asili vinavyoatikana ndian ya uke na gozi husika.
TATU, Njia ya haya kubwa ni Maalumu kupitisha Kinyesi tu.
Kwa jinsi ambavyo njia hii imeundwa ama kutengenezwa ni maalumu kwa kuhimili na kupitisha kinyeshi tu na si vinginevyo.
Njia
ya haja kubwa imezungukwa na kama misuli mfano wa ringi ama kwa
kitaalamu huitwa (Anal sphincter) ambayo kazi yake ni kukaza eneo hilo
kabla na baada ya kujisaidia tu.
Kipindi ambapo misuli hiyo
(anal sphincter)imekazwa ama kubwa kwa kuingiziwa kitu kingine kigumu
huweza kusababisha maumivu makali kwa muhusika.
Panapoendelea
kuwa na mrudio wa mara kwa mara wa ufanyaji wa Ngono kwa njia hii ya
haja kubwa ama kinyume na maumbile hufanya misuli hiyo ya njia ya haja
kubwa kuwa dhaifu ama kulegea na isiwe na uwezo tena wakukaza kama kazi
yake inavyotakiwa kufanya. Na hivyo kuwa vigumu kuweza kuzuia kinyesi
kuweza kupita mpaka utapokuwa tayari kuweza kukitoa hivyo kusababisha
utokaji ovyo wa kinyesi.
NNE, Njia ya haja kubwa imejaa bacteria wengi.
Njia
ya haja kubwa imejaa bacteria wengi sana tofauti na Ukeni kulivyo hata
kama wapenzi hawana maambukizi yeyote ya zinaa au ugonjwa wowote
bacteria huwa wapo tu eneo hilo na hawa ni bacteria wa kawaida (Normal
flora).
Mtu anapokuwa naingiza uume ndani ya njia ya haja
kuwa anakuwa anaingiza vimelea vingine vya bacteria katika eneo hilo na
wanapokutana na wale bacteria wengine waliopo katika eneo hilo
husababisha madhara.
Pia pale unapohamisha uume toka katika
njia ya haja kubwa na kupeleka katika Njia ya Uke badi bacteria hao
utawapeleka katika eneo Uke ambapo Njia ya haja kubwa inakuwa na
bacteria wengi na hivyo kupelekea maambukizi ukeni na pia maambukizi
katika njia mkojo.
Ngono kwa njia ya haja
kubwa inaweza kusababisha madhara mengine kwa afya ya watu
wanaojihusisha na Njia hii ya ngono na wanaweza kupata madhaara kama
haya yafuatayo,
Pale mdomo unapogusana na njia ya haja kubwa
au kugusa uume uliotoka kwenye njia ya haja kuwa kwa mdomo kunaweza
kupelekea kupata kwa wote mtu na mpenzi wake kuwa katika hatari ya
kupataa magonjwa ya HEPATITIS C, HERPES/ malengelenge, kupata virusi vya
human papillomavirus (HPV) na maambukizo mengine.
Hata
hivyo, majeraha makubwa wakati wa ngono kwa njia ya haja kubwa mara
nyingine ingawa sio kila mara hali hii kutokea inaweza kupelekea Damu
kuvuja kwa ndani (hemorrhoids) baada ya tendo hilo kufanyika ambalo
inaweza kusababisha au kupasuka ama kuchanika kwa misuli/nyama ndani ya
njia ya haya kubwa kwa sababu ya msuguano mkali na muda mwingine
hupelekea kuweza kutoboka kwa utumbo mpana(colon) hii huweza kwa ni
tukio la hatari zaidi ambalo huhitaji msaada wa kitabibu haraka kwa
matibabu na hata kufanyiwa upasuaji zaidi na hata kupoteza maisha
kunaweza kutokea.
TANO, pia kwa wanawake wengi
wanaofanya ngono kinyume na maumbile wamekuwa wakipata shida wakati wa
kujifungua kwa misuli yao kushindwa kuhimili kukaza kwakati wa kusukuma
mtoto na hivyo inaweza kupelekea utokaji wa kinyesi wakati wa kusukuma
mtoto. jambo ambalo huleta tabu kwa wahudumu wa afya kwa kutumia muda
mwigi kuwahudumia.
Njia pekee ya kuepuka kabisa hatari hizo za ngono kinyume na maumbile ni kuacha kabisa ngono kwa njia hiyo ya haja kubwa.
shiriki
katika ngono kwa njia ya kawaida na ikibidi kwa kutumia kondomu ili
kujilinda dhidi ya kuenea kwa maambukizi ya magonjwa ya zinaa.
Kuepuka kuingiza uume ndani ya uke na kisha mdomoni ikiwa uume ulikuwa umeingizwa katika njia ya haja kubwa.
Ikiwa
umepata michubuko na kutoka damu baada ya ngono ama vidonda karibia na
njia ya haja kubwa na hata katika maeneo ya uke basi onana na daktari
wako haraka iwezekanavyo ili upatiwe tiba hii iakusaidi kuzuia
maambukizi ya vimelea katika eneo la jeraha.
MADHARA ANAYOWEZA KUYAPATA MWANAUME ANAYEPENDA KUJIHUSISHA NA MCHEZO HUU WA NGONO NI KAMA IFUATAVYO;
KWANZA,
Kunauwezekano wa Njia ya haja ndogo kuziba kiasi au kuziba kabisa kwa
sababu ya vimelea kuingia na kuziba ama kuingia kwa kinyesi katika njia
ya haja ndogo hivyo kukuweka katika wakati mgumu utapohitaji kujisaidia
haja ndogo.
PILI,unaweza kupata magonjwa ya saratani(kansa) ya tezi tezi Prostate gland
TATU,Maambukizi
ya Virusi vya ukimwi kwa sababu kuna uwezekano mkubwa sana wa kupata
maabukizi tofauti na kwenye njia ya Uke hii ni kutokana na kuwa na
uwezekano mkubwa wa kupata michubuko kiurahisi
NNE, Kuathirika kisaikolojia hivyo mhusika kuandamwa na msongo wa mawazo kila wakati kujutia tendo hili baya.
Nina
imani ndugu msomaji wa makala hii umeweza kuona madhara mabaya sana ya
tabia hii mbaya. Inawezekana umezoea mchezo huo wa kuwaingilia wenzako
ama kuingiliwa kwa namna hiyo na kuona raha lakini umeziona hasara zake,
amabazo kwa hakika kama wewe ni mmoja wao, unatakiwa kuacha mara moja
kwa vile mwisho wake ni majuto na mateso.
Jiepushe na kuiga
mambo bila kujua hasara zake, pia usimtie mwenzako majaribu kwa
kumlazimisha kufanya kitendo hiki na wanaume kwa kigezo cha kuachwa kwa
lengo la kuwaingilia kinyume na maumbile kwa kuwatishia kuwaacha kama
watakataa.
Kipi bora kuharibiwa ama kuachwa? Jibu unalo mhusika!!
Kumbuka
baada ya kuharibwa thamani yako inashuka mbele ya jamii. Kasha
kupelekea kuingia katika msongo wa mawazo na mateso ya ugonjwa ama
magonjwa utakayoyapata baada ya kukubali kuingiliwa kinyume na maumbile.
UKWELI MCHEZO HUU UMEWAATHIRI SANA WANAWAKE AMBAO WENGI WANAUJUTIA.
JIEPUSHE NA NGONO KINYUME NA MAUMBILE!!!!
No comments:
Post a Comment