Kesi ya wanaume
kupungukiwa nguvu za kiume zimezidi kushika kasi, kiasi cha kufanya
dawa za kuongeza nguvu hizo kuwa maarufu na zenye mahitaji makubwa
katika jamii.
Waganga
wa kienyeji wamekuwa wakitumia dawa hizo kama tiba ya msingi ya
kuwavutia wateja kwenye biashara zao. Hii inaonesha kuwa tatizo hili ni
kubwa miongoni mwa wanaume wengi katika jamii yetu.
Hata
hivyo, utafiti unaonesha kwamba wengi kati ya wanaume waliowahi kutumia
dawa za asili na zile za hospitali kuondokana na tatizo la upungufu wa
nguvu za kiume hawakufanikiwa kupata tiba ya kudumu, matokeo yake
wamegeuzwa kuwa watumwa wa kila wanapotaka kushiriki tendo lazima wabwie
‘kolezo’ la kuwasaidia kuamsha hisia zao.
Kwa wanaume, ukosefu wa nguvu ni jambo linalouma
na kuondoa kabisa ujasiri. Wengi kati yao wako tayari kutumia pesa na
uwezo wao wote kuhakikisha kuwa heshima ya tendo la ndoa ikuwa katika
miliki yao daima.
Lakini,
watafiti wa masuala ya mapenzi nikiwemo mimi, tumegundua kuwa wengi
kati ya hao wanaolalamika kupungukiwa nguvu za kiume, hawafahamu chanzo
cha matatizo na namna wanavyoweza kuepukana na kasoro hizo.
Ushahidi
uliopatikana kwa waathirika wa tatizo hili, unaonesha kuwa wanaume
wanapokabili upungufu wa nguvu za kiume huishia kujuta na kujilaumu
wenyewe bila kutazama upande wa pili wa washirika wao, namaanisha
wanawake.
Zipo kesi za wanaume kujiua au kujinyofoa sehemu zao za siri kwa sababu ya kushindwa katika tendo la ndoa. Hali hii inatoa picha kwamba wanaume wengi hujitwika mzigo wa lawama wenyewe.
Dokta Bianca P. Acevedo kutoka Chuo Kikuu cha California, Santa Barbara anasema,
wanawake huchangia kwa kiasi kikubwa tatizo la upungufu wa nguvu za
kiume, jambo ambalo nami nalithibitisha kwa ushahidi wa kitaalamu
ufuatao:
1: KAULI
Miongoni
mwa mambo ambayo mwanaume hataki kuyasikia yakitoka kwenye kinywa cha
mwanamke ni kuambiwa HAWEZI TENDO LA NDOA. Mwanamke akimwambia mwanaume
wakati au baada ya tendo kuwa hawezi, atakuwa amemsababishia tatizo
kubwa la kisaikolojia ambalo litampelekea kupotea nguvu za kiume
taratibu.
Msaada unaohitajika kwa mwanamke anayekutana na mwanaume dhaifu kwenye tendo si kumwambia hawezi, bali ni
kumtia moyo na kumsaidia kuweza. Wanawake wamewasababishia waume zao
upungufu wa nguvu za kiume kwa kuwaambia maneno kama haya: “Yaani siku
hizi sijui umekuwaje, yaani huwezi kazi kabisa!”
Wanawake
wengi hasa waliopo kwenye ndoa, wanapuuza ujuzi kwenye tendo la ndoa.
Hawajishughulishi kumsaidia mwanaume ‘kuwika’, si wabunifu na watundu,
jambo hili humfanya mwanaume kushiriki tendo kwa kutegemea kupanda kwa
hisia zake mwenyewe, hivyo anapokuwa amechoka au ana mawazo, hawezi
kusisimka kwa vile hapati ushirikiano toka kwa mwenzake.
Mwanamke
anapokuwa si msafi, huweza kumsababishia mwanaume matatizo ya upungufu
wa nguvu za kiume. Sote tunafahamu umuhimu wa usafi wa mwili na kero za
uchafu wakati wa tendo, hivyo ni wazi kuwa mwanamke akiwa mchafu
atamfanya mwanaume apoteze msisimko na uwezo wa tendo la ndoa. Unadhifu
wa mavazi na mwili ni muhimu sana katika mapenzi.
Jambo
lingine linaloweza kumsababishia mwanaume upungufu wa nguvu za kiume ni
gubu au karaha za maneno ya uchokozi yasiyokuwa na kichwa wala miguu.
Uchokonozi wa mambo, ugomvi, usaliti na hali ya kutokuwa na staha ni
mambo yanayosababisha tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.
Tabia
ya usaliti kwa mwanamke ni chanzo kingine cha mwanaume kupata tatizo la
upungufu wa nguvu za kiume. Mwanaume anapoona, kuhisi au kubaini kuwa
anasalitiwa, huumia sana moyoni, maumivu ambayo hatimaye humfanya
muhusika kuwa na mawazo mengi ambayo humuondolea hamu ya tendo.
No comments:
Post a Comment